Pamoja na AG na Msajili wa Hazina kushauri marekebisho ya mkataba, NARCO yasaini mkataba huo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,046
144,448
Mkataba usio na masilahi kwa Taifa ulioandaliwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (Narco) kuipa kampuni ya Overland Livestock Multiplication & Embryo Transfer umiliki wa Ranchi ya Mzeri iliyoko Tanga umetiwa saini licha ya mamlaka za kisheria kuukataa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru ambaye ni msimamizi wa mashirika yaliyokuwa chini ya Shirika Hodhi la Taifa (CHC), walishauri mkataba huo ufanyiwe marekebisho ili uwe na masilahi kwa Taifa, lakini katika mazingira tata ulitiwa saini na kampuni hiyo ikapewa umiliki kwa miaka 66.

Novemba mwaka jana, Narco na Overland walianzisha kampuni ya kuendesha ranchi hiyo iitwayo Ovenco Ranches Limited. Narco imetoa ardhi yenye ukubwa wa hekta 20,000 sawa na asilimia 30 ya hisa huku Overland ikichangia mtaji wa Dola 15 milioni za Marekani (Sh3.2 bilioni), mifugo, mashine pamoja na vifaa mbalimbali vyote vikiwa sawa na asilimia 70 ya hisa.

Katika tovuti yake, kampuni hiyo inaonyesha imejipanga kuzalisha mitamba ya ng’ombe wa nyama na wa maziwa 7,000 wenye sifa za kijenetiki ili kusaidia sekta ya mifugo nchini.

“ORL inatarajia kuzalisha mitamba kwa kutumia njia za kawaida na teknolojia za juu kama vile In-vitro Production Embryo Transfer (IVP-ET),” inaeleza tovuti hiyo.

Kampuni ya Overland kutoka Australia inafanya kazi kwa kushirikiana na Kampuni ya Animal Breeding Services (ABS) ya New Zealand.

Mafuru alipoulizwa kuhusu utaratibu uliotumika kuibinafsisha ranchi hiyo alisema anaufahamu mkataba huo lakini aliukataa kwa vile ulikuwa na vipengele visivyoeleweka.

“Huo mkataba uliletwa kwetu lakini tukagundua hauna masilahi kwa Taifa tukawarudishia waurekebishe na hawajarudi mpaka leo. Ulikuwa na vipengele vingi havieleweki. Sasa kama wanaendelea na kazi, watapambana na vyombo vya dola, mimi kama Msajili wa Hazina kazi yangu ni kuhakikisha mkataba uko sawa.”

Masaju alipoulizwa kuhusu mkataba huo alisema: “Tulishauri kama sheria inavyotaka, kwa hiyo hao waliopewa ushauri walifuata au hawakufuata ndiyo waulizwe. Waulizeni kama waliufuata ushauri wangu au hawakufuata.”

Meneja Mkuu wa Miradi wa Ovenco Ranches Ltd, Dk Sharif Hamad alipotafutwa alisema hana nafasi ya kuzungumzia suala hilo, lakini Mwenyekiti Mtendaji wa Ovenco, Faisal Awadh alisema kama kuna matatizo kwenye mkataba, Msajili wa Hazina awaondoe kwenye uwekezaji huo.

“Hakuna mgogoro wowote, hakuna shida kwenye mkataba na kazi inaendelea kama kawaida. Ila kama wao wamekwambia kuna mgogoro ungewauliza mgogoro wa aina gani. Kuna mashamba ya ranchi 129, hakuna hata mwekezaji mmoja aliyejitokeza kuwekeza, ni sisi tu tumejitokeza. Hiyo migogoro wanayotaka kuianzisha sisi haitusumbui. Mwambie Msajili wa Hazina, kama anaona huo mkataba umeingiwa kimakosa, sisi tunaondoka… Watu wengi wamewekeza kwenye biashara hiyo wameshindwa wameondoka.”

Awadh alisema, mazingira ya uwekezaji kwenye mifugo kwa Tanzania ni magumu kiasi kwamba wawekezaji wengi wanaondoka lakini wao wamebaki wakivumilia.

“Mkataba umepita kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mara mbili na umerekebishwa na alitoa barua ikisema mkataba uridhiwe. Mnajua hawa wawekezaji kutoka New Zealand na Australia wanaondoka? Kuna ng’ombe 7,000 wako pale na kuna meli inaingia Septemba italeta ng’ombe.

“Kuna wawekezaji wengi tu wanaondoka. Jiulize kwa nini nchi za wenzetu kama Botswana, Zimbabwe, Kenya wanaendelea vizuri. Iulize Wizara ya Kilimo na Mifugo, mbona mpaka leo tunaagiza ng’ombe nje ya nchi? Tuna ng’ombe 26 milioni, mbona tunaagiza nyama na maziwa kutoka nje?”

Utata wa uwekezaji

Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya Narco zinadai kuwa mkataba huo ulishinikizwa na ‘mamlaka za juu’ bila kufuata sheria za ununuzi na kanuni za uwekezaji.

“Suala hili lilifanyika tangu Agosti mwaka jana wakati nchi inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Ni wakati ambao hata Baraza la Mawaziri lilikuwa linaelekea kuvunjika na kulikuwa na shinikizo la wakubwa,” kilisema chanzo chetu ndani ya Narco.

Mtoa taarifa alisema katika majadiliano ya mkataba huo, Bodi ya Narco ilitaka Kampuni ya Overland ipewe hekta 10,000 pia ipewe miaka 33 ya kumiliki ardhi hiyo kwa majaribio, lakini kulikuwa na shinikizo kutoka ‘juu’ la kumilikisha ranchi hiyo kwa miaka 99.

“Kulikuwa na mvutano mkubwa, ikabidi suala hilo lifikishwe kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alibadilisha baadhi ya vipengele kikiwamo cha kuvunja mkataba kama mwekezaji hatatimiza masharti,” alisema.

Hata hivyo, AG Masaju alisema: “Sijawahi kushinikizwa na kusaini mkataba wowote na wala kwa jambo lolote lile.”

Habari zinasema baada ya mvutano mkali, iliamuliwa Kampuni ya Overland ipewe miaka 66 ya umiliki wa ardhi hiyo.

Narco

Meneja wa Masoko Narco, Immanuel Mnzava alisema uwekezaji huo ulifanyika kwa lengo zuri japokuwa ulitokana na shinikizo kutoka ngazi za juu.

“Ranchi ya Mzeri inaendeshwa kwa ubia kwa uwekezaji wa kisasa kwa sababu hatukuwa na mtaji wa kutosha. Mambo mengine siwezi kukueleza hadi Meneja Mkuu aje ataeleza, lakini kulikuwa na shinikizo kutoka ngazi za juu,” alisema.

Narco ni miongoni mwa mashirika yaliyowekwa chini ya Tume ya Rais ya Ubinafsishaji Mashirika ya Umma (PSRC) na baadaye CHC na sasa chini ya Msajili wa Hazina.

Mwaka 2006, Baraza la Mawaziri liliagiza Narco igawanye maeneo yake sehemu mbili kwa mita 2,500 hadi 4,000 na vitalu vigawanywe kwa wafugaji wazalendo na eneo linalobaki libaki kuwa la mfano kwa wananchi wanaozunguka.

Vitalu hivyo vilitolewa kwa wawekezaji wazawa kwa njia ya ushindani. Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuna vitalu 121 vilivyogawanywa kwa wawekezaji hao, wengi wao wakiwa watu mashuhuri.

“Mchakato ulikuwa wazi kwani mwekezaji alitakiwa kuja na barua ya Serikali za Mitaa, wizara na taarifa zake za fedha. Wamepewa vitalu hivyo kwa miaka 33 kisha itaangaliwa upya,” alisema Mnzava.

Kaimu Meneja Mkuu wa Narco, Bwire Kafumu alisita kuzungumzia suala hilo kwa kina kwa maelezo kwamba vyombo vya dola vinachunguza mkataba huo.

“Mimi hapa ninakaimu tu nafasi, siyo ‘General Manager’. Suala la Mzeri na Overland liko kwa Msajili wa Hazina na mamlaka nyingine zinachunguza. Msajili wa Hazina ndiye mwenye dhamana na mashirika yote ya umma. Kuna mamlaka nyingine pia zinashughulikia. Tuwe na subira tu, siwezi kueleza maana nitakuwa naingilia,” alisema Bwire.

Hata hivyo, alisisitiza, “Siyo kila mara katika uwekezaji kunakuwa na ushindani, kama amepatikana mwekezaji na ana sifa anapewa tu.”

Bwire alikaimishwa nafasi hiyo, Desemba mwaka jana baada ya aliyekuwa Meneja Mkuu, Dk John Mbogoma na bodi yote ya wakurugenzi kusimamishwa kazi na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba kutokana na kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa katika eneo la Ruvu.

Kuhusu utata huo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alisema: “Takukuru tunafanya uchunguzi, inawezekana upo, lakini mpaka nifuatilie ili kujua kama kweli upo.”

Chanzo:Mwananchi

Majipu mengine sio tu yamekaa sehemu mbaya,bali utaalamu wa kuyatumbua unapatikana nje ya nchi sisi tumeshindwa!
 
Sawa tu, acha wasaini maana kikwete alisema ukipewa akili changanya na za kwako. Ushauri wao ni ama uchukuliwe au uachwe. Yote sawa tu.
 
By Elias Msuya, Mwananchi emasuya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkataba usio na masilahi kwa Taifa ulioandaliwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (Narco) kuipa kampuni ya Overland Livestock Multiplication & Embryo Transfer umiliki wa Ranchi ya Mzeri iliyoko Tanga umetiwa saini licha ya mamlaka za kisheria kuukataa.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru ambaye ni msimamizi wa mashirika yaliyokuwa chini ya Shirika Hodhi la Taifa (CHC), walishauri mkataba huo ufanyiwe marekebisho ili uwe na masilahi kwa Taifa, lakini katika mazingira tata ulitiwa saini na kampuni hiyo ikapewa umiliki kwa miaka 66.

Novemba mwaka jana, Narco na Overland walianzisha kampuni ya kuendesha ranchi hiyo iitwayo Ovenco Ranches Limited. Narco imetoa ardhi yenye ukubwa wa hekta 20,000 sawa na asilimia 30 ya hisa huku Overland ikichangia mtaji wa Dola 15 milioni za Marekani (Sh3.2 bilioni), mifugo, mashine pamoja na vifaa mbalimbali vyote vikiwa sawa na asilimia 70 ya hisa.

Katika tovuti yake, kampuni hiyo inaonyesha imejipanga kuzalisha mitamba ya ng’ombe wa nyama na wa maziwa 7,000 wenye sifa za kijenetiki ili kusaidia sekta ya mifugo nchini.

“ORL inatarajia kuzalisha mitamba kwa kutumia njia za kawaida na teknolojia za juu kama vile In-vitro Production Embryo Transfer (IVP-ET),” inaeleza tovuti hiyo.

Kampuni ya Overland kutoka Australia inafanya kazi kwa kushirikiana na Kampuni ya Animal Breeding Services (ABS) ya New Zealand.

Mafuru alipoulizwa kuhusu utaratibu uliotumika kuibinafsisha ranchi hiyo alisema anaufahamu mkataba huo lakini aliukataa kwa vile ulikuwa na vipengele visivyoeleweka.

“Huo mkataba uliletwa kwetu lakini tukagundua hauna masilahi kwa Taifa tukawarudishia waurekebishe na hawajarudi mpaka leo. Ulikuwa na vipengele vingi havieleweki. Sasa kama wanaendelea na kazi, watapambana na vyombo vya dola, mimi kama Msajili wa Hazina kazi yangu ni kuhakikisha mkataba uko sawa.”

Masaju alipoulizwa kuhusu mkataba huo alisema: “Tulishauri kama sheria inavyotaka, kwa hiyo hao waliopewa ushauri walifuata au hawakufuata ndiyo waulizwe. Waulizeni kama waliufuata ushauri wangu au hawakufuata.”

Meneja Mkuu wa Miradi wa Ovenco Ranches Ltd, Dk Sharif Hamad alipotafutwa alisema hana nafasi ya kuzungumzia suala hilo, lakini Mwenyekiti Mtendaji wa Ovenco, Faisal Awadh alisema kama kuna matatizo kwenye mkataba, Msajili wa Hazina awaondoe kwenye uwekezaji huo.

“Hakuna mgogoro wowote, hakuna shida kwenye mkataba na kazi inaendelea kama kawaida. Ila kama wao wamekwambia kuna mgogoro ungewauliza mgogoro wa aina gani. Kuna mashamba ya ranchi 129, hakuna hata mwekezaji mmoja aliyejitokeza kuwekeza, ni sisi tu tumejitokeza. Hiyo migogoro wanayotaka kuianzisha sisi haitusumbui. Mwambie Msajili wa Hazina, kama anaona huo mkataba umeingiwa kimakosa, sisi tunaondoka… Watu wengi wamewekeza kwenye biashara hiyo wameshindwa wameondoka.”

Awadh alisema, mazingira ya uwekezaji kwenye mifugo kwa Tanzania ni magumu kiasi kwamba wawekezaji wengi wanaondoka lakini wao wamebaki wakivumilia.

“Mkataba umepita kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mara mbili na umerekebishwa na alitoa barua ikisema mkataba uridhiwe. Mnajua hawa wawekezaji kutoka New Zealand na Australia wanaondoka? Kuna ng’ombe 7,000 wako pale na kuna meli inaingia Septemba italeta ng’ombe.

“Kuna wawekezaji wengi tu wanaondoka. Jiulize kwa nini nchi za wenzetu kama Botswana, Zimbabwe, Kenya wanaendelea vizuri. Iulize Wizara ya Kilimo na Mifugo, mbona mpaka leo tunaagiza ng’ombe nje ya nchi? Tuna ng’ombe 26 milioni, mbona tunaagiza nyama na maziwa kutoka nje?”

Utata wa uwekezaji

Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya Narco zinadai kuwa mkataba huo ulishinikizwa na ‘mamlaka za juu’ bila kufuata sheria za ununuzi na kanuni za uwekezaji.

“Suala hili lilifanyika tangu Agosti mwaka jana wakati nchi inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Ni wakati ambao hata Baraza la Mawaziri lilikuwa linaelekea kuvunjika na kulikuwa na shinikizo la wakubwa,” kilisema chanzo chetu ndani ya Narco. (shinikizo la wakubwa...ndiyo akina nani hao?)

Mtoa taarifa alisema katika majadiliano ya mkataba huo, Bodi ya Narco ilitaka Kampuni ya Overland ipewe hekta 10,000 pia ipewe miaka 33 ya kumiliki ardhi hiyo kwa majaribio, lakini kulikuwa na shinikizo kutoka ‘juu’ la kumilikisha ranchi hiyo kwa miaka 99.

“Kulikuwa na mvutano mkubwa, ikabidi suala hilo lifikishwe kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alibadilisha baadhi ya vipengele kikiwamo cha kuvunja mkataba kama mwekezaji hatatimiza masharti,” alisema.

Hata hivyo, AG Masaju alisema: “Sijawahi kushinikizwa na kusaini mkataba wowote na wala kwa jambo lolote lile.”

Habari zinasema baada ya mvutano mkali, iliamuliwa Kampuni ya Overland ipewe miaka 66 ya umiliki wa ardhi hiyo.

Narco

Meneja wa Masoko Narco, Immanuel Mnzava alisema uwekezaji huo ulifanyika kwa lengo zuri japokuwa ulitokana na shinikizo kutoka ngazi za juu.

“Ranchi ya Mzeri inaendeshwa kwa ubia kwa uwekezaji wa kisasa kwa sababu hatukuwa na mtaji wa kutosha. Mambo mengine siwezi kukueleza hadi Meneja Mkuu aje ataeleza, lakini kulikuwa na shinikizo kutoka ngazi za juu,” alisema.

Narco ni miongoni mwa mashirika yaliyowekwa chini ya Tume ya Rais ya Ubinafsishaji Mashirika ya Umma (PSRC) na baadaye CHC na sasa chini ya Msajili wa Hazina.

Mwaka 2006, Baraza la Mawaziri liliagiza Narco igawanye maeneo yake sehemu mbili kwa mita 2,500 hadi 4,000 na vitalu vigawanywe kwa wafugaji wazalendo na eneo linalobaki libaki kuwa la mfano kwa wananchi wanaozunguka.

Vitalu hivyo vilitolewa kwa wawekezaji wazawa kwa njia ya ushindani. Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuna vitalu 121 vilivyogawanywa kwa wawekezaji hao, wengi wao wakiwa watu mashuhuri.

“Mchakato ulikuwa wazi kwani mwekezaji alitakiwa kuja na barua ya Serikali za Mitaa, wizara na taarifa zake za fedha. Wamepewa vitalu hivyo kwa miaka 33 kisha itaangaliwa upya,” alisema Mnzava.

Kaimu Meneja Mkuu wa Narco, Bwire Kafumu alisita kuzungumzia suala hilo kwa kina kwa maelezo kwamba vyombo vya dola vinachunguza mkataba huo.

“Mimi hapa ninakaimu tu nafasi, siyo ‘General Manager’. Suala la Mzeri na Overland liko kwa Msajili wa Hazina na mamlaka nyingine zinachunguza. Msajili wa Hazina ndiye mwenye dhamana na mashirika yote ya umma. Kuna mamlaka nyingine pia zinashughulikia. Tuwe na subira tu, siwezi kueleza maana nitakuwa naingilia,” alisema Bwire.

Hata hivyo, alisisitiza, “Siyo kila mara katika uwekezaji kunakuwa na ushindani, kama amepatikana mwekezaji na ana sifa anapewa tu.”

Bwire alikaimishwa nafasi hiyo, Desemba mwaka jana baada ya aliyekuwa Meneja Mkuu, Dk John Mbogoma na bodi yote ya wakurugenzi kusimamishwa kazi na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba kutokana na kutoridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa katika eneo la Ruvu.

Kuhusu utata huo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola alisema: “Takukuru tunafanya uchunguzi, inawezekana upo, lakini mpaka nifuatilie ili kujua kama kweli upo.”
 
Tatizo ni majina tu si mkataba.

Mi ranchi wamejibinafsishia akina Lowassa na haina faida yoyote kwa serikali zaidi ya kuzalisha fedha ambazo sasa zinaipinga serikali na haiwi mwao. Lakini hii ranchi pekee ambayo imeonesha tija na mafanikio kwa nchi na serikali na inayoelekea kuwa mfano wa kuigwa ndiyo itapigwa vita na wale wale. Sababu?

Hakuna zaidi ila majina tu.
 
[QUOHi "sensor, post: 16340744, member: 270875"]Shinikizo kutoka 'ngazi za juu'

Eeeeeh kheeee!!! Ngazi za juuu[/QUOTE]
Leo hii mzawa akiwa na kitu tuna haha lakini mijitu mingine wanyonyaji kutoka nje wakimiliki mali zetu tunashangilia. Hakuna nchi yenye maendeleo endelevu kwa Uchumi wake kushikiliwa na watu wa nje iko siku uchumi husika utayumba tujitahidi kuwapa watu wetu nafasi ya kuwekeza katika taifa Lao.
 
Mkataba umesainiwa kwa shinikizo kutoka juu karibia kabisa na Oct 2015 wakati wa kampeni....baraza la mawaziri halina nguvu tena watu wana focus majimboni ndio vitu hivi vikapitishwa! Shinikizo toka juu ni wapi hulo? Nani anahusika huko juu?
Tatizo ni majina tu si mkataba.

Mi ranchi wamejibinafsishia akina Lowassa na haina faida yoyote kwa serikali zaidi ya kuzalisha fedha ambazo sasa zinaipinga serikali na haiwi mwao. Lakini hii ranchi pekee ambayo imeonesha tija na mafanikio kwa nchi na serikali na inayoelekea kuwa mfano wa kuigwa ndiyo itapigwa vita na wale wale. Sababu?

Hakuna zaidi ila majina tu.
 
Mkataba umesainiwa kwa shinikizo kutoka juu karibia kabisa na Oct 2015 wakati wa kampeni....baraza la mawaziri halina nguvu tena watu wana focus majimboni ndio vitu hivi vikapitishwa! Shinikizo toka juu ni wapi hulo? Nani anahusika huko juu?
Nchi inaliwa na kina Faisal Awadh na Dk Sharif Hamad.
Kweli Baba Ritz amewatengenezeeni Wafilisti pepo hapahapa duniani
 
''SIRI zinazohusu utajiri na mipango ya baadaye ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tisa wa Tanzania, Edward Lowassa, baada ya kuachia wadhifa wake kwa kutajwa katika kashfa ya Kampuni ya Richmond, zimeanza kufichuliwa.

Aidha, shaka nyingine inayojitokeza ni usiri uliopo kati ya Lowassa na Kampuni ya Olospa inayodaiwa kuwa licha ya kutambuliwa kama mmiliki wa ranchi hiyo na NARCO, jina la Lowassa halimo katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Kwamba katika misingi ya uadilifu wa uongozi, Lowassa alipaswa kutangaza mapema masilahi yake katika Kampuni ya Olospa ili asishirikishwe katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya maombi ya kampuni hiyo ya kutaka kumilikishwa ranchi hiyo.

Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima wiki iliyopita kupitia simu yake ya kiganjani, Lowassa alikiri kumiliki ranchi hiyo na kueleza kwamba haoni kosa lolote kuwa mmiliki wa ranchi hiyo kwa sababu hapakuwa na sheria ya kumzuia kuinunua''.
 
Tatizo ni majina tu si mkataba.

Mi ranchi wamejibinafsishia akina Lowassa na haina faida yoyote kwa serikali zaidi ya kuzalisha fedha ambazo sasa zinaipinga serikali na haiwi mwao. Lakini hii ranchi pekee ambayo imeonesha tija na mafanikio kwa nchi na serikali na inayoelekea kuwa mfano wa kuigwa ndiyo itapigwa vita na wale wale. Sababu?

Hakuna zaidi ila majina tu.
''SIRI zinazohusu utajiri na mipango ya baadaye ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tisa wa Tanzania, Edward Lowassa, baada ya kuachia wadhifa wake kwa kutajwa katika kashfa ya Kampuni ya Richmond, zimeanza kufichuliwa.

Aidha, shaka nyingine inayojitokeza ni usiri uliopo kati ya Lowassa na Kampuni ya Olospa inayodaiwa kuwa licha ya kutambuliwa kama mmiliki wa ranchi hiyo na NARCO, jina la Lowassa halimo katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Kwamba katika misingi ya uadilifu wa uongozi, Lowassa alipaswa kutangaza mapema masilahi yake katika Kampuni ya Olospa ili asishirikishwe katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya maombi ya kampuni hiyo ya kutaka kumilikishwa ranchi hiyo.

Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima wiki iliyopita kupitia simu yake ya kiganjani, Lowassa alikiri kumiliki ranchi hiyo na kueleza kwamba haoni kosa lolote kuwa mmiliki wa ranchi hiyo kwa sababu hapakuwa na sheria ya kumzuia kuinunua''.
kama amekubali kumiliki hiyo ranchi basi sawa. Nilijua ataikana kama lile pori la Makuyuni. Hata Vodacom ipo siku atakiri pia. Na kama amekiri kumiliki hiyo ranchi ambayo umiliki wake na menejiment vyote hamna jina lake, basi naamini kuna rasilimali nyingi nchini ni za kwake hata magodown yaliyoficha sukari anamiliki kwa kutumia majina bandia. Yaani ni sawa na ITV utafute kuanzia mwanzo hadi mwisho jina la R. Mengi lisiwepo. Asante Mungu, fisadi linazidi kujileta.
 
Wanatutisha ati Meli inakuja na Ng'ombe, si wakafugie huko kwao! Wamewanyang'anya wenyeji wa ile nchi ardhi yao na sasa wenyeji wanaishi maporini. Mtu anakuja na vimilioni vyake anapewa hisa 70% huku tumetoa ekari 20,000 za ardhi kwa miaka 66!! Thamani ya hiyo ardhi ni kiasi gani?

Nyerere aliposema tusichimbe madini hadi tuwe na uwezo hakukosea. Hivi hatuna uwezo wa kufuga kweli?
Mkuu Mwigulu Nchemba onyesha weredi hapa. tafuta Watanzania watatu wenye nia ya kufuga, wawezeshe kwa kila namna wapewe hizo ranchi wafuge kwa faida ya watanzania.
 
Nchi inaliwa na kina Faisal Awadh na Dk Sharif Hamad.
Kweli Baba Ritz amewatengenezeeni Wafilisti pepo hapahapa duniani

Naam, hayo majina ndiyo tatizo. Laiti kama ingekuwa Tom, Dick na Harry kusingekuwa na tatizo lolote.
 
''SIRI zinazohusu utajiri na mipango ya baadaye ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tisa wa Tanzania, Edward Lowassa, baada ya kuachia wadhifa wake kwa kutajwa katika kashfa ya Kampuni ya Richmond, zimeanza kufichuliwa.

Aidha, shaka nyingine inayojitokeza ni usiri uliopo kati ya Lowassa na Kampuni ya Olospa inayodaiwa kuwa licha ya kutambuliwa kama mmiliki wa ranchi hiyo na NARCO, jina la Lowassa halimo katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Kwamba katika misingi ya uadilifu wa uongozi, Lowassa alipaswa kutangaza mapema masilahi yake katika Kampuni ya Olospa ili asishirikishwe katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya maombi ya kampuni hiyo ya kutaka kumilikishwa ranchi hiyo.

Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima wiki iliyopita kupitia simu yake ya kiganjani, Lowassa alikiri kumiliki ranchi hiyo na kueleza kwamba haoni kosa lolote kuwa mmiliki wa ranchi hiyo kwa sababu hapakuwa na sheria ya kumzuia kuinunua''.

Hii habari yako inajichanganya, Aya ya kwanza unasema jina la Lowasa halimo, Aya ya mwisho unanukuu majibu ya Lowassa. Kipi ni kipi boss wangu.?? Hebu fanya marekebisho habari inoge zaidi waweza kuta hii ikapitisha jina lako kwenye ile list mpya.
 
Tatizo ni majina tu si mkataba.

Mi ranchi wamejibinafsishia akina Lowassa na haina faida yoyote kwa serikali zaidi ya kuzalisha fedha ambazo sasa zinaipinga serikali na haiwi mwao. Lakini hii ranchi pekee ambayo imeonesha tija na mafanikio kwa nchi na serikali na inayoelekea kuwa mfano wa kuigwa ndiyo itapigwa vita na wale wale. Sababu?

Hakuna zaidi ila majina tu.
Si kweli naijua vizuri kampuni ya ranchi za taifa. Tatizo la hii kampuni ni uongozi hasa menejiment iliyopita ambayo Mwiguru aliisimamisha walikuwa wapiga dili. Lowasa aliondoka muda mrefu katika wadhifa wa waziri wa maji na mifugo na baadae mawaziri wengi walifuata akina Kawambwa, Magufuli, Mathayo David na wengineo lakini walishindwa kabisa kushughulikia kiini cha tatizo la uongozi hadi Mwiguru alipokuja kuusimamisha juzi. Hii mikataba ya hovyo yote imeingiwa kipindi hiki Loawasa akiwa nje ya serikali.
 
Inaonekana hawa wawekezaji wanatumia udhaifu wetu kwamba kwakuwa hakuna ranchi yoyote hapa iluyofanikiwa kiutendaji kwa hiyo waingie mkataba kinyemela tena kwa jeuri. Hii kimsingi haiwezekani lazima kuwe na maslahi ya taifa.

Lakini suali kuu ninalojiuliza ni ipi nafasi ya wasomi wetu hususani katika nyanja hii ya mifugo na viwanda. Laiti tungekuwa na sera madhubuti za kuwatumia wasomi wetu tatizo la ajira lingekoma kabisa.
Tunazalisha wasomi ambao hawana mahali pakushika. Hivi tumelogwa na nani kazi ya kuzalisha na kuchunga ngombe kiutaalamu inatushinda kweli? huku tunao wasomi wenye masters mpaka Proffesors.
Hii ni aibu kubwa sana kwa taifa kushindwa kuendesha NARCO secta ambayo ipo ndani ya uwezo wetu. Ni kiongozi gani mzalendo atakaye ona haya mambo baadala ya kuzalisha wasomi watakaotetea maslahi ya taifa hili ambalo limepoteza dira.

Kila kitu wawekezaji wawekezaji! Wawekezaji tumewafanya miungu ya Tanzani. Kwakweli inafedhehesha sana hata kwenye kuchunga ngombe tunaweka wawekezaji.
 
Mwekezaji wa kwanza hapa kwetu nadhani alikuwa Carl Peters. Huyo alitupa chumvi tu, na sisi tukampa nchi. Sasa wamebadilisha kidogo. Wanaahidi watafanya maajabu kwenye ardhi yetu, na sisi tunaachia ardhi kwa hizo ahadi. Huwa kazitimii.

Kuna watu wanafukuzwa kwenye makazi yao kwa madai ya "kupatikana mwekezaji". Hao wananchi walikuwa wanadhani wao "wamewekeza" vitu vyao vidogo vidogo. Huu ugonjwa wa uwekezaji wa sasa hauna tofauti na ule wa wakati wa Carl Peters. Kiwango cha ulimbukeni ni kile kile na namna ya kutumia viongozi kunyonya wananchi ni ile ile. Na viongozi wa sasa hawajawazidi akili wale wa wakati wa Carl Peters.
 
Back
Top Bottom