Pemba yavamiwa, Wapemba wasema amani itavunjika na wapo tayari!

Hivi ghafla Nduguyo wa damu anakuletea ulinzi nyumbani kwako maaskari kama 20 hivi, pana usalama kweli hapo?

Tatizo ni kutoamini kila kinachofanywa na bara. Unaposema unaletewa ulinzi nyumbani kwako unamaanisha askari hawana mandate ya kufanya kazi Pemba? Suala la usalama si la muungano au na hili liliingizwa kinyemela kwenye mambo yahusuyo Muungano? IGP akisikia kuna hali isiyoridhisha Pemba asiongeze askari na kuwasikiliza akina Rashid Mohamed kuwa kuna usalama kwa hiyo aache? Acheni ubaguzi!!
 
Tatizo la Wapemba wamekaa kisharishari. Mbona wao wakiishi Tanzania bara au Tanganyika kama wanavyoitwa wao hawaitwi wavamizi! Mnatafuta sababu tu za kuanza fujo! Sasa hawa ambao wako kazini kisheria wanaitwa wavamizi, acheni ubaguzi bwana!

Mi sio mpemba, lakini hapa nadhani unawaonea.

Sioni kama ni dhambi wao kuto ichagua CCM, na hao askari wanao pelekwa nina hakika unajua ndani ya moyo wako wanacho enda kukifanya, si kuwalinda wapemba, hilo unalijua. Wakati mwingine ni vyema ukaukubali ukweli kwani siku zote ukweli huwa unabaki huo huo, asante ndugu.
 
Amin. Lakini msifanye mlichofanya huko nyuma. Hatimaye wanaoathirika ni ndugu zetu. Na msiba wako Junius ni msiba wa kwangu.
Tuombe Mungu iwe salama. Lakini hali inakatisha tamaa mpaka sasa. Naona hivi vichwa vya ndugu zetu wa Tanganyika wanaopelekwa Zanzibar kwa kisingizio cha kuimarisha usalama(ukweli ni kulinda maanguko ya CCM) kama vinapelekwa machinjioni vile, watu hawajasahau askari hawa walivyofanya unjama wao, mara hii tuna wakaribisha sana tu 'jino kwa jino'. Dunia itashangaa kabla ya mapambuzuko ya asubuhi kutakuwa kumekucha usiku na asubuhi giza.

Tatizo la Wapemba wamekaa kisharishari. Mbona wao wakiishi Tanzania bara au Tanganyika kama wanavyoitwa wao hawaitwi wavamizi! Mnatafuta sababu tu za kuanza fujo! Sasa hawa ambao wako kazini kisheria wanaitwa wavamizi, acheni ubaguzi bwana!
Hujaonja na nakuombea Mungu usije ukaonja machungu ya kumwagwa damu ya ndugu yako wa damu kabisa, haina mfano machungu yake. imagine ndugu yako anakuaga anakwenda kuchota maji kisimani, punde unaambiwa ameuwawa kwa risasi, waliomuuwa ni walinzi wa manani na utulivu, hii inakaa vizuri katka akili yako?(dont reason fanatically)
 
Habari ni kuwa wananchi waPemba wamezidi hamasa na wameshawishika zaidi kutembea vifua mbele baada ya kuonekana ni tishio ,na hupita chini ya mapolisi huku wakirusha maneno ya ajabu ajabu ,ambayo kwa hali yeyote ile hayapendezi kwa waliotumwa kukaa gadi.
 
duh! ikiwa watu wanapelekewa ulinzi siku za kujiandikisha na siku za uchaguzi tu,tena wanavuka bahari.. sijui wale mapolisi wa znz hawatoshi au vipi.. Na sijui ni hakki hiyo? na sijui kama hapo pana democracy? basi ccm watangaze tu kuwa tunarudisha mfumo wa chama kimoja,bora kuliko kuwanyanyasa watu kama hivi kwa hakki yao.. Juzi kuna muandishi mmoja alitaka kumhoji sheha na baadhi yaa waandikishaji ktk kituo kimoja alivomkaribia sheha akaambiwa haturuhusiwi kuongea na mtu yeyote hapa,mwandishi akauliza kwa nini,akaambiwa angalia pale pembeni,tumepewa maagizo na wale usalama wa taifa tusiongee kitu,na wale usalama wanatoka bara.. sasa sijui kule hakuna serikali au ndo ile ahadi aliyoitoa Kikwete wakati alivokwenda znz akafanya mkutano kibanda maiti akasema,TUTAYALINDA MAPINDUZI YETU KWA GHARAMA YOYOTE NA ATAKAECHEZEA MAPINDUZI ATAKIONA...
wanaokejeli wana dhimma kubwa sana siku ya mwisho.. mimi nashanga nikiona wananchi wa znz wanasikitika wakiona ndugu zao wa bara wanaponyanyasika,lkn wa bara wana wa kejeli.. inauma sana. siku utakayokataliwa wewe kupiga kura hapo ndo utajua uchngu wake,au atakapouliwa mtu wako wa karibu tena hana kosa lolote,Mungu akuepushie mbali na hayo..
 
Habari ni kuwa wananchi waPemba wamezidi hamasa na wameshawishika zaidi kutembea vifua mbele baada ya kuonekana ni tishio ,na hupita chini ya mapolisi huku wakirusha maneno ya ajabu ajabu ,ambayo kwa hali yeyote ile hayapendezi kwa waliotumwa kukaa gadi.
Mh!!! Nyimbo ya uchochezi hiyo. Tunakwenda kwa sheria na tunafuata sheria.
 
Back
Top Bottom