KWELI Paul Kagame alihudumu kwenye Jeshi la Uganda na kufikia cheo cha Mkuu wa Usalama wa Jeshi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda.

Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani.

Kagame.png

Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
 
Tunachokijua
Paul Kagame, Rais wa sasa wa Rwanda alizaliwa Gitarama, katikati mwa Rwanda, Oktoba 23, 1957, katika familia ya Watutsi. Mwaka 1959, mauaji ya Watutsi yaliyofanywa na Wahutu yalipoanza, familia ya Paul Kagame ilikimbilia Uganda pamoja na maelfu ya Watutsi ili kuokoa maisha yao.

Mwaka 1979, akiwa na umri wa miaka ishirini na miwili, Kagame alijiunga na kundi la National Resistance Army (NRA), lililokuwa linaongozwa na Yoweri Museveni, wanamgambo waliokuwa wanaoungwa mkono na Marekani kupigana na dikteta wa Uganda wa miaka ile, Idi Amin Dada.

Mwaka 1986, NRA ilimpindua Obote na Museveni akawa Rais na kumteua Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Ulinzi ya Uganda.

"Kwa miongo kadhaa, Kagame na Museveni walipigana bega kwa bega, na kumwangusha dikteta wa Uganda, Milton Obote kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1986 na kumwangusha Mobutu Seko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1997. Kagame, ambaye alipata mafunzo ya ujasusi nchini Tanzania, akawa mkuu wa ujasusi wa Museveni na msiri wa karibu. Kwa upande wake, Museveni alisaidia kuinuka kwa Kagame madarakani, na kuwaingiza wakimbizi wa Rwanda ambao hatimaye waliunda Rwanda Patriotic Front. Kwa kuungwa mkono na Museveni, Kagame aliivamia Rwanda, na kumaliza mauaji ya kimbari ya 1994", wanaandika Council on Foreign Relation.

Mnamo 1990, baada ya kuhudhuria kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Merika huko Fort Leavenworth, Kansas, Kagame alianza kutawala katika nchi yake ya asili ya Rwanda na Oktoba 1, 1990, Front Patriotique Rwandais (FPR), iliyojumuisha Watutsi wengi walio uhamishoni, na kuundwa katika miaka ya 1980, walianza kushambulia miji ya mpakani mwa Rwanda. Oktoba 2, kiongozi wa FPR Fred Rwigema alikufa vitani na Rais Museveni akamteua Kagame kama kiongozi mpya wa FPR.

Kati ya 1991 na 1993, Kagame aliongoza FRP katika mazungumzo huko Arusha, Tanzania ili kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Rwanda. Mwaka 1994, hata hivyo, baada ya kifo cha Rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana katika ajali ya ndege, mauaji ya halaiki yalianza ambapo takriban watu milioni moja waliuawa wakati wa mauaji hayo.
Alikuta watu wako kazini tayari,
Fred Rwigema ndiye alikua front,Salim Saleh,Sam kaka,na wengineo hao ndio waliingia mazima na makamanda kama Samson Mande ndio aliikamata Kampala.
Ye hakuwepo,alikutana nao washamaliza kumkimbiza Amin wanaelekea njiani Chigali.
Fred ndo alikua na kikosi kizima,akalimwa shaba ya kisogo na wenzie hao hao,wakasonga mbele.
Pk ndio akashika Mpini.
Hao wote wamekulia hapo bongo Upanga,na waliondokea hapo kulianzisha huko.
Kwenye vita ukiwa jasusi weye kazi yako ni kutafuta taarifa kupitia njia mbalimbali, mawasiliano ni mojawapo. Wawekwa sehemu yaitwa " listening post".

Pale "intelligence analyst" ndo hupata kila kitu na makamanda hupewa mkeka mzima.

Ila kiukweli, hili kundi la akina Rwigyema, Nyamwasa, Ssemwogerere na wengine walikuwa ni kundi "special".

Kuna ule msemo usemao mafahari wawili hawakai zizi moja.

Sasa kundi hili lilikuwa na mafahari zaidi ya 10, ni lazima aibuke fahari mmoja au wawili na ndicho kilotokea leo twafahamu ni mafahari gani tulo nao.
 
Wote washamwagwa hao,ndugu yao anakula keki ya taifa mdogo mdogo.
Nyamwasa yuko rest house kwasasa Belgium au Swissland.
Kuna Rose na wengine walikua front wameishia wapi?
Kuna mambo mengi ile nchi ni kuwaombea tu.
Ni kamkoa ketu.
 
Paul Kagame alikulia katika kambi ya wakimbizi ya Nshurungerezi iliyoko Uganda.

Lakini baadae akiwa na rafiki yake Fred Rwigyema walijiunga na FRONASA ambalo lilikuwa ni kundi la waasi la Uganda lilokuwa na makazi yake Tanzania na liloongozwa na mzee Yoweri Kaguta Museveni.

FRONASA walipewa hadhi ya ukimbizi nchini Tanzania na serikali ya Tanzania na Yoweri Museven amesoma chuo kikuu cha Dar-es-salaam.

Kulipoibuka vita ya Tanzania na Iddi Amin mwaka 1979, mzee Kagame na rafiki yake Fred Rwigyema waliungana na wapiganaji wa FRONASA chini ya Museveni kumuondoa Iddi Amin.

Hapo ndipo Paul Kagame alifanya kazi za uchambuzi wa kijasusi (intelligence analyst) kwa serikali na majeshi ya Tanzania na aliongoza kazi maalum ziloratibiwa na kusimamiwa na marehemu brigedia (baadae luteni jenerali) Imran Kombe.

Mzee Paul Kagame amesoma na kupata mafunzo ya kijeshi kutoka katika chuo cha kijeshi cha CGSC cha nchini Marekani.

Umenikumbusha mbali sana. Luteni General Imran Kombe! Kumbe PK alikuwa ni mmoja wa wanaomfanyia kazi? Naamini Tanzania ilimpika kama wengine wengi. Ila anachofanya sasa kitamrudi. Awe na maarifa
 
For decades, Kagame and Museveni fought side by side, toppling Ugandan dictator Milton Obote via military coup in 1986 and overthrowing Mobutu Seko in the Democratic Republic of Congo in 1997. Kagame, who trained in Tanzania as a spy, became Museveni’s head of military intelligence and close confidant. In return, Museveni aided Kagame’s rise to power, incubating Rwandan refugees that eventually formed the Rwanda Patriotic Front. With the backing of Museveni, Kagame invaded Rwanda, ending the 1994 genocide.

Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda.

Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani.

Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
Dunia
2645411.jpg
 
Kwa taarifa hizi Tanzania hatukupaswa kuongozwa na mama kizimkazi. Tutafute rais maana tunazungukwa na majenerali hatari
 
Umri mkubwa /Longevity is the blessing from God/baraka toka kwa Mungu. It's written "I will fulfill the numbers of your days" Exodus 23:26
Nakubali Mzee wangu, aisee ukichngia kwenye mada zinazohusu michango ya urusi/Ukrein/Israel/Palestine, picha yangu ilikua inakuja kuwa wewe utakua nikijana tu wa malika yangu, Kwa namna ulivyo eleza hapo juu yaani umri wako ukiurudisha miaka 20 nyuma, bado unabaki kua kama kaka yangu. Ndio maana nasema Shikamoo mzee wangu.
 
Mwaka 1979 Kagame alikuwa na umri gani?
Mara baada ya vita ya Kagera kumalizika mwaka 1979 Uganda na Rais wake General Idd Amin Dada kutimuliwa na majeshi ya Tanzania uongozi wa nchi ulishikiliwa kwa na late Major General Msuya wakati huo akiwa na cheo cha Col.

Mwaka 1979 April Uganda ilianza kuongozwa na Bwana Yusuf Lule kuanzia April 1979 hadi June 1979.
Mwaka 1979 June hadi mwaka April 19780 Bwana Godfrey Binaisa aliongoza Uganda.
Mwaka 1980 Uongozi ulishikiliwa na Paul Muwanga
Mwaka 1980 hadi 1985 Milton Obote aliongoza Uganda kwa mara ya pili kwa kipindi cha miaka 5.
Kipindi cha miaka 5 ya uongozi wa Bwana Milton Obote ndipo kosa kubwa lilitokea wakati zilikuwepo juhudi za kuunganisha makundi mengi madogo madogo.

Kipindi hicho Bwana Kaguta Museveni alikuwa Waziri wa Ulinzi chini ya uongozi wa Obote.Tanzania ikatoa offer ya kuliunda jeshi la Uganda.Maafisa wa jeshi wakapata nafasi ya kujiunga na chuo cha kijeshi Monduli {Officer Cadet} kwakuwa Museveni alikuwa Waziri wa Ulinzi alitumia nafasi hiyo kuhakikisha watu wake wengi wanakwenda Monduli.

Mwaka 1985 Mkuu wa Jeshi General Tito Okello alimpindua Milton Obote na kuongoza Uganda hadi Mwaka 1986 alipopinduliwa na Kaguta Museveni ambaye tayari alikuwa na vijana wake wengi waliopata mafunzo ya kijeshi nchi Tanzania Monduli.
Ukitaka kujua ni muda gani Kagame alipata mafunzo Tanzania ni kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 1985 kwasababu ndipo nafasi nyingi sana za mafunzo ya kijeshi zilitolewa.

Obote alizubaa sana alitakiwa kuhakikisha msaada ya mafunzo ya kijeshi unagusa makundi yote hasa makabila yote.General Tito Okello alijikuta akizidiwa ujanja na Museveni kwasababu maofisa vijana wenye mafunzo ya hali ya juu walikuwa watiifu kwa Museveni akiwemo Kagame na wenzake wengi waliokuwa na asili ya Rwanda.
 
Nkunda Mungu wa Mbinguni akutunze, akupe maono nauendelee kutupa siri kwaajili ya amani ya nchi yetu Tanzania.
 
Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda.

Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani.

Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
Sio kweli ni uongooo kagame ajawai kuwa Mwanajeshi wa Uganda
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom