Hili jambo limenishangaza kweli, Yaani Kagame hata kabla ya kukutana na Tshisekedi tayari anaongea kwa kujiamini tena kwa mkwara mzito, kwamba wasipohafikiana yeye yupo tayari kupigana.
Kagame hii jeuri ya kuzozona na kila nchi Africa Mashariki anaitoa wapi?
Kagame anajiona nani haswa hapa EA?
Lakini pia nimegundua JK alikuwa sahihi alipotaka kumuwajibisha, huyu mtu ameota mapembe hapa EA.
_________________________
Kagame: Nimejiandaa kwa mabaya zaidi katika mzozo wa DR Congo
Rais wa Rwanda Paul Kagame anasema anatarajia mema lakini "amejitayarisha kwa mabaya zaidi" kuhusu mzozo kati ya nchi yake na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
DR Congo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa Congo wa M23 na hivi majuzi ilisitisha mikataba yote ya biashara na ushirikiano. Rwanda inakanusha madai hayo.
Rais Kagame anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake wa Congo, Rais Félix Tshisekedi siku ya Jumatano katika mji mkuu wa Angola, Luanda.
Mazungumzo hayo yanasimamiwa na Rais wa Angola João Lourenço.
Lakini kabla ya mkutano huo, Rais Kagame ametuma ujumbe katika mtandao wa twirtter akisema anajiandaa kwa mabaya zaidi.
"Natarajia mema kwa sisi sote, Congo na Rwanda. Lakini kama yaliyo bora hayatakuja, watakuta nimejiandaa kwa mabaya. Hiyo ndiyo njia ya kwanza ninayoishughulikia. Ninajiandaa kwa mabaya lakini ninawatakia mema zaidi na ninamaanisha."
Rais wa Rwanda anasema hakuna "suluhisho la kichawi" katika mvutano kati ya majirani hao wawili.
"Hakuna suluhisho la uchawi hapa kwangu zaidi ya kuwasilisha ukweli kama ninavyouelewa na ukweli umeshawasilishwa... sio watu kuunda ukweli wao wenyewe au kufikiria tu kwamba watatoa suluhisho kwa upande mmoja au mwingine."
Chanzo REUTERS, Aljazeera, BBC
View attachment 2281873
Annunaki upo vema sana. Sema tu Kule kwenye ligi yetu ya Ukraine unanisikitisha upande uliochagua.