Onyesha Upendo kwa Vitendo

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,462


love.jpg

Hi


wanajamvi wenzangu natumai mko fiti na mnaendelea
na majukumu kwa wale walioko job, wafanyabiashara na
wasomi pia ilakwa wale ambao wanajipumzisha kila lakheri

Weekend hii nimefurahi sana kuwaambia kitu ambacho ni
muhimu sana hasa katika mahusiano yetu yawe ya mmoja,
urafiki, undugu, ujamaa, ujirani na hata mahusiano ya
kwenye Ndoa. Jambo la muhimu kwenye mahusiano ni
hili la kuzingatia kuwa na Upendo wa dhati na sio wa
unafiki kwa yule umpendaye hasa hasa. Huna budi kuonesha
kuwa umekubalika kwake na kuwa mmojawapo katika nafasi
yake na vilevile huna budi kuonesha Upendo wa vitendo kwa
huyo umpendaye au uwapendao ili kudumisha hisia, penzi, na
undugu wa kweli kati yetu.


Zipo baadhi tu za dokezo ambazo zaweza kuwa sababisho la
wewe kufanya yule umpendaye awe mume, mwenzi, au rafiki
yako wa karibu kuvutiwa nawe na kuona kuwa wewe unamjali

Dondoo za Upendo wa agape:-

a) Huna budi kuwa nae karibu huku ukimpa maneno yenye
nyama ya ulimi usiokuwa na mfupa yaani kumbembeleza
kwa laini na yenye mvuto huku ukimwambia kuwa
unampenda hata kama amekukosea au pale unapoona
kuwa yu mashakani au ameumizwa uko alikotoka/ au
kapatwa na jambo la huzuni au furaha wewe onesha
uko pamoja nae.

b) Kuonesha kwa hisia za karibu sana tena kwa vitendo
kwa yule umpendaye japo kumnunulia kazawadi kawe
kakubwa au kadogo kutokana na jinsi mfuko wako wa
wa fedha kile kidogo ulichonacho kitamfanya aone kuwa
unajali na kumthamini vile yeye alivyo.

c) Onesha kujali pale ambapo anataka kuongea au kusema
na wewe na onesha kuwa uko pamoja nae katika yale
ayaongeayo yawe ni mambo yahusuyo maisha au ninyi
kazi, masomo, na hata biashara pia wewe kuwa msikivu

d) Jali na penda ndugu au familia yake au jali wale ambao
huko katika familia yako kwa ujumla, na hata marafiki zako
onesha kuwa uko pamoja nao katika furaha na huzuni hata
katika mambo mazito na magumu wewe kuwa mfumbuzi wa
hayo matatizo yaliyowapata wenzako wengine.

e) Jiheshimu na waheshimu marafiki, ndugu , jamaa, jirani hata
huyo uliyenaye kwani unapowaheshimu na kujiheshimu wa
leta kupendwa zaidi na hao wakuzungukao. na unaleta
amani, furaha kwao.

f) Kuwa mtu mwenye kudadisi na kubuni jambo ambalo wengine
hasa marafiki zakio watalipenda na kukupa support kwa jambo
hilo kwakufanya hivyo utajiletea na kujiongezea marafiki wengi
na wengi watakuita bora.

g) Kuwa mtu mwenye uchangamfu na mpole kwa kiasi na usipende
makuu hata kama uwezo wako ni mdogo ishi vile ulivyo na sio
kuiga wengine walivyo. Ukifanya hivyo utajiongezea kupendwa
na wale ndugu, jirani hata mwenzi wako naye atafurahi kuona
kuwa niliyenaye si mtu anayependa makuu na mwenye kujitukuza

TAMATI:
wapendwa wangu marafiki zangu napenda kuwashauri kuwa uwe
mtu mwenye mfano wa kuigwa na wengine kwa kuonesha upendo
usio na unafiki wala choyo kwani utakapokuwa hivyo utajijengea
heshima, kupendwa, na hata kuwa na marafiki wengi na pale
utakapopita katika magumu hao marafiki zako au ndugu zako
watakufaa zaidi.

Sitamsahau laaziz wangu Mentor anayenipa usingizi mwororo na
kunifanya niwe kila wakati nikimuwaza yeye kwa kumSURPRISE
namna hii kwa kazawadi kadogo haka hapa pokea bestito
orange.jpg

Mwisho kabisa acha niseme kuwa nawapenda marafiki zangu na
pokeeni zawadi hii ya upendo wangu kwangu ilove u.jpg


Copy: Mentor, Mtambuzi, Paloma, charminglady, watu8, Erickb52
Mr Rocky, Madame B, Chimbuvu, Baba V, Nicas Mtei, stevoh,
Jiwe Linaloishi, mpenda Yesu, Mzizi mkavu, Mamndenyi, Smile,
sweetlady, Ruttashobolwa, Excellent, Arushaone, Filipo,
marejesho, AshaDii, KakaKiiza, steven L. Masaku, gfsonwin,
amu, Asprin, Passion Lady, Lady, Preta, @FP, Kongosho,
fetty, mathematics, Dio, nitonye Catherine Denzi, na marafiki
zangu wote ambao kwa namna moja ama nyingine nimewasahau pokeeni.

Nawatakia Weekend njema yenye utulivu na upendo wa agape kwenu wote
 
Last edited by a moderator:
At last someone is not talking about love and sex!
Asante kwa kutujuza. Wengi wetu hatuna people's skills. Ndo maana tunashindwa kuishi na ndugu zetu na hata ndugu wa wenza wetu.

Kama kitu unachotaka kusema sio cha kistaarabu (kind. ), bora usikiseme kabisa (unless ni jf hehehe, hapa tu ndo unaweza kum-blast mtu). Huhitaji kuongea kila kinachopita kwenye kichwa chako.
 
umenichekkeshaje best yani mpaka mbavu zangu zimekauka we acha tu
wengine majangili ukileta za kuleta wanakupelekesha dawa jino kwa jino ukucha kwa ukucha tu
na ukiwa wa :A S 20: utaipata freshi utakondeana kama mtu mwenye HIV wa zamani
 
asante sn ila sijakuelewa best hiyo paragraph ya mwisho hebu nifafanule kidogo
At last someone is not talking about love and sex!
Asante kwa kutujuza. Wengi wetu hatuna people's skills. Ndo maana tunashindwa kuishi na ndugu zetu na hata ndugu wa wenza wetu.

Kama kitu unachotaka kusema sio cha kistaarabu (kind. ), bora usikiseme kabisa (unless ni jf hehehe, hapa tu ndo unaweza kum-blast mtu). Huhitaji kuongea kila kinachopita kwenye kichwa chako.
 
jamani laaziz lini utasema kitu kizuri kwangu maana wewe kila siku unanipa huzuni na kunpa presha ya hali ya juu hivi ninavyoongea niko wodini kwa sababu yako natundikiwa drip double double halafu umeondoka hapa hospital unadai kwenda kuleta supu kumbe uko huko haya mm naendelea kukupenda mpaka milele endelea kunumiza tu
 
Back
Top Bottom