Pendekezo la timu ya kampeni ya CHADEMA kwenye uchaguzi wa marudio Sumbawanga

Wakuu wote heshima mbele,
Kama tunavyojua miezi michache ijayo CHADEMA itaingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Ubunge wa Jimbo la Sumbawanga. Ni muda muafaka tutafakari kwa pamoja na kumshauri Katibu Mkuu wetu Dr. Willbrod Slaa namna atakavyounda timu ya kampeni hususani timu kuu ya kuratibu Kampeni za Chama. Hapa chini nimejaribu kuweka altenative nane (Plan A to Plan H). Tujaribu kuchagua Plan moja au kufanyia maboresho ili tuikabidhi majukumu ya Kikampeni huko ya huko Sumbawanga.

Chini ya hizi Plan kuna Kamati yetu ya Ufundi (Evaluation & Monitoring Team) ambayo kimsingi hii inabaki kama ilivyo kama tulivyokuwa tunaitumia katika chaguzi zilizopita. Pia timu ya Washauri (Consultants). Hii nayo itabaki kama ilivyo kama tulivyokuwa tunaitumia kwenye chaguzi zetu za nyuma. Tujikite kupembua ni "Plan" ipi inafaa au kama haipo basi tutoe mapendekezo kwa Chama, ni timu gani unayoona itafaa kuituma Sumbawanga kufanya Kampeni na tuibuke na ushindi mnono.


PLAN A
1. Kampeni Meneja - Peter Msingwa
2. Naibu Kampeni Meneja - Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu
3. Kamanda wa Operesheni - Godbless Lema
4. Naibu Kamanda wa Operesheni - Ally Banaga

PLAN B:
1. Kampeni Meneja - Vincent Nyerere
2. Naibu Kampeni Meneja - Meshak Opulukwa
3. Kamanda wa Opereshini - Mwita Waitara
4. Naibu Kamanda wa Operesheni - Joshua Nassari

PLAN C:
1. Kampeni Meneja - Godbless Lema
2. Naibu Kampeni Meneja - Peter Msingwa
3. Kamanda wa Operesheni - John Heche
4. Naibu Kamanda wa Operesheni - David Silinde

PLAN D:
1. Kampeni Meneja - Tundu Lissu
2. Naibu Kampeni Meneja - Vincent Nyerere
3. Kamanda wa Operesheni - John Mrema
4. Naibu Kamanda wa Opereshini - Msafiri Mtemelwa

PLAN E:
1. Kampeni Meneja - Ezekiel Wenje
2. Naibu Kampeni Meneja - Godbless Lema
3. Kamanda wa Opereshini - Benson Kigaila
4. Naibu Kamanda wa Opereshini - Tumaini Makene

PLAN F:
1. Kampeni Meneja - Mabere Marando
2. Naibu Kampeni Meneja - John Mnyika
3. Kamanda wa Opereshini - Halima Mdee
4. Naibu Kamanda wa Opereshini - Joshua Nassari.

PLAN G:
1. Kampeni Meneja - Israel Natse
2. Naibu Kampeni Meneja - Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu
3. Kamanda wa Operesheni - David Silinde
4. Naibu Kamanda wa Opereshini - Tumaini Makene

PLAN H:
1. Kampeni Meneja - Vincent Nyerere
2. Naibu Kampeni Meneja - Godbless Lema
3. Kamanda wa Operesheni - Mwita Waitara
4. Naibu Kamanda wa Operesheni - James Ole Millya

MONITORING AND EVALUATION (M&E) TEAM
1. Freeman A. Mbowe
2. Dr. Willbrod Slaa

STRATEGISTS / CONSULTANTS:

1. Said Arfi - Mzee Arfi atatushauri kwenye masuala ya mila na destruri za Wenyeji wa Sumbawanga. Pia atatusadia kupanga mbinu za ushindi kwa kuwa ni mzoevu wa siasa za Nyanda za Juu kusini especially Mkoa wa Rukwa.

2. Prof Abdallah Safari - Huyu ni Mtaalamu wetu wa Sheria. Tumtumie ku-monitor mwenendo wa kampeni za CCM, mchakato wa kupiga kura na kutangaza matokeo. Hili swala ni muhimu kwa sababu litatusaidia kukusanya ushahidi wa kupeleka Mahakamani baada ya Matokeo ya Uchaguzi kutangazwa kama ikibidi kufanya hivyo.

3. Dr Kitila Mkumbo - Mtaalamu wetu wa Saikolojia. Tumtumie kupanga mbinu za kisiasa kuwaandaa wapiga kura kisaikojia kujitokeza kupiga kura na kulinda kura zao kama walivyofanya Wana Arumeru Mashariki. Ni mtaalamu pia wa mbinu za kikampeni kwenye chaguzi.

4. Prof Mwesiga Baregu - Mtalaamu wetu wa Sayansi ya Siasa. Ushauri wake wa kisomi utumiwe kuendesha kampeni za kisomi zisizohitaji raslimali nyingi na zenye matokeo chanya.

5. Edwin Mtei - Uzee ni dawa. Wazee wameona mengi hadi hapo walipofika. Kuna mambo tunaweza kuona ni mageni kwetu lakini kwa wazee si mageni. Tunapopata changamoto za kikampeni si vibaya kuwasiliana nae kupata mchango ushauri wake.

Nawasilisha.

TUMBIRI (PhD, HULL University - United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com

Nakala: POMPO, Mungi, Crashwise, Kimbunga, Matola, Ben Saanane, Mikael P Aweda, Mzee Mwanakijiji, Candid Scope, Yericko Nyerere, Pasco, Mwita Maranya, Molemo, Mkandara, Excy, Isango, Invisible, Josephine, zomba, Rejao, TUNTEMEKE, Losambo, BAK, nk
Naona Leo umeamka ukiwa na hamu ya kuandika majina ya watu,
 
Plan H imekaa sawa sana kamanda..ina vichwa makini sana na mchanganyiko wake ni dhahiri unaonyesha nuru ya ushindi.
 
Hivi kwanini zitto huwa hayupo sana na chadema??????????????....au na yeye anakampeni zake
 
Naona Leo umeamka ukiwa na hamu ya kuandika majina ya watu,

Epuka ku-quote comment ndefu. Unawatesa sana wenzetu wanaotumia simu hususani Crashwise. Just quote sehemu unayotaka kuichangia, zingine zifute.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakubali Plan zote,ila ujue kuna chaguzi zinakuja tena hapo mbeleni,Chadema ina timu nzuri inayokubalika kwa wananchi,nafikiri uongozi uangalie nani afanye nini kwa sababu wote ni wakali!
 

Epuka ku-quote comment ndefu. Unawatesa sana wenzetu wanaotumia simu hususani Crashwise. Just quote sehemu unayotaka kuichangia, zingine zifute.

mshauri anunue desk top Computer awe anatembea nayo kwenye box ili kuipata JF kwa uhakika, nashukuru kwa ushauri.
 
mkuu tumbiri plan c imetulia ila nadhani katika picha za hivi karibuni nimeona kama msigwa anamatatizo ya miguu(anatembea kwa magongo) so sidhani kama hataweza kukabiliana na purpushani za uchaguzi kwahiyo napendekeza vicent nyerere achukue nafasi yake....alafu sasa hayo makundi mengine yatawanywe kwenye kila kata kama ilivyokua arumeru
 
Mkuu nakubali Plan zote,ila ujue kuna chaguzi zinakuja tena hapo mbeleni,Chadema ina timu nzuri inayokubalika kwa wananchi,nafikiri uongozi uangalie nani afanye nini kwa sababu wote ni
wakali!

Ni wakati sasa CDM kuanza kufikiri katika ujengaji uwezo kwa Wanachama na uongozi husika katika jimbo kusimamia kampeni zake na kupata ushindi. Huu mfumo wa kutumia watu wale wale hasa Wabunge ni mzuri kwa chaguzi ndogo lakini unaweza kukigharimu chama kwenye chaguzi kuu hasa 2015.

Nasema hivyo kwa sababu mfumo unajenga utegemezi na itapofika 2015 ambapo kila mgombea anapaswa kujisimamia katika jimbo lake kutakuwa na shida kubwa. Hapa ndipo gamba huwa linajisimika na kukwapua majimbo kwa maana ya kutumia fedha, wanachama wake pamoja na dola.

Apoly, si Mwanachama wa chama chochote cha Siasa,ila ni mfuasi wa mabadiliko (Nachukia Rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na uonevu).
 
Zito yupo katika plan ipi?Tusiache mbachao kwa msila upitao kakitoa mbali chama jamani aisee!! Vijana wengi wamona wanaziweza siasa kwa kumtumi zito kama role mode wao leo mnamshau hata kwenye plan yeyote?Sisi wengine tupo kwenye plan za EXTERNAL OBSERVERS TU.
 
Mkuu,
Plan zote safi,
kinachohitajika zaidi ni uhakika wa uwepo au upatikanaji wa kamanda wakati huo wa kampeni kitegemeana na majukumu mengine ya chama.

halafu Mkuu mbona Zito hayuko kwenye plan yoyote?
Hata kama ana issues..., vizuri jina lake liwepo vinginevyo atakuwa na sababu ya kupanga kampeni au safari zake!
 
katika hiyo timu nashauri, mchanganyiko wa umri, jinsia na asili vizingatiwe ili kugusa makundi yote katika jamii. na viongozi wakuu washiriki zaidi katika uratibu wa ndani wa zoezi lenyewe. lakini jembe mawazo nashauri awe sehemu ya kampeni. milya aendelee kuimarisha chama mikoani/
 
Vicent Nyerere jina linausika sana, vile vile ana cv nzuri uchaguzi uliopita (arumeru),
John Heche mkutano wa juzi alipata mapokezi makubwa uko sumbawanga, anakubalika
Sugu moto chini kama kawa
James Millya kuonesha udhaifu wa ccm

Angalizo.
Joto la kisiasa sasa hivi lipo juu sana viongozi wakuu wapumzike Dr slaa/Mbowe, wahusike ktk uzinduzi na kufunga kampeni
 
Ni wakati sasa CDM kuanza kufikiri katika ujengaji uwezo kwa Wanachama na uongozi husika katika jimbo kusimamia kampeni zake na kupata ushindi. Huu mfumo wa kutumia watu wale wale hasa Wabunge ni mzuri kwa chaguzi ndogo lakini unaweza kukigharimu chama kwenye chaguzi kuu hasa 2015.

Nasema hivyo kwa sababu mfumo unajenga utegemezi na itapofika 2015 ambapo kila mgombea anapaswa kujisimamia katika jimbo lake kutakuwa na shida kubwa. Hapa ndipo gamba huwa linajisimika na kukwapua majimbo kwa maana ya kutumia fedha, wanachama wake pamoja na dola.

Mkuu Apolycaripto,
Jiulize wakati wa uchaguzi mkuu 2010 Majimbo ya Nyamagana, Ilemela, Ubungo, Kawe, Musoma Mjini, Mbeya Mjini, Iringa, Karatu, Arusha na majimbo mengine tulishindaje? Kwamba tulitumia mfumo huu huu? Mi nadhani unapaswa utambue kwamba Chaguzi ndogo mara nyingi zinakuwa na sura ya uchaguzi wa Kitaifa ndiyo maana hata magamba nao huwa wanawaita vipanga wao kina Lusinde kuokoa jahazi.

Unapochukua timu makini na kuipelekea kwenye Chaguzi ndogo ndipo unapata fursa ya kuwafundisha kwa vitendo wanachama na uongozi husika wa Jimbo, Wilaya na Mkoa jinsi ya kuratibu chaguzi. Ndivyo hivi tumekuwa tukifanya na tutaendelea kufanya hivi Mkuu wangu. Siyo kwamba timu inavyokwenda 'site' wanachama wa eneo husika wanalala. La hasha! Wao ndio watendaji wakuu wa mchakato mzima lakini wanakuwa wanasimamiwa na timu iliyoteuliwa na Chama Makao Makuu.


TUMBIRI (PhD In Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), B.com(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Plan C imekaa vizuri japo ingefaa sana kama plan zote zingepata majukumu huko nadhani chama kitajipanga zaidi
 
Back
Top Bottom