Pamoja na Yote, Hongereni Simba SC

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,997
3,937
Pamoja na KUTOLEWA, Simba imecheza Classic Game. CONGRATULATIONS.

MAPENDEKEZO
1. Gomes ni Kocha Mzuri, Simba iendelee nae.
2. Nadhani Simba itafute Forward mwenye UWEZO na MBINU.
Mugalu HAPANA, ni BIG NO ! Mugalu hana TALENT ya mpira kama Morrison au Luis.Nunueni forward mwenye uwezo wa kufunga goli kwenye IMPOSSIBLE ANGLES. That is what Simba lacks.

3. Usajili wa Beki UZINGATIE na VIMO. Kuwe na AverageHEIGHT angalau 178 cm tall .
Djuma Shabani.

4. Nadhani pia Wawa ameshaanza KUCHOKA, mtaangalia namna ya kufanya nyie wenyewe.
5. Manula na CHAMA wanahitaji msaidizi, pengine bora zaid yao. Chama ni bishoo kama yule Bwalya wa Ahly, hawapaswi kucheza dakika 90 , kuna moment wanazi cost timu sana. REPLACEMENT AT SOME POINT ni lazima.

6. Kikosi KISIBOMOLEWE, wachezaji kama Morrison, Luis, Bwalya , Chama, Gomes na wale wengine ambao ni CREAMS WASIUZWE. Makosa haya yalifanywa na As Vita na MAZEMBE,? Building CHEMISTRY iliyopo sasa sio kazi ya OVERNIGHT. kikosi kiboreshwe maeneo MUHIMU tu

7. RIPOTI ya kocha juu ya mapendekezo yake kuhusu REFORMS ya timu IHESHIMIWE. Simba mnatabia ya KUCHAMBIA recommandations za makocha.
———————————
Utopolo wenzangu tupunguze majungu , mpira wa sasa sio blah blah ni INVESTMENT na STRUCTURE, sio kulalamika lalamika kama mke aliye TALIKIWA. Simba mpaka sasa kaingiza Bilioni zaidi ya 3 , sisi UTOPOLO tumeingiza ngapi,?

Uwezekano wa SIMBA SC kucheza tena Robo fainali mwakani ni zaidi ya asilimia 60%, sisi UTOPOLO ni ngapi....? Ifike mahali YANGA tu FOCUS kwenye mambo ya MSINGI, MPIRA NI BUSINESS, otherwise tutaendelea kuwaangalia SIMBA wakila CAKE ya CAF kila mwaka.

Mwisho, Nawapongeza sana SIMBA SC, wachezaji na benchi la ufundi for the good fight na kuendelea kutujengea HESHIMA ya SOKA letu EAST AFRICA. tumeona leo Cavin Hunt alivyokuwa anasali sala zote mpira uishe, KICHEKO CHA DHARAU KILIPOTEA LEO , hii ni ishara GOMES akipewa uwezo , hakika anaipeleka SIMBA fainali, time will tell!
 
Hapo kwa Mugalu upo sahihi sana mkuu

Mimi nashangaa wanasema eti ana hold mipira, wakati mwingine timu inahitaji magoli. Halafu mbona AFRICA zipo forward za kibabe tu ; huyu MUGALU kawapa nini simba. Wanamtetea kweli ; foward gani mechi kama hii Hata goli moja; kazi kutafuna MIRUNGI TU
 
Aisee hapo Kwa Hunt bana nimecheka Sana...nilimsubiri Kwa hamu acheke tena badala yake akawa karibu na kulia😁😁

20210522_120010.jpg
 
Hongereni viongozi, wachezaji na benchi la ufundi la Simba. Kwa kweli leo timu nzima ilijitoa bila kuchoka kwa dakika zote 90. Nina uhakika kabisa Mo na bodi yake wameona sehemu chache za kuongeza wachezaji ili mwakani timu ifanye vizuri zaidi. Nionavyo mimi Simba wanahitaji kusajili wachezaji wasiozidi watano tu ili wasipoteze huu muunganiko ambao tayari upo.
 
Hongereni viongozi, wachezaji na benchi la ufundi la Simba. Kwa kweli leo timu nzima ilijitoa bila kuchoka kwa dakika zote 90. Nina uhakika kabisa Mo na bodi yake wameona sehemu chache za kuongeza wachezaji ili mwakani timu ifanye vizuri zaidi. Nionavyo mimi Simba wanahitaji kusajili wachezaji wasiozidi watano tu ili wasipoteze huu muunganiko ambao tayari upo.

Yes, IMESHAURIWA hapo juu kuwa, Kikosi kisibomolewe; wafanye maboresho maeneo muhimu.
 
Back
Top Bottom