Parking Hospital za Umma na Binafsi

ze_nigga

Member
Oct 5, 2016
10
15
Binafsi nilitembelea hospitali ya Muhimbili jana, nikiwa nimeenda pale Institute ya Jakaya Kikwete, nikakuta hamna parking kabisa nikaelekezwa kupaki upande wa clinic ya watoto. Na kufika upande huo nikakuta parking zilizopembeni ya jengo zote ni za staff, sisi wengine tunapaki nyuma huko karibu na msikiti.

Sasa nikajiuliza ivi ni nani anatakiwa apewe kipaumbile cha parking? Kati ya mgonjwa ama staff? Mgonjwa anaweza kuja pale hoi anafika anapaki mbali mnoo yaani kitendo cha kutembea tena mwendo mrefu, itakuaje kama akianguka pale na kupoteza maisha! Lawama atabeba nani?

Swala la parking liangaliwe upya hasa kwenye hospital za umma. Staff magari yao yapo siku nzima kwann wao wasipangiwe huko nyuma maana hayana movement baada ya kufika!
 
Ukifa unadhani kuna mtu atashtuka? Unadhani kwa siku pale wanafariki watu wangapi? Usilete kisingizio mgonjwa atashushiwa wapi kwani Kama una mgonjwa pana eneo maaalum mlangoni kabisa la kushushia watu/wagonjwa na hua halizibwi, kisha wewe dreva utaondoa gari lako ukatafute parking utakakoipata.
 
Unapeleka mgonjwa kwanza mnamshusha panapohusika halafu unaenda kutafuta parking. Au labda kama mgonjwa ndo dereva na yuko mahututi hapo ndo shida.
 
Sio wagonjwa wote wanawatu wakuwapeleka mkuu. Wengi wao wanajiendesha wenyewe. Sasa ulitaka mtu anajiona hali sio anawahi hospital alafu anapaki mbali sana akianguka itakuwaje?
 
Mgonjwa anaweza kuja pale hoi anafika anapaki mbali mnoo yaani kitendo cha kutembea tena mwendo mrefu, itakuaje kama akianguka pale na kupoteza maisha! Lawama atabeba nani?
Akija yuko hoi kuna sehemu ya kushushia wagonjwa assuming kwamba anaendeshwa na huyo aliyemleta ndiye akahangaike kutafuta parking
 
Back
Top Bottom