Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 16,488
- 41,635
Wote ni mashahidi kuwa Sensa ya mwaka huu ilikuwa na promo sana ukilinganisha na zilizopita, na dhumuni kubwa ni kuongeza hamasa kwa wananchi ili waweze kushiriki.
Ila kama ilivyokuwa kwa post code(anuani ya makazi), sensa inaharibikia mwishoni, na data zitakazokusanywa hazitakuwa na uhalisia, hii inatokana na sababu zifuatazo:
1. Walioomba hizi kazi, walipata msukumo kutoka kwenye hela za malipo bila kupima uzito wa kazi.
2. Makarani wanapika sana hizi data na hawafati misingi ya sensa inavyotaka.
Imagine karani alikuwa anahoji mwanamke ambaye anaishi na watoto wake wawili, ila usiku wa tarehe 22 kuamkia 23, hawa watoto hawakuwepo hapa Dar, wapo likizo kijijini kwa bibi yao.
Ila huyu Mama alimuomba karani watoto wake wahesabiwe hapa Dar, na karani alimkubalia, huko walipo it's obvious watahesabiwa tena .
3. Karani alikuja kwangu, akaniuliza umri, majina, tunaishi wangapi, tuliolala pale 22 kuamkia 23, namba ya nida na bima ya afya. Then after hapo akawa kimya muda mrefu, namuuliza vipi mbona kimya? Akanijibu kuwa taarifa zinazofata zinaeleweka ndio maana anajaza, so nisiwe na wasi. Ila nikahisi kama amemaliza kujaza dodoso, ikabidi nimuulize, mbona taarifa za ninaeishi nae hajachukua hata moja? Maana hakuniuliza umri wake, majina elimu n.k.
Yule karani akanijibu kuwa wanawake taarifa zao zinachukuliwa kwenye kaya za jamii. Nikamuuliza why iwe hivyo wakati anaishi hapa? Akanijibu kuwa taarifa zingine wanaume hatuwezi kuwa nazo, au unakuta ni za siri hivyo inabidi zitolewe na wanawake wenyewe kwenye dodoso za kaya za jamii, akatolea mfano mwanamke anaweza kuwa na mtoto wa nje alaf wewe hajakwambia .
Ilifikia hatua nikamwambia wewe nenda tu, maana sidhani hata kama unakijua unachoongea.
Sasa nikawa najiuliza, why wapike data? Kusave time, wamechoka au nini? Maana kazi ndio kwanza siku ya 3, au ni vile wanahasira/uchungu wa hela ambazo wanahisi wamepigwa?
Maana wanasema hela za chakula walizokatwa, zilikuwa haziendani na chakula wanachopewa. Lakini pia kuna certain amount in cash walitakiwa kupewa, nazo hawajui hatma yake.
Anyway, waendelee kujitahidi kwa hizi siku zilizobaki, ila wawe makini wasije kutoa data zikaonesha tupo wachache kulinganisha na 2012, au la, kukawa na unrealistic changes.
Regards,