Panya Road wavamia maeneo ya Magomeni, Mwananyamala na Kinondoni jijini Dar

Wanatisha usiombe kukutana nao hawa panya wa barabarani. Mimi nimewaona meno yao kama ngiri, nimejaribu kupiga picha camera haiwanasi, Muda huu wanakatiza hapa nanjilinji ni zahiri wanaelekea msumbiji.
 
Manzese hadi urafiki ni mbiombio tu na machinga na abiria hakuna utulivu hata kidogo..kila mmoja hajui anakimbia nini na kuelekea wapi..viatu mkononi.!

Tuna asili ya hawa jamaa.

Blue-wildebeest-ssp-taurinus-adult-and-infant-running.jpg
 
Ni kwamba wanamtafuta mwenzao katekwa na Kundi la Washawasha la Mwananyamala kisiwani. so wanawatafuta kabla hawajamfikisha mwenzao kituo cha polisi cha Mabatini. Polisi wameshafika makumbusho stand kwani walikua washaanza kuiba vitu

Kutoka PANYA ROAD,MBWA MWITU, WAAMERIKA WEUSI,mpaka KUNDI LA WASHAWASHA LA MWanayamala...! inSecurity in Dar is at verge of point of no return...!
 
Mi nilikua maeneo ya mexico bar kinondoni gafla nikaona kundi la watu wanakimbia kuuliza wakasema panya road wapo masai club wanapora, kuna jamaa zangu watatu nilikua nao wote wana vyamoto walikua wameshakaa tayari kuwafyeka hao panya road bahati ya hawakuja maeneo tulipo.

Hizi flash bhana, utakuta upo zako gheto unakula ugali dagaa kama mimi hapa.
 
Mi nipo knyama watu walikuw wnafunga maduka kw romours zilizokuwa zimeenea mitaani. Diffender mbili zimepita zikitokea mabatini kituo cha polisi na kupiga risasi moja hewani kabla hawajakunja kufuata akachube road ilielekeayo mwananyamala. Nothing has been known kuanzia nusu saa iliyopita.
 
MIMI niko sinza tume jifungia ndani, kwakweli hali ni mbaya mno. Nchi hii tunaenda wapi jamani. The country is not peace kwakweli
 
Wananchi inabidi mjilinde kwa namna yoyote ile na si kutegemea serikali tu.

Kama vipi nunueni hata bunduki kwa njia zisizo halali.
 
Maeneo ya Mwananyamala watu wamekimbilia hosp kujificha. I hope polisi watawadhibiti kabla hawajahamishia fujo ndani ya hosp.
 
Hawa watoto serikali inawachekea,leo wameleta taharuki mitaa ya uzuri,sinza hadi ubungo,ni mda muafaka wapigwe risasi tu.
 
PANYA ROAD:~ kama kweli mmechoshwa na ufisadi wa nchi hii tafadhalini nendeni kwa waliowaibia MASAKI,MIKOCHENI,IKULU,NYAMBA ZA MAWAZIRI MIKOCHENI,BUNGENI DODOMA NA KWINGINEKO AMBAKO MNAJUWA VIONGOZI WENU WANAPOISHI SISI MASIKINI WA MANZESE TANDALE MWANANYAMALA HATA BUGURUNI TAFADHALINI HATUJAWAIBIA NYIE WAZALENDO HATA SENT TANO CHONDE CHONDE
 
Yes, sinza wamepita. Tena wamepita nje ya nyumba yangu kabisa. Nimefunga milango na mageti yote nipo ndani tu na umeme umekatika. Ila kwa sasa pako shwari sijui wameeleka pande zipi. Ila ni hatari mtaa wote kimya kimya kabisa. Hata wenye za moto wanahofia endapo utaua mmoja wao wanarudi kwa kisasi.
 
Tuna asili ya hawa jamaa.

Blue-wildebeest-ssp-taurinus-adult-and-infant-running.jpg

Hahahaaaa

Hili linchi watu wake mafisi kabisa.

Yaani kweli hao panya road wanafunga kabisa mitaa na kufanya watu waache kula bata batani kwenye mabaa na kutimua mbio?

Hahahahahaaaa daaaah!

Kwani wana silaha gani hao wahuni hadi wafanye watu kuogopa kiasi hicho?

Only in Tanzania!!!!!!!!!!!
 
Haya ndo Madhara ya Social GAP kuwa Kubwa!!! Nyerere aliliona sana hili, Lakini hawa watawala wa sasa wamezidisha Ubinafsi kiasi cha kusababisha kipato kati ya Walionacho MAFISADI na Walalahoi kuwa kubwa umbali wa mbingu na Ardhi!!! Regemalira anagawa fedha za Umma kwa matajiri wenzie huku akina katelephone wakikosa Elimu, maji, Umeme, hata mlo mmoja unawashinda!!! ... The Only solution ni kutengeneza ajira na maisha bora kwa Watanzania wenye Utajiri mwingi waliopewa na Allah S.W.T... Haiingii akilini eti Almasi ya Mwadui, Dhahabu ya Geita, Chuma ya Liganga, Uranium ya Bahi, Tanzanite ya Mererani ziwanufaishe WAGENI na MAFISADI Wachache ...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom