Orodha ya Watanzania waliolitumikia taifa kwa Uzalendo mkubwa ambao wametambuliwa na kukumbukwa chini ya Uongozi wa Rais Magufuli

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Tangu kuingia madarakani mwaka 2015, ifuatayo ni orodha ya baadhi ya Watanzania ambao walilitumikia taifa kwa moyo wa kizalendo ambao Rais kutokana na utamaduni wake wa kupenda kutambua michango na juhudi za watu mbalimbali, aliamua ama kuwatambua kwa mara ya kwanza au kuendelea kuwatambua baada ya serikali za nyuma kufanya hivyo:

a)JUMANNE NGOMA
Mgunduzi wa madini ya Tanzanite, ambayo yanapatikana Tanzania pekee dunia nzima. Licha ya kupewa cheti cha kutambuliwa na Serikali Oktoba 10, 1980 na Mwl Nyerere na kingine mwaka 1984. Mnamo April 6, 2018 Rais Magufuli akiwa katika uzinduzi wa ukuta wa Mererani aliendelea kutambua mchango wake kwa taifa kwa kumzawadia fedha taslimu tsh 100,000,000 pamoja na mambo mengine zimsaidie katika matibabu ya maradhi yanayomsumbua.

b) PATRICK MFUGALE
Mhandisi mbombezi ambaye amelitumikia taifa kupitia TANROAD katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo mkurugenzi wa barabara, mhandisi mkuu wa madaraja n.k na kufanikisha ujenzi wa madaraja ya Rufiji(Pwani), Rusumo (Mara), Kikwete(Malagarasi Kigoma)na Nyerere (Kigamboni). Rais Magufuli kwa kutambua mchango wake alioutoa kwa muda mrefu aliagiza daraja la juu 'fly over' lililopo eneo la Tazara lipewe jina la MFUGALE.

c) MAZIZ MAPUNDA
Rubani mtaafu na wa kwanza kuendesha Ndege ya ATCL, enzi za utumishi wake anakumbukwa kwa ujasiri na uzalendo wa kuokoa ndege ya Tanzania miaka 1970. Inaelezwa wakati wa kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika mmashariki(1970) alikuwa na ndege ya Tanzania lakini ilipotolewa maelelkezo ndege zote ziegeshwe Nairobi yeye kwa Uzalendo wa Nchi yake(Tanzania) hakufanya hivyo aliirusha na kuileta nchini bila kujali hatari ambayo angeweza kuipata. Jana Rais wakati wa kupokea ndege ya airbus A220 - 300 alimzawadia fedha tasilimu tsh 10,000,000 na kuagiza akiwa na safari yeye na mke wake wapande bure kwenye ndege za ATCL.

d) Wengine ni marehemu FRANCIS NGOSHA ambaye ni mchoraji na mbunifu wa Nembo ya taifa ambapo Serikali alipopatwa na maradhi iligharamikia matibabu yake na rais alikwenda kumjulia hali wakati amelazwa muhimbili, hata pale Mungu alipoamua kumuita( fariki) Serikali iligharamikia gharama zote za mazishi na usafiri.

Kutokana na matukio hayo ambayo Rais ameyafanya tunajifunza kuwa:

i) Watanzania tuendelee kujituma kufanya kazi kwa ajili ya taifa bila kutanguliza maslahi binafsi, kwani ipo siku michango yetu itatambulika kitaifa.

ii) Rais Magufuli ameonesha utofauti katika uongozi wake kwake yeye hasubir mtu afariki ndipo aanze kummwagia sifa, anazitoa na kutambua mchango wa kila mtu hasa ule wa kizalendo ungali hai (rejea tukio la MFUGALE)

iii) vyama vya siasa hasa vya upinzani navyo visibaki nyuma, vianze utamaduni wa kuipongeza Serikali inapofanya mambo mazuri mathalani ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa bwawa la kufua umeme 'stigliers gorge' na ununuzi wa ndege, visisubiri rais aondoke madarakani ndipo vianza kumsifia kama ilivyo kwa JK.

iv) Serikali itunge sheria itakayotoa mwongozo wa kila mtanzania anayefanya jambo la kiuzalendo lenye manufaa makubwa kwa taifa atambuliwe, apewe zawaidi n.k kwani kuna uwezekano akaja Rais ambaye hana moyo wa kiuzalendo kama MAGUFULI utamaduni huo ukapotea kabisa.

v)Kuna faida kubwa ya kuwa mzalendo kwa taifa lako, fikiria jina la MFUGALE litakavyodumu vizazi hadi vizazi, wakati wengine majina yetu hufutika muda mfupi tu baada ya kumaliza safari yetu ya duniani.

vii) Kuwa mzalendo hakuhitaji nafasi kubwa za kiuongozi na madaraka Kama vile Rais, Wazir, Mbunge, mkurugenzi kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuwa mzalendo tena kwa kiwango cha kitaifa rejea uzalendo wa Mzee NGOMA na NGOSHA hawa walikuwa wananchi wa kawaida kabisa kipindi wanajitoa kwa ajili ya taifa!
 
Ungeleta na orodha ya waliofikwa na madhira baada ya ujio wa jamaa na mpaka sasa majina yao kuwa chini ya viwango ingawa kitambo hiko walikuwa madon na watu wenye wadhiwa wao ingekuwa safi sana.
 
Hili neno uzalendo mbona linatumika sana awamu hii? Neno hili hutumiwa na madikteta kutaka kuhalalisha ubaguzi wa kundi fulani la watu wanaowapinga au wenye mtazamo tofauti. Madikteta hutumia mwanya huo kuwasweka ndani wapinzani wao ambao wanawaona siyo "wazalendo".
 
Vijana wa si

vijana wa siku mmekua katika kipindi ambacho kumekuwa na mdororo wa elimu ya uzalendo lakini tuliozaliwa enzi za mwalimu elimu ya uzalendo ilikuwa kila pahala
 
mfugale mtoe kabisa hapo,anatumika na mkuru kupitisha harama tanroads
 
Iko siku Tundu lissu nae atapewa mabilioni kwa uzalendo wake wakuwa muwazi na kutoa kwake ushauri juu ya nn kifanyike ili nchi ipate faida ktk madini na kipoozeo juu ya madhila yaliomfika yeye mwenyewe
 
Hili neno uzalendo mbona linatumika sana awamu hii? Neno hili hutumiwa na madikteta kutaka kuhalalisha ubaguzi wa kundi fulani la watu wanaowapinga au wenye mtazamo tofauti. Madikteta hutumia mwanya huo kuwasweka ndani wapinzani wao ambao wanawaona siyo "wazalendo".
Mkuu kuna neno umeliacha hapo kwenye uzalendo jinsi linavyotumika. Ungesema kabisa neno uzalendo awamu hii linatumika kipumbavu sana!
 
Umemsahau Tundu Antipas Lisu. Kiboko yao
Tangu kuingia madarakani mwaka 2015, ifuatayo ni orodha ya baadhi ya Watanzania ambao walilitumikia taifa kwa moyo wa kizalendo ambao Rais kutokana na utamaduni wake wa kupenda kutambua michango na juhudi za watu mbalimbali, aliamua ama kuwatambua kwa mara ya kwanza au kuendelea kuwatambua baada ya serikali za nyuma kufanya hivyo:

a)JUMANNE NGOMA
Mgunduzi wa madini ya Tanzanite, ambayo yanapatikana Tanzania pekee dunia nzima. Licha ya kupewa cheti cha kutambuliwa na Serikali Oktoba 10, 1980 na Mwl Nyerere na kingine mwaka 1984. Mnamo April 6, 2018 Rais Magufuli akiwa katika uzinduzi wa ukuta wa Mererani aliendelea kutambua mchango wake kwa taifa kwa kumzawadia fedha taslimu tsh 100,000,000 pamoja na mambo mengine zimsaidie katika matibabu ya maradhi yanayomsumbua.

b) PATRICK MFUGALE
Mhandisi mbombezi ambaye amelitumikia taifa kupitia TANROAD katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo mkurugenzi wa barabara, mhandisi mkuu wa madaraja n.k na kufanikisha ujenzi wa madaraja ya Rufiji(Pwani), Rusumo (Mara), Kikwete(Malagarasi Kigoma)na Nyerere (Kigamboni). Rais Magufuli kwa kutambua mchango wake alioutoa kwa muda mrefu aliagiza daraja la juu 'fly over' lililopo eneo la Tazara lipewe jina la MFUGALE.

c) MAZIZ MAPUNDA
Rubani mtaafu na wa kwanza kuendesha Ndege ya ATCL, enzi za utumishi wake anakumbukwa kwa ujasiri na uzalendo wa kuokoa ndege ya Tanzania miaka 1970. Inaelezwa wakati wa kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika mmashariki(1970) alikuwa na ndege ya Tanzania lakini ilipotolewa maelelkezo ndege zote ziegeshwe Nairobi yeye kwa Uzalendo wa Nchi yake(Tanzania) hakufanya hivyo aliirusha na kuileta nchini bila kujali hatari ambayo angeweza kuipata. Jana Rais wakati wa kupokea ndege ya airbus A220 - 300 alimzawadia fedha tasilimu tsh 10,000,000 na kuagiza akiwa na safari yeye na mke wake wapande bure kwenye ndege za ATCL.

d) Wengine ni marehemu FRANCIS NGOSHA ambaye ni mchoraji na mbunifu wa Nembo ya taifa ambapo Serikali alipopatwa na maradhi iligharamikia matibabu yake na rais alikwenda kumjulia hali wakati amelazwa muhimbili, hata pale Mungu alipoamua kumuita( fariki) Serikali iligharamikia gharama zote za mazishi na usafiri.

Kutokana na matukio hayo ambayo Rais ameyafanya tunajifunza kuwa:

i) Watanzania tuendelee kujituma kufanya kazi kwa ajili ya taifa bila kutanguliza maslahi binafsi, kwani ipo siku michango yetu itatambulika kitaifa.

ii) Rais Magufuli ameonesha utofauti katika uongozi wake kwake yeye hasubir mtu afariki ndipo aanze kummwagia sifa, anazitoa na kutambua mchango wa kila mtu hasa ule wa kizalendo ungali hai (rejea tukio la MFUGALE)

iii) vyama vya siasa hasa vya upinzani navyo visibaki nyuma, vianze utamaduni wa kuipongeza Serikali inapofanya mambo mazuri mathalani ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa bwawa la kufua umeme 'stigliers gorge' na ununuzi wa ndege, visisubiri rais aondoke madarakani ndipo vianza kumsifia kama ilivyo kwa JK.

iv) Serikali itunge sheria itakayotoa mwongozo wa kila mtanzania anayefanya jambo la kiuzalendo lenye manufaa makubwa kwa taifa atambuliwe, apewe zawaidi n.k kwani kuna uwezekano akaja Rais ambaye hana moyo wa kiuzalendo kama MAGUFULI utamaduni huo ukapotea kabisa.

v)Kuna faida kubwa ya kuwa mzalendo kwa taifa lako, fikiria jina la MFUGALE litakavyodumu vizazi hadi vizazi, wakati wengine majina yetu hufutika muda mfupi tu baada ya kumaliza safari yetu ya duniani.

vii) Kuwa mzalendo hakuhitaji nafasi kubwa za kiuongozi na madaraka Kama vile Rais, Wazir, Mbunge, mkurugenzi kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuwa mzalendo tena kwa kiwango cha kitaifa rejea uzalendo wa Mzee NGOMA na NGOSHA hawa walikuwa wananchi wa kawaida kabisa kipindi wanajitoa kwa ajili ya taifa!
 
Ungeleta na orodha ya waliofikwa na madhira baada ya ujio wa jamaa na mpaka sasa majina yao kuwa chini ya viwango ingawa kitambo hiko walikuwa madon na watu wenye wadhiwa wao ingekuwa safi sana.
Ilete wewe hiyo orodha. Yaani watu hamna jema?!
 
Hili neno uzalendo mbona linatumika sana awamu hii? Neno hili hutumiwa na madikteta kutaka kuhalalisha ubaguzi wa kundi fulani la watu wanaowapinga au wenye mtazamo tofauti. Madikteta hutumia mwanya huo kuwasweka ndani wapinzani wao ambao wanawaona siyo "wazalendo".
Kwa hiyo ulitaka wasiswekwe ndani hata kama wanafanya makosa ya kisheria..? Huo ni mtazamo wako..hata wewe ukivunja sheria unaswekwa ndani tu..jaribu uone..hakuna mudawa kubembelezana katika uendeshaji wa nchi..awamu iliyopita mlichezea sana serikali
 
Back
Top Bottom