Onyo kwa CHADEMA na angalizo kwa Dr. Slaa - We are watching you!

Nchi yetu ni moja kati ya nchimasikini duni sana duniani japo ina rasilimali nyingi kuliko hata baadhi ya nchi ambazo zimeendelea na ni wahisani wetu wa maendeleo. Kuna sababu nyingi za hali hiyo lakini kwa leo sijapanga kuingia kwa undani sababu za umasikini wetu.Nchi yetu inakabiliwa na changamoto nyingi katika kukabiliana na umasikini wa kipato kwa wananchi wake,kukuza pato la taifa, ukosefu wa ajira kwa vijana, mikopo ya elimu ya juu,kuboresha kilimo chetu ambacho kinaajiri zaidi ya 80% ya watanzania wote na pia kurekebisha mfumo wetu wa elimu ili kuwezesha wahitimu wetu kujiajiri na sikusubiri kuajiriwa.

Hivi karibuni kiasi kikubwa chagesi asilia kimegundulika nchini katika mkoa wa Mtwara. Hii inaongeza idadi ya rasilimali zilizokwisha kugundulika nchini ikiwa imetanguliwa na almasi,dhahabu, tanzanite na madini mengine. Vilevile kuna matumaini ya mafuta kugundulika nchini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinazoendelea katika fukwe za bahari yetu.Hivyo nchi yetu inahitaji uongozi thabiti ili kuhakikisha rasilimali hizi zinanufaisha watanzania wote na kuwaletea maendeleo hivyo kuondokana na umasikini. Uwepo wa rasilimali hizi bila kuwepo uongozi thabiti,shirikishi na sikivu unaweza kuitumbukiza nchi yetu katika kile kinachoitwa laana ya rasilimali au kwa kimombo resources curse. Ambayo si kingine bali machafuko ndani ya nchi sababu ya wananchi kutonufaika na zawadi hii kutoka kwa mwenyezi Mungu.

Mwaka 2015 nchi itafanya uchaguzi mkuu wa tano tangu vyama vingi viruhusiwe tena nchini mwaka 1992. Kuna wanasiasa kadhaa wanatajwa kujipanga/kujiandaa kugombea urais ili kumrithi Rais Kikwete hawa ni kutoka chama tawala na vyama vya upinzani. Kwa leo nataka kumjadili Dr Wilbroad Slaa katibu mkuu wa CHADEMA ambaye aligombea urais mwaka2010 na kuangushwa na Rais Kikwete. Dr Slaa ana shahada ya uzamivu katikas heria za kanisa. Ikumbukwe kuwa Dr Slaa amepata kuwa padri wa kanisa katoliki na kufikia kuwa katibu mtendaji mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania(TEC). Napata tabu kuoanisha sifa hizi za kitaaluma za Dr Slaa na changamoto zinazoikabili nchi yetu kwa sasa kama nilivyoziainisha kwa uchache hapo juu. Kweli ni msomi na ana uzoefu wa kiuongozi lakini si katika jamii pana bali katika shughuli za kanisa hivyo nina mashaka na weredi wake kitaaluma katika masuala hayo yanayolikabili taifa kwasasa. Wako watakaosema Rais ana washauri katika nyanja zote, lakini ni vema kuwa na Rais mwenye taaluma sahihi kwa maendeleo ya jamii nzima na si kundi mojal inalofungamana na imani yake tu.

Tukiachana na masuala ya kielimuDr Slaa anatajwa kuwa kiongozi imla, hili liko wazi ukiangalia zoezi la timuatimua linaloendelea ndani ya chama hicho. Habari za ndani zinasema wahanga wengi wa timuatimua ndani ya CHADEMA ni wale ambao kwa namna moja au nyingine wamewahi kutofautiana kimtazamo, kifkra na hata kimkakati na Dr Slaa. Kwakifupi Dr Slaa ni mtu asiyevumilia mawazo tofauti na yake. Pia Dr Slaa hana udhibiti wa familia yake, “mkewe” Josephine amekuwa akiingilia sana shughuli za kiutendaji ndani ya CHADEMA kwa kivuli cha “mumewe” wakati yeye hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho.Itafakari Tanzania yenye rasilimali lukuki; gesi, almasi, mafuta, dhahabu, wanyama pori nk ikiwa chiniya Rais asiyeshirikisha wenzie katika maamuzi hivyo kuendesha nchi kwa maono na mawazo yake pekee. Rais asiye na udhibiti wa familia yake kiasi cha “mkewe”kuingilia watendaji na utendaji wa shughuli za umma huku Rais akiwa hana kauli. Je tutasalimika kweli RESOURCES COURSE chini ya Dr Slaa? Jibu langu HAPANA.


Hakuna mtu duniani ambaye amewahi kuwa everything. Na hatuwezi kuchagua rais kwa kuangalia kuwa ana profession hii. Kuwa kiongozi wa umma ni ku-oversee taasisi na urais ni taasisi ndio maana kiongozi wake mkuu anakuwa na taaluma moja au mbili lakini anao wasaidizi wenye professional carriers mbalimbali na ambao wanaunganisha tija, ujuzi, uzoefu na elimu yao katika kuendesha nchi. Halafu umesema alikuwa ni padre na akafikia kuwa na cheo cha katibu mkuu wa TEC. Alikuwa haongozi maaskofu bali taasisi nzima ya Kanisa Katoliki Tanzania lenye miradi mingi ya shule, vyuo, hospitali,zahati, kilimo, viwanda vidogovidogo na vyote hivi vinahudumia na vina interaction ya watu mbalimbali wa dini tofauti na wasiokuwa na dini. Huu ni uzoefu toja wenye diversity ya hali ya juu na unaboreshwa na uzoefu wake kwenye siasa.

Halafu ukumbuke nchi inaongozwa na sheria na ndio maana tunasema uongozi wa sheria. Vitu vyote ulivyotajwa vina sheria zake (acts) na haitakuja iwe kwamba rais aamue kuweka sheria pembeni ili matakwa yake ndio yatimie halafu abaki salama. Tunaenda kwenye katiba mpya naona mambo yatakuwa safi. Lakini Dr.Slaa tunayemjua tangu aingie harakati za ukombozi si mtu wa aina hiyo. He's not greedy, not glutton, not hyneous. Labda kama unatwambia mwingine. Sitegemei awe mlafi akiwa rais abaki salama.

Swala la mama Josephine naona ni fabricated story ambayo imekosa evidence. Nilitegemea wewe mleta uzi ungetuletea researched findings and facts ili utete hoja yako. Bahati mbaya na wewe umebaki kuwa na source ya kijiweni. This is very bad to write based on cacaphony song na watu wanaoeneza mambo hayo ambao hivi juzi wamevuliwa nguo na wako wanahaha. Halafu CDM ni taasisi ambayo imeonyesha kwa vitendo kuwa bold na principled. Haiwezi kuwa driven na msichukue jinsi CCM first ladies wanavyofanya mkafikiri ndivyo CDM itakavyokuwa kama kitakuwa kwenye uongozi wa nchi. These are not correlative at all.

Kuwa kiongozi wa kiimla same as swala mke na ndoa yake. Fabricated stories maana CDM ni taasisi iliyo na transparency na fare treatment
 
Mwakidondo,Jf,wananchi,kwenye madaladala,kwenye tax, wanamzungumzia Dr Slaa.Viongozi wa kitaifa wanamzungumia Dr Slaa,W.J Malecela anamzungumzia Dr Slaa,Ukienda saluni kunyoa wanamzungumzia Dr slaa,demu wangu kaenda saluni kusuka nako wanamzungumzia Dr. slaa.Nimempeleka Mwanangu shule nako wanamzungumzia Dr .slaa.Wakulima na wafanyakazi nao wanamzungumzia Dr. slaa.Nape na Nchemba wanamzungumzia Dr slaa,Waandishi habari(makanjanja)wanamzungumzia Dr. slaa,Masalia(pindua mbowe0 wanamzungumzia Dr.slaa.

Huyu mtu anawanyima usingizi sana magamba.
Huyu Dr Slaa ndiye Watanzania tunayemhitaji 2015 awe Rais wetu
 
Nchi yetu ni moja kati ya nchimasikini duni sana duniani japo ina rasilimali nyingi kuliko hata baadhi yanchi ambazo zimeendelea na ni wahisani wetu wa maendeleo. Kuna sababu nyingi zahali hiyo lakini kwa leo sijapanga kuingia kwa undani sababu za umasikini wetu.Nchi yetu inakabiliwa nachangamoto nyingi katika kukabiliana na umasikini wa kipato kwa wananchi wake,kukuza pato la taifa, ukosefu wa ajira kwa vijana, mikopo ya elimu ya juu,kuboresha kilimo chetu ambacho kinaajiri zaidi ya 80% ya watanzania wote na piakurekebisha mfumo wetu wa elimu ili kuwezesha wahitimu wetu kujiajiri na sikusubiri kuajiriwa. Hivi karibuni kiasi kikubwa chagesi asilia kimegundulika nchini katika mkoa wa Mtwara. Hii inaongeza idadi yarasilimali zilizokwisha kugundulika nchini ikiwa imetanguliwa na almasi,dhahabu, tanzanite na madini mengine. Vilevile kuna matumaini ya mafutakugundulika nchini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinazoendelea katika fukweza bahari yetu.Hivyo nchi yetu inahitaji uongozithabiti ili kuhakikisha rasilimali hizi zinanufaisha watanzania wote nakuwaletea maendeleo hivyo kuondokana na umasikini. Uwepo wa rasilimali hizibila kuwepo uongozi thabiti na sikivu unaweza kuitumbukiza nchi yetu katikakile kinachoitwa laana ya rasilimali au kwa kimombo resources curse. Ambayo si kingine bali machafuko ndani ya nchisababu ya wananchi kutonufaika na zawadi hii kutoka kwa mwenyezi Mungu.Mwaka 2015 nchi itafanya uchaguzimkuu wa tano tangu vyama vingi viruhusiwe tena nchini mwaka 1992. Kunawanasiasa kadhaa wanatajwa kujipanga/kujiandaa kugombea urais ili kumrithi RaisKikwete hawa ni kutoka chama tawala na vyama vya upinzani. Kwa leo natakakumjadili Dr Wilbroad Slaa katibu mkuu wa CHADEMA ambaye aligombea urais mwaka2010 na kuangushwa na Rais Kikwete. Dr Slaa ana shahada ya uzamivu katikasheria za kanisa. Ikumbukwe kuwa Dr Slaa amepata kuwa padri wa kanisa katolikina kufikia kuwa katibu mtendaji mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania(TEC).Napata tabu kuoanisha sifa hiziza kitaaluma za Dr Slaa na changamoto zinazoikabili nchi yetu kwa sasa kamanilivyoziainisha kwa uchache hapo juu. Kweli ni msomi na ana uzoefu wakiuongozi lakini si katika jamii pana bali katika shughuli za kanisa hivyo ninamashaka na weredi wake kitaaluma katika masuala hayo yanayolikabili taifa kwasasa. Wako watakaosema Rais ana washauri katika nyanja zote, lakini ni vemakuwa na Rais mwenye taaluma sahihi kwa maendeleo ya jamii nzima na si kundi mojalinalofungamana na imani yake tu.Tukiachana na masuala ya kielimuDr Slaa anatajwa kuwa kiongozi imla, hili liko wazi ukiangalia zoezi la timuatimua linaloendelea ndani ya chama hicho. Habari za ndani zinasema wahangawengi wa timuatimua ndani ya CHADEMA ni wale ambao kwa namna moja au nyinginewamewahi kutofautiana kimtazamo, kifkra na hata kimkakati na Dr Slaa. Kwakifupi Dr Slaa ni mtu asiyevumilia mawazo tofauti na yake. Pia Dr Slaa hanaudhibiti wa familia yake, "mkewe" Josephine amekuwa akiingilia sana shughuli zakiutendaji ndani ya CHADEMA kwa kivuli cha "mumewe" wakati yeye hana nafasiyoyote ya uongozi ndani ya chama hicho.Itafakari Tanzania yenyerasilimali lukuki; gesi, almasi, mafuta, dhahabu, wanyama pori nk ikiwa chiniya Rais asiyeshirikisha wenzie katika maamuzi hivyo kuendesha nchi kwa maono namawazo yake pekee. Rais asiye na udhibiti wa familia yake kiasi cha "mkewe"kuingilia watendaji na utendaji wa shughuli za umma huku Rais akiwa hana kauli.Je tutasalimika kweli RESOURCES COURSE chini ya Dr Slaa? Jibu langu HAPANA.
mwakidondo: Nasikitika kusema kuwa uliyoyandika hapa kwa mtu mwenye busara zilizokamilika kama anafanya masahihisho atakupatia sifuri tena yenye masikio. Kwa nini nasema hivyo! Kwanza kati ya yote uliyorundika hapa na kufanya watu washindwe kutafakari mada za msingi, napenda nijadili tu hapo kwenye RED.
1. Napata tabu kuoanisha sifa hiziza kitaaluma za Dr Slaa na changamoto zinazoikabili nchi yetu: Kwanza kumbuka kuwa DR kule Kanisani alikuwa akitawala watu kama hawa Rais wetu waq sasa anaowatawala. Na zaidi ni kuwa TAALUMA na HEKIMA ni vitu viwili tofauti. Unaweza kuwa na taaluma lakini ukshindwa kutawala watu wako (Rejea maandiko- Musa aliweza kuwaongoza wana wa Israel kwa HEKIMA kwa sababu alikuwa akimsikiliza MUNGU w2ake) Viongozi wetu hawa hawasikilizi wala hawaoni.

2.Kweli ni msomi na ana uzoefu wakiuongozi lakini si katika jamii pana bali katika shughuli za kanisa: (SIO KATIKA JAMII?! Jamii ipi tena zaidi ya hii tuishimo? Hapa ndipo unapoonesha umbumbumbu wako! Hivi hujui kuwa Makanisani na Misikitini ndiko kwenye jamii kubwa na yenye maono kuliko wale wasiokuwa na dini? Na Je, wajua kuwa uongozi nao watoka kwa Mungu.

3. lakini ni vemakuwa na Rais mwenye taaluma sahihi kwa maendeleo ya jamii nzima: Huyu tuliyenaye sasa ana taaluma gani sahihi na kwa maendeleo yapi? Ni ujinga kujisifu mbele za watu kuwa unajua kuvaa suti vizuri wakati wanao ------ yakiwa wazi! Hivi ndivyo anavyotufanyia Rais wetu kuonesha umma wa nje kuwa ameijenga nchi kwa kupaka rangi nyeusi ardhini (IKIITWA LAMI wakati inatifuka baada ya mwezi) huku jamiinzima ikilia njaa na mfumko wa bei. Huu ni usomi gani?
4. si kundi mojalinalofungamana na imani yake tu: Kama ni suala la makundi kufungamana na yanayoegemea upande wa utawala uliopo, hebu tutajie tangu enzi za utawala wa Mwl. Nyerere hadi sasa ni wakati gani na kundi lipi ambalo limekuwa klikitumia mwanya wa utawala uliopo kufanya mambo ya hovyo?

Yapo mengi sana ya kujadili kwa hii mada yako ila ngoja niwaachie wenzangu waendeleze.

 
Mi nafikiri tuache kujadili hoja hewa hili sio jukwaa la umbea wala la akina Shekh yahya. Tujadili vitu concrete tutaokoa mda wa kujadili masuala badala ya hearsay. CCM wameeshawashika wengi humu mtajadili mpaka bila mwisho na kila mtu atakuwa mbaya humu JF. Na dalili zimeshaanza kuonekana kwani hamna kuamianiana kila mtu mamluki. Tuachane na woga kiasi hiki tutaogopa mpaka vivuli vyetu. CDM sio wajinga kiasi hicho wala Dr. Slaa mpaka waruhusu Josephine kugombea Jimbo ambalo tayari ni mtaji wa chama, huo ni umbea na mbinu za magamba za kuwaondoa kwenye hoja za umeme, maji, EPA, Rich monduli, barabara na mengine mengi. Hatuwezi kupoteza mda kujadili nani anagombea wapi kwa sasa issue ni nini kifanyike wapi watu wapate unafuu wa maisha. Hizi ni hoja za kitoto mpaka kina Nepi huko waliko wanawacheka kwamba mmeingia kwenye mtego wa kitoto. Ifike Kipindi tuseme Hatudanganyiki na hoja za kitoto.
 
Kuna msemo wa kiswahili usemwao lisemwalo lipo na kama halipo laja ili sipendi lije kwa sababu halina tija kwa wapenda mabadiliko.

Ni wazi CCM sasa inatumia kila aina ya Propaganda ili kuhakikisha Taswira ya CHADEMA inaharibika katika umma au kuwagombanisha wenyewe kwa wenyewe kama inavyofanyika kwa Zitto Kabwe.

Kuna tetesi sasa hivi zimeenea kwamba Josephine anapiga jalamba kugombea Ubunge wa Kawe, kama tetesi hizi ni za kweli na zisipokanushawa basi moja kwa moja Dr Slaa hana sifa za kugombea Urais kwa kushindwa kuisimamia nyumba yake na kushindwa kumdhibiti Josephine katika harakati hizi haramu za kisiasa.

Ila nisiseme mengi kwa sababu hizi ni tetesi nawakaribisha wote waliozipata tetesi hizi ukweli wake ni upi? na kama si kweli ni kwa Josephine asiitishe Press Conference kukanusha hili officially? ni kichaa peke yake ndani ya CHADEMA anayeweza kugombea na Halima Mdee kura za maoni 2015 ili kufanya Halima Mdee asigombee tena.

Nakala kwa Molemo
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.
 
nyie CHADEMA WEHU KWELI KWELI MNAKALILISHANA MISTARI YA BIBLE KUHARARISHA HARAMU...HUU NI UPUUZI.
 
Mie binafsi ni mkazi wa Kawe hakuna ubaya wowote Josephine, kugombea ubunge Kawe kama mwanachama wa Chadema ni haki yake ya kikatiba.

Msitake kubaka demokrasia Halima Mdee hana hati miliki ya jimbo la Kawe.
Hivi nyie magamba mtamnadi lini yule msichana wenu wa kazi Magufuli?
 
ANGALIZO KWA DR SLAA NA LOWASA
Kabla sijaanza kuelezea lolote napenda kumukumbusha Slaa ambaye ana taalum ya upadri.
Katika kitabu cha matendo ya Mitume kuna ushahidi kwa Sauli alikuwa muuaji na tena alikuwa anauwa mitume lakini alipata padiliko la kweli na kujiunga na mitume wengine.

Wakati Sauli anafanya hivyo Mitume wengine walianza kumunyanyapaa na kumuogopa lakini katika bibilia , imethibitishwa kwamba hadi leo Paulo (aliyekuwa Sauli) ndiye aliyefanya kazi kuliko Mitume wote.

Bila shaka kuna watu ndani ya Chadema na hata nje ya chadema wanataka kujenga hoja ya kumunyanyapa LOWASA ati ni Fisadi , hata mimi niliingia mtego huu lakini napenda kuhojhi yafuatayo:
(1)Lowasa amehama CCM na kwa hatua hiyo ameingamiza nafsi yake kwa kiwango Kikubwa.
(2)Lowasa yupo tayari kutumia Pesa yake na mali yake kubomoa CCM
(3)LOWASA anahasira kali na CCM na miungu watu ndani ya CCM
(4)LOWASA kama waziri Mkuu mstafu ametake risk ya Kifo kiasi kwamba anataka kupiga CCM kwa Nyaraka zito za Siri ambazo Slaa hawezi kuzielezea
(5) Lowasa anajua mikakati ya Wizi wa Kura ndani ya CCM kwa miakazaidi ya 40
(6) Ndani ya CCM hawakutarajia wala hawakuwahi kupanga kuwa mtu kama Lowasa ambaye amewshijka nafasi nyeti kama waziri mkuu anaweza kuasi serikali kiasi hiki
Huu uasi unatisha na haujawahi kutokea, na hata pale ulipojaribu kutokea wahusika hawakubaki hai
(7)Kwa sasa CCM wanahaha sana juu ya Lowasa kuchukua form. Mikakati ya CCM iliielekeza Nguvu kumshambulia Slaa lakini Mungu amebadili Plan ghafla na kumuleta Lowasa amabaye hawajajipanga nan i Pigo kubwa
(8)Kwa sasa Uasi uliojitokeza CCM ni vigumu kujua nani yupo kwa nani
Angalia mtandao wa Lowasa ndani ya CCM unatisha na umetulia Kimia.
Mtandao huu jumlisha nguvu ya Umma ni lazima CCM ibaki kama KANU
MAONI KWA SLAA.
(1)Wakati unagombea urais ulikuwa na Rozi Kamili ukamwacha na kumuoa Josephine
Rozi Kamili alikubali ujio wa Josephine lakini leo Josephine huyo amekuwa kikwazo kwa maamuzi yako.
(2)Mambo ya Chama huwezi kumuhusisha Mwanamke, huo ni udhaifu mkubwa na kama kweli unamsikiliza mwanamke basi ujue hutapata nafsi ya kurudi kwenye jamii na wakakuamini na kukupa heshima kama walivyokupa.
Mke ni mshauri wake kwa mambo yote lakini kikao kama kamati kuu kinapopitisha maamuzi harafu mkeo anapinga maana yake mke huyo hafai kuwa First Lady na hata wewe hufai kuwa Kiongozi
MAONI KWA LOWASA
(1)Umeitwa Mwizi kwa siku nyingi sana na hata mimi nimekuita hivyo , sasa huu ni wakati wa wewe kutuambia mwizi halisi ni nani na utoe Ushahidi
(2) Zipo taarifa kwamba CCM wanapanga kukata jina lako kwenyenye tume ya uchaguzi hivyo nakusihii usikate tama .Muombe Mungu .Hii ni safari ya ushindi na si matumaini tena
(3)Usiogope kushambulia Ikulu kwa kuwa Mussa alikaa Ikulu ya Farao na kulelewa hapo lakini Mungu alimupa kazi ya kumuangamiza Farao.
Hivyo Lowasa umepewa kazi ya Kuingamiza CCM hivyo fanya kweli ujue kwamba Slaa hajui haya.

​Looks like I can sniff the MAN behind this mask!
 
Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho!"MM
 
kwani ubunge ni uflume hadi mtu aongopwe kupingwa kisa aendelee na ubunge au democracy haba nn, mama wa watu anahaki yakufanya ivo kabisa
 
Back
Top Bottom