Pasaka imenipotezea rafiki yangu kipenzi

Daa
Kichwa cha habari kina utata kidogo “Pasaka imenipotezea Rafiki yangu......”inaleta maana tofauti,anyway RIP Fred !km itakupendeza mtoa post naomba utukumbishe post zake alizozitoa ndg yetu huyu (maana majina yetu JF ni ya bandia )ila na sisi tushiriki msiba huu kwa Feeling.
! Daa! Mkuu hata Mimi siijui ila alikuwa akitumia nikname Kama wengi humu, Mimi Ni rafiki yake wa Karibu Sana,Mara kadhaaa Aliniambia yeye pia ni member wa JF
 
Ni wiki moja tu imepita, Tulichati kwa whatsap.Tulikuwa tukicheka madakika yakapita.Sikujua Kama Ulikuwa waniaga, Umeondoka mkuu.Pumzika kwa Aman Kaka Fred,Mungu akupokee. Mpaka Sasa sielewi na pia siamini Kama kweli umetutoka, nawaza na kujifariji labda kesho utaamka.Taarifa za kifo chako, zinatatiza ni ngumu kuelewa.Pumzika kwa Aman Kaka Fred, Mungu akupokee. Taarifa zinaeleza ulikuwa watoka kijijini Kilolo, mara Izraeli akakupata,ghafla bila kujua Pumzika kwa Aman Kaka,hiyo ni njia yetu sote. Utakumbukwa Sana mitamdaoni,fb mpaka jf.Fb ulijulikana na ukurasa wako wa vichekesho,Tabasamu na Fuledi,wengi walikuelewa,na walipenda vichekesho vyako.Pumzika kwa Aman Kaka,Mungu akupokee.Ajali ya gari imekatisha uhai wako, Tena siku ya Pasaka,kweli kifo ni fumbo,nakosa hata wa kunisimulia ilikuwaje,kila mtu anasema juu juu tu,Pumzika kwa Aman broo Mungu akupokee.😭
aaaaaaaaa dah so sad! Aiseee hata siamini jamaa alkuwa rafiki yangu fb nilikua nafuatilia sana vichekesho vyake kweli dunia mapito ajali imetokea wap kwan? Dah R I P Fuledi mwagito
 
Back
Top Bottom