Onyo kwa CHADEMA na angalizo kwa Dr. Slaa - We are watching you!

....kwa Josephine asiitishe Press Conference kukanusha hili officially?....

Awe Dr. Slaa au Josephine kitendo cha kufanya Press litakuwa ni kosa la pili la kiufundi na la ki-kimkakati kufanywa na CDM katika kipindi cha hivi karibuni. Kwa kufanya hivyo; wale wapenzi wa Football tunasema CDM watakuwa wameanza rasmi kucheza “Defense” wakati wao ndiyo walikuwa wanaongoza game kwa mashambulizi. Kwa wapenda Disco hatua hiyo naweza kuilinganisha na Dj kuamua kuwa Dancer! Huko ni kuthibitisha kuporomoka.

Lisilo na damage ni Mh. Mdee mwenyewe kuikandia hii tetesi.

Hata kichaa wakati Fulani ana akili. Kwenye hili Nape na ccm wametumia akili.
 
Ni vyema hizi habari zikakanushwa humu. Kama watuhumiwa wataamini kuwa hizi ni habari za mitandao tu na kwamba hadi jambo liandikwe magazetini ndipo liaminike, basi kuna mengi sana ya kuyarudia ili kuyafanyia kazi humu maana ni habari za mitandao tu
 
Ni mchezo upi huo haswa wa kipuuzi? kwanini mnajenga hoja hafifu kama hizi kwa kuficha sura zenu kwa majina ya pompo na picha za celebrities? Kama mnatete nchi bila uwoga, ni muhimu mkjajitambulisha, sio kujificha ficha; Mimi sina uwoga, na sijali kwani naangalia kwanza taifa langu, kuna wakati naichukiza CCM na wananisema na kunitisha mengi, na kuna wakati naisema vilivyo Chadema na napigwa makombora, lakini yote ni kwa kuweka taifa langu kwanza mbele, au kuwa objective kwa hoja;

Katika hili, kama ulitumia muda kunisoma vizuri, nilichosema ni kwamba iwapo tetesi kwamba Dr. Slaa na kadi ni za kweli, basi hili ni tatizo,..iwapo tetesi kwamba suala la Josephine Kugombea Kawe ni za kweli, hili ni tatizo...., na linaweza kuharibu image ya Dr. Slaa kuelekea 2015; Sasa nini cha kipuuzi hapo, inachotakiwa ni kuthibitisha kwamba tetesi hizi hazina ukweli wowote, basi, tusonge mbele kwenye masuala mengine ya kujenga taifa;

Kuna umuhimu wa kuweka ushabiki wa vyama pembeni kwanza na kulivaa suala husika objectively, kwani kwa kufanya hivyo, utarudi kwenye imani yako ya chama ukiwa na kitu cha uhakika kichwani, na utajenga hoja, na watu watasema naam; lakini kuvamia kila hoja kwa kope za vyama (subjectively), bila kutoa fursa ya objectivity, hakuna mjadala wa maana utakaoendelea; Mbona wenzenu wengine wanaelewa hoja kama zangu na tunabadilisha maneno vizuri tu, hasa pale wanapohimiza kwamba hili suala ni tetesi, halina ukweli wowote......

TAFDHALI FAFANUA HII PHRASE YAKO:.iwapo tetesi kwamba suala la Josephine Kugombea Kawe ni za kweli, hili ni tatizo...., na linaweza kuharibu image ya Dr. Slaa kuelekea 2015;

UKIWEZA BASI TAFADHALI ONESHA WAZIWAZI KWAMBA TATIZO LENYEWE NI LIPI? SISI WENGINE HATULIONI NDIO MAANA TUNAHITAJI UTUELEWESHE NDIPO TUCHANGIE MADA YAKO HIYO.
 
Du!
Kweli boli la kisiasa sasa linachezewa karibu na goli la CDM.
Mafowadi wote wamerudi nyuma na CCM inafanya mashambulizi ya kushtukiza.
Dr Slaa kesha jichokea na hana tena stamina ya kujibu mashabulizi sasa hivi ulimi nje!
Mmemchezesha staa wenu sasa magoti gongana.
Dakika 90 mwisho ni 2015, na jamaa wa CCM ndo kwanza wanatroti!
 
Kwanini Josephine asije kujibu humu hata kwa mistari 2 tujue ukweli? Haya maswala ndio tulikuwa tunamponda Zitto kwann hajibu tuhuma dhidi yake na badae kijana akabadilika,
Josephine njoo hujibu hapa kama zamani ulivyokuwa active.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Matola

Asante sana kwa nakala.

Nieleze kidogo kwamba habari hii ilianza kutolewa na gazeti la HOJA
ambalo linamilikiwa na Kada wa CCM aliyewahi kuwa Meya wa DSM.Gazeti
hili limekuwa likiandika habari za kukashifu kila wiki chama cha
Chadema.Anayetaka kuamini kesho Ijumaa litatoka na habari nyingine ya
kashfa za uongo na za hovyo hovyo dhidi ya Chadema.

Wapo watu hawalali wanataka kutumia kila njia kugombanisha
wapiganaji.Wanadhani kwa vile Josephine anaishi jimboni Kawe basi njia
rahisi ya kugombanisha wanachadema ni kusema Josephine anataka kugombea
Kawe.Huu ni ujinga na upuuzi wa hali ya juu.

Hata hivyo si vibaya Josephine akajitokeza kukanusha hili ingawa naamini
viongozi wa Chadema watazushiwa mengi na makubwa zaidi kwa siku
zijazo.Sasa najiuliza watakanusha mangapi? Kwa sababu kazi ya viongozi
wa Chadema itabaki ni kukanusha tu.Kwa mfano kuna gazeti la CCM
liliandika Freeman Mbowe anataka kumfukuza Dr Slaa Ukatibu Mkuu sasa Je
Mbowe naye ajitokeze kukanusha hamfukuzi Dr Slaa?

Makamanda wakati mwingine msitishwe na Propaganda.Hizo zipo sana tu na
zitaendelea kuja kwa hali msiyoamini..

Molemo...

maskini CDM wamekuwa watu wa kukanusha tu, itafika wakati watu wataona aibu kujiita wanaCDM
 
Katika hili, kama ulitumia muda kunisoma vizuri, nilichosema ni kwamba iwapo tetesi kwamba Dr. Slaa na kadi ni za kweli, basi hili ni tatizo,..iwapo tetesi kwamba suala la Josephine Kugombea Kawe ni za kweli, hili ni tatizo...., na linaweza kuharibu image ya Dr. Slaa kuelekea 2015; Sasa nini cha kipuuzi hapo, inachotakiwa ni kuthibitisha kwamba tetesi hizi hazina ukweli wowote, basi, tusonge mbele kwenye masuala mengine ya kujenga taifa;

Mkuu Mchambuzi nadhani hoja inakuwa na mashiko baada ya kujiridhisha mantiki na source yake. Taarifa za tetesi hizi zimetoka wapi? na ni akina nani wanazisambaza hasa? Unajua sometime ukishajua na kupima mantiki na source ya tetesi zaidi impact yake ni busara kukaa kimya tu na kuendelea na mambo ya msingi.

Unachofanya hapa ni kutaka kuuaminisha umma kwamba credibility na popularity ya Dkt. Slaa itaporomoka kuelekea mwaka 2015 kutokana na tetesi (propaganda) hizi. Tunasahau mwaka 2010 CCM hawahawa walizunguka nchi nzima kumtangaza Dkt. Slaa ni mzinzi, mwizi wa wake za watu hadi kufikia hatua ya kumpa mamilioni mtalaka wa Josephine Bw. Mahimbo ili amfungulie kesi Dkt. Slaa? Ni kwa kiwango gani Dkt. Salaa aliporomoka kisiasa? Ina maana kweli leo tumesahanu siasa taka za CCM? Ni lini wametangaza kuziacha? Leo tunashindwa kuzitambua?
 
Last edited by a moderator:
Hivi Chadema hakuna anaefaa kuwa Katibu Mkuu zaidi ya Slaa? mbona kuna vijana hodari na wachapakazi wenye maadili kama Zito Kabwe?
Chadema kinahusishwa na udini na ukanda! Slaa ni Padre na mlei wa Kanisa aliesaini mkataba wa KIFISADI wa MOU 1992 akiwakilisha Kanisa na Edwad Lowasa kama Waziri ktk Serikali ya awamu ya Pili!

kama mnataka kufuta hisia za kidini Chadema hamna budi kumsimamisha Mgombea urais mwingine mwenye sifa za uongozi na asie na kashfa za kifisadi, kimaadili au za kidini!
Slaa ni msalaba wenu na mkiendelea kumlea na kumuenzi, basi mjue Chadema itafia mikononi mwake!

Asiejua kifo aangalie kaburi! NCCR iko wapi?

Kuna ujinga unaoendelea aidha kwa kufanya makusudi au wengine kwa kutokuwa na uelewa wa kutosha.udini wa Slaa upo kwenye urais na si ubunge?Huko kwenye ubunge udini ni halali lakini urais ni haramu.Wapo watanzania wengi sana wasio jua elimu ya kanisa katoliki na uendeshaji wa mambo yake.Ni kosa kubwa kumwita mtu padre wakati alisharuhusiwa kwa mujibu wa sheria za kanisa katoliki kuacha huduma ya upadre.Mimi niliyepitia huko najua Slaa kwa sasa si padre.
Anayeondoa upadre wa mtu yeyote aliyewahi kuwa padre ni Papa pekee.Ndio maana padre akiomba kwa askofu wako kuwa hana tena wito huo Askofu anachofanya ni kuitaarifu Vatican kwa ushahidi wa padre mwenyewe na Baba Mtakatifu akijiridhisha,anatoa kibali rasmi cha kuacha kwake upadre. Nina hakika wengi wenu hamjui sheria za kanisa katoliki na hivyo kusema mambo ya kusikia tu.
Hoja ya kutafuta katibu mkuu mwingine,hapa tatizo ni nini hadi wengine mtake aondoke madarakani?Najifunza jambo hapa,aidha uwepo wake katika cheo hicho unawapa tatizo wengine au mnataka mtu mtakaye weza kumrubuni ili chadema iparaganyike. Utendaji kazi wake unawapa tabu nyie.
Nijuavyo pia cheo hicho hakujipachika.Kama anafanya madudu basi wahusika wangemwondoa.
Mwisho napata hasira sana ninapoona watu wanachanganya sana "udini" wa Slaa kama "padre wa zamani" na kugombea urais. Hivi sasa hata kina Nape wanapenda sana Slaa aondolewe katika madaraka yake.Hapa kuna agenda imejificha.Kawakosea nini Slaa?Mbona hamsemi Naibu Katibu Mkuu au Mwenyekiti wake aondolewe?Kila siku Slaa, Slaa.Mnaboa sana.Kuna agenda gani?
 
Katika hali ya kawaida wewe ni kibaraka wa magamba,au huyu boc anaetaka upresda..nakushauri wewe si mshauri wa cdm,hivyo huna right ya kusema chochote kuhusu cdm,hatuitaji mavuvuzela tunajua yanakopatikana.sec nakuonya cheza na vitu vyote lakiani si hisia za mtu..
Vipi ratiba ikoje mnaenda tena kujitambulisha nec mpya wapi%&?shame on you.
Huna tofauti na maiti.

Umesema vema lakini huu ulioandika ni unafiki mtupu!
Mafarisayo upati tabu kuwatambuwa.

Tuliwaambia wakina Nicholous na Jmushi waachane na CDM wakabisha, hii thread sikutegemea itoke kwa Matola
Usidhani mimi ni Zezeta kama wewe, ninahoji na kudadisi, na kwa taarifa yako mimi si mwanachama wa Chadema, kuipinga CCM haku justifies kuwa mtu ni Chadema, upo gizani sana, hii vita badly hamumjui adui yenu CCM, nakutambulisha kuanzia leo adui yenu mkuu ni umma wa Watanzania na tunawashambulia kutoka kila upande.

Ni vyema hizi habari zikakanushwa humu. Kama watuhumiwa wataamini kuwa hizi ni habari za mitandao tu na kwamba hadi jambo liandikwe magazetini ndipo liaminike, basi kuna mengi sana ya kuyarudia ili kuyafanyia kazi humu maana ni habari za mitandao tu
Umenena vyema Mkuu, leo John Mnyika alikuwa humu kukanusha Propaganda za kijinga dhidi yake, napinga kabisa Dr Slaa kujibu Propaganda za Nape lakini jambo kama hili linapaswa na liko ndani ya uwezo wa Josephine kulitolea maelezo.
Du!
Kweli boli la kisiasa sasa linachezewa karibu na goli la CDM.
Mafowadi wote wamerudi nyuma na CCM inafanya mashambulizi ya kushtukiza.
Dr Slaa kesha jichokea na hana tena stamina ya kujibu mashabulizi sasa hivi ulimi nje!
Mmemchezesha staa wenu sasa magoti gongana.
Dakika 90 mwisho ni 2015, na jamaa wa CCM ndo kwanza wanatroti!
Wewe si wa viwango vyangu hukustahili hata nilivyokuquote hapa, this is not Comedy young boy.
Mkuu Mchambuzi nadhani hoja inakuwa na mashiko baada ya kujiridhisha mantiki na source yake. Taarifa za tetesi hizi zimetoka wapi? na ni akina nani wanazisambaza hasa? Unajua sometime ukishajua na kupima mantiki na source ya tetesi zaidi impact yake ni busara kukaa kimya tu na kuendelea na mambo ya msingi.

Unachofanya hapa ni kutaka kuuaminisha umma kwamba credibility na popularity ya Dkt. Slaa itaporomoka kuelekea mwaka 2015 kutokana na tetesi (propaganda) hizi. Tunasahau mwaka 2010 CCM hawahawa walizunguka nchi nzima kumtangaza Dkt. Slaa ni mzinzi, mwizi wa wake za watu hadi kufikia hatua ya kumpa mamilioni mtalaka wa Josephine Bw. Mahimbo ili amfungulie kesi Dkt. Slaa? Ni kwa kiwango gani Dkt. Salaa aliporomoka kisiasa? Ina maana kweli leo tumesahanu siasa taka za CCM? Ni lini wametangaza kuziacha? Leo tunashindwa kuzitambua?
Kama unashindwa kuona tatizo alilolileta Museven Uganda basi wewe utakuwa kipofu kabisa, Museven alijaza familia yake kwenye uongozi na mke wake akmpa uwaziri pia,tunapopinga siasa za BMW kwa Familia ya Kikwete si kama tunamuonea hatutaki nchi yetu igeuzwe ya kisultani.

Hainingii akilini Wabunge wanaowakilisha Chadema vyema bungeni wasipewe fursa na chama kugombea tena kwenye majimbo yao, tunapohubiri Demokrasia haimaanishi kwamba kila uchaguzi ni lazima watu washindanishwe wakati aliyepo anafaa na anafanya vyema. jiulizeni kwanza nchi kama Ujerumani ambayo imeendelea na wana Demokrasia pana je Angel Merkel huu ni mwaka wa kumi na ngapi anakiongoza chama chake?
 
Josephine ni chaguo la uongozi CDM HQ wakati wana Kawe tunataka utashi 2015 ni mgombea yeyote toka chama imara - CCM
 
Kwanini inachukua mda Josephina kukanusha habari hizi???????

Kwanini unataka akanushe? Hupendi kuona Josephine anatekeleza haki yake ya kikatiba? Mnatamani kuendeleza mfumo wa kimagamba wa kumiliki jimbo na kupitwa bila kupingwa? Kwanini mnakuwa waoga wa demokrasia? Kama kuna hoja zenye mashiko kwanini Josephine asipambane na Mdee ziwekwe wazi na sio hoja nyepesi kama hizo. Mbona first lady Hilary aligombea na Barrack huku mumewe Bill akiwa na influence kubwa kwenye chama na mambo yalienda?
 
mkuu hebu tueleze kikao kilifanyika wapi na nani walihudhuria ili josephine atangaze nia yake ya kugombea .na hili suala wewe unalichukuliaje maoni yako
 
Dr. Slaa atawanyima usingizi zaidi na zaidi. hizo personal attacks watanzania wameshazizoea na wanazidharau, kizuri zaidi ndiyo mnazidi kumpaisha juu katika medani za kisiasa.

Angalia mtu anasimama na kusema:-
1. CDM ina kiongozi mmoja tu --- naye ni DR. Slaa so msiwape nchi wataiuza
2. DR. Slaa ana kadi ya CCM

Sasa kwa kuona hizi mpya hazifui dafu mmekuja na hii ya Josephine kugombea kawe - kila siku mnaambiwa watanzania mliozoea kuwageuza kama chapati sasa wamejanjaruka..

Jitahidini kupunguza makali ya maisha kwa wananchi hasa wa hali ya chini si eti kuibuka na hoja za DR. Slaa kafanya hiki na kile - mnaonekana hamjui mnalolifanya na muda ndiyo huo unayoyoma kuelekea 2015.

Ushauri wa bure:

Waambieni mabosi wenu wa CCM - watekeleze ilani ya uchaguzi ya CDM ya 2010 kama mlivyoanza itasaidia kiasi kurudisha imani kwa wanananchi, kuzurura na mawaziri mikoani bila chochote kufanyika ni kuwaudhi wananchi zaidi. ni sawa na kumwona mwizi wako wa msosi live wakati ukiwa na njaa kali tumboni fikiri nini kitatokea hapo.
 
Chadema ni chama mufilisi kipo ICU shuhuda ni Dr Fr Slaa alipokuwa M4D mkoani DSM
 
Josephine ni chaguo la uongozi CDM HQ wakati wana Kawe tunataka utashi 2015 ni mgombea yeyote toka chama imara - CCM
 
Mkuu Nicas heading ya thread ni tetesi, na nimeziona zinasambaa kwa nguvu kwenye social media, ndio maana nikasema ni vizuri hizi habari kama si za kweli zikanushwe mara moja. sipendi ninapoona jina la Josephine likihusishwa sana na mambo ya Chadema hii inaharibu Image ya Chadema na tunavyomthamini Dr Slaa.
Huna taarifa kuwa magamba wamebadilisha sekretarieti yao!
 
Back
Top Bottom