Oparesheni 255 yatikisa Nchi, Magazeti yaanza kuishambulia CHADEMA ili kuokoa CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,343
FB_IMG_1684874501884.jpg

Tulionya Mapema sana kwamba tukipewa nafasi ya kupanda kwenye majukwaa kwenye mikutano ya hadhara na kuongea na wananchi, tuna uwezo wa kuteketeza ccm kwa muda wa siku 7 tu na sasa imedhihirika rasmi kwamba bil Polisi na Tume ya Uchaguzi CCM ni wepesi kuliko Pamba.

Kuna taarifa zimevuja kwamba baada ya hoja nzito na za Ukweli zinazotolewa na CHADEMA kwenye oparesheni hiyo kuibabua CCM na serikali yake kumewekwa mkakati wa kuyatumia baadhi ya Magazeti kwa lengo la kuandika uongo kuhusu Chadema ili kupotosha wananchi (Orodha ya Magazeti hayo na majina yake tunayo), lakini kwa sababu za kimaadili tunayahifadhi kwa sasa.

Tunatambua baadhi ya Wahariri wanashinda kwenye korido za viongozi kwa lengo la kuomba msaada wa kuendeshea magazeti yao, hasa baada ya kupuuzwa na wananchi kutokana na kuandika habari za upande mmoja tu, na hivyo kudoda sokoni na kusababisha ugumu wa maisha kwao. Pamoja oparesheni ya Chadema kufukua mambo mengi mazito ya msingi sana kwa nchi yetu , Magazeti hayo hayaandiki habari hizo , bali yaamua kuunganisha uzushi wao na kuuchapisha .

Ushahidi wa kufirisika kwa Magazeti hayo ni kuundwa kwa Tume na Waziri wa Habari, Nape Nnauye iliyoelekezwa kuchunguza dhiki inayovikabili vyombo vya Habari vya Tanzania na hasa Magazeti kwa lengo la kuvisaidia .

Hata hivyo ni vema Magazeti hayo yakazingatia mwongozo na sheria za kusajiliwa kwake, ambavyo vinakataza kuandika habari za uongo kwa nia ovu, tena hasa baada ya kulipwa kwa Mkakati Maalum. Magazeti yanayo nafasi ya kujisahihisha kabla hatujaamua kuyashambulia hadharani na kuyamaliza kabisa wakakosa na hicho kidogo wanachopata.

Tunarudia tena kwa mara nyingine kuonya kwamba HAKUNA MAHALI POPOTE KWENYE DUNIA HII AMBAKO SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU.
 
Mwl Nyerere: HOJA haipigwi Rungu, HOJA hujibiwa Kwa HOJA.

Ni Kweli CHADEMA ni wamoja, na ni chama chenye ukomavu wa DEMOKRASIA.

Angalizo: Mh Lisu apewe support ya chama mguu wake ni mbovu,

Msirudie tena kumpandisha ktk majukwaa ya namna Ile.

Kama tatizo ni pesa semeni tuchangie .
 
Unayafahamu majukwaa waliyokuwa wanayatumia Mitume waliokuwa wanaeneza neno la Mungu ?

Kukomboa nchi si kazi ya lelemama inahitaji Uzalendo haswa , halafu kingine ni hiki , ni kweli kwamba Mguu wa Lissu ni Mbovu na tunatambua kuwa mnamuita CHIBA , bali mlichosahau ni kwamba LISSU HAKUTIBIWA MUHIMBILI

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Tulionya Mapema sana kwamba tukipewa nafasi ya kupanda kwenye majukwaa kwenye mikutano ya hadhara na kuongea na wananchi , tuna uwezo wa kuteketeza ccm kwa muda wa siku 7 tu , na sasa imedhihirika rasmi kwamba Bila Polisi na Tume ya Uchaguzi CCM ni wepesi kuliko Pamba .

Kuna Taarifa zimevuja kwamba baada ya hoja nzito na za Ukweli zinazotolewa na CHADEMA kwenye oparesheni hiyo kuibabua ccm na serikali yake kumewekwa mkakati wa kuyatumia baadhi ya Magazeti kwa lengo la kuandika uongo kuhusu Chadema ili kupotosha wananchi (Orodha ya Magazeti hayo na majina yake tunayo ) , lakini kwa sababu za kimaadili tunayahifadhi kwa sasa .

Tunatambua baadhi ya Wahariri wanashinda kwenye korido za viongozi kwa lengo la kuomba msaada wa kuendeshea magazeti yao , hasa baada ya kupuuzwa na wananchi kutokana na kuandika habari za upande mmoja tu , na hivyo kudoda sokoni na kusababisha ugumu wa maisha kwao , Ushahidi wa kufirisika kwa Magazeti hayo ni kuundwa kwa Tume na Waziri wa Habari , Nape Nnauye iliyoelekezwa kuchunguza dhiki inavyovikabili vyombo vya Habari vya Tanzania na hasa Magazeti .

Hata hivyo ni vema Magazeti hayo yakazingatia mwongozo na sheria za kusajiliwa kwake , ambavyo vinakataza kuandika habari za uongo kwa nia ovu , tena hasa baada ya kulipwa kwa Mkakati Maalum , Magazeti yanayo nafasi ya kujisahihisha kabla hatujaamua kuyashambulia hadharani na kuyamaliza kabisa wakakosa na hicho kidogo wanachopata .

Tunarudia tena kwa mara nyingine kuonya kwamba , HAKUNA MAHALI POPOTE KWENYE DUNIA HII AMBAKO SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU
 
Kuibabua CCM na Serikali yake..!!!!! Kumbe siyo habari ya Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi?
 
Back
Top Bottom