Ongezeko la wagonjwa wenye Vimelea vya Helicobacter Pylori nini Shida

Anhaaa, sasa napata connection. Kuna dogo mmoja kule Buzuruga, Mwanza aliniambia kuwa yeye alikua anasumbuliwa na vidonda vya tumbo akawa akila pilipili anaumia sana lakini baadae anakuwa poa. Akawa anazila kwa fujo tumbo likiuma kisha linatulia.
Baadae akanipa habari ile hali ya tumbo kujaa gesi, kuunguruma, kuharisha imeisha. Anakula maharage, dagaa na kila kitu. Kiufupi alipona.
Ni Kweli, matumizi ya pilipili yanamsulubu bacteria asizidishe uharibifu tumboni, hiyo Inaitwa, dawa ya moto ni moto.

Mimi niliambiwa dawa hiyo na Mhindi nikapuuza, baadae nikatumia kidogo kidogo, ilisaidia sana.

Bt hatua muhimu ya kwanza ni kuzingatia kula Kwa wakati na kuepuka vyakula vyenye gas kama maharage nk nk

Pia hasira na kutunza visasi, kiufupi stress ni chanzo kikuu Cha madonda.

Pilipili, Kwa kuanzia, usile pilipili kichaa, Utaharibu,

Anza na pilipili zile zenye harufu nzuri zinazopikiwa kwenye mboga.

Unajua kama huna pesa, halafu uwe na madonda yanayokuzuia kutumia maharage ni taabu kubwa.

Mungu atusaidie.
 
Mkuu rabbon kwema, nina vidonda vya tumbo pia hivi karibuni Kuna jamaa kanishauri nitumie pilipili hapa napo naona umetoa ushairi wa pilipili, nakumbuka kipindi cha nyuma wakati pia nilipokuwa na vidonda nilipojaribu mara kadhaa kutumia pilipili nilipatwa na kuendesha sana hilo unalionaje? Na pia pilipili zipo za Aina nyingi kwenye matumizi ni pilipili yoyote au ? Maswali ni mengi naomba nifahamishe hilo Asante
Soma pia comment no 40, Sean Paul, ameweka ushuhuda wa mhanga wa madonda aliyetumia pilipili, akatoboa.
 
Helicobacter Pylori ni bacteria ambao wanasadikika kusababisha vidonda vya tumbo na pia Kansa ya utumbo/tumbo, njia zake za kuambukizwa ni kupitia matumizi ya vitu vyenye vya H-Pylori kama vile maji au vyakula na pia kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Helicobacter Pylori ni kati ya bacteria ambao zamani hawakuwepo sana ila kwa sasa kati ya wagonjwa kumi wanaofika kwenye vituo vya afya na wenye dalili za kuumwa matumbo, tumbo kujaa gesi, uchovu, kichwa, kuharisha...nk wakipimwa kutumia kipimo cha choo wengi wanakutwa positive kwa huyu bacteria.

Achana na wale wanaotaka kuuza Heligo-kit ila kiuhalisia watu wengi sana wanaopata huduma kwenyevituo rasmi vya afya ni wahanga wa hawa bacteria.

Je shida kubwa ni nini, watu hawana elimu juu ya hawa bacteria au mazingira yetu yamekua machafu au usafi kwenye uandaaji wa vyakula vyetu sio mzuri.
Hiyo sample ya wagonjwa unaowasemea umeiotoa kwenye vituo Gani vya afya? Halmashaur,wilaya, mkoa ama kituoni kwako?
 
Helicobacter Pylori ni bacteria ambao wanasadikika kusababisha vidonda vya tumbo na pia Kansa ya utumbo/tumbo, njia zake za kuambukizwa ni kupitia matumizi ya vitu vyenye vya H-Pylori kama vile maji au vyakula na pia kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Helicobacter Pylori ni kati ya bacteria ambao zamani hawakuwepo sana ila kwa sasa kati ya wagonjwa kumi wanaofika kwenye vituo vya afya na wenye dalili za kuumwa matumbo, tumbo kujaa gesi, uchovu, kichwa, kuharisha...nk wakipimwa kutumia kipimo cha choo wengi wanakutwa positive kwa huyu bacteria.

Achana na wale wanaotaka kuuza Heligo-kit ila kiuhalisia watu wengi sana wanaopata huduma kwenyevituo rasmi vya afya ni wahanga wa hawa bacteria.

Je shida kubwa ni nini, watu hawana elimu juu ya hawa bacteria au mazingira yetu yamekua machafu au usafi kwenye uandaaji wa vyakula vyetu sio mzuri.
Punguzeni kula denda
 
Punguzeni kula denda
Hili pia tatizo.
Mimi sikuwahi kuwa na H Pylori kwa miaka zaidi ya 32. Nilipoanza mahusiano na mama mtoto wangu nikapata H pylori, katika kutafiti kwangu nikaona kula denda nako kunahusika. Yeye ana madonda yale akichelewa kula tu shida.

Nilivyogundua tu nina shida, nikachange life style. Mama mtoto najizuia sana kumla denda, kama hapa nna week 3 sijakutana naye, hayupo.
Madonda yalipona. Ukiniuliza nilipona na nini hata mimi sijui. I tried several remedies ile ikiisha hii naweka hii na kubadili life style. Sina tena shida.
 
Usishangae wingi wa wachina wanaoingia wanakuja na mbinu za kutupunguza, 100 years to come ninahofu huenda dominant race ikawa chinese arabs na indians
 
Hili pia tatizo.
Mimi sikuwahi kuwa na H Pylori kwa miaka zaidi ya 32. Nilipoanza mahusiano na mama mtoto wangu nikapata H pylori, katika kutafiti kwangu nikaona kula denda nako kunahusika. Yeye ana madonda yale akichelewa kula tu shida.

Nilivyogundua tu nina shida, nikachange life style. Mama mtoto najizuia sana kumla denda, kama hapa nna week 3 sijakutana naye, hayupo.
Madonda yalipona. Ukiniuliza nilipona na nini hata mimi sijui. I tried several remedies ile ikiisha hii naweka hii na kubadili life style. Sina tena shida.
Denda watu wanagawiana H Pylori vizuri kabisa.

Pamoja na wazama chumvini.

Vidonda vya tumbo dawa yake kubadili life style tu na mlo unaokula
 
Tuanzie hapa kwanza.

H. pylori Infection: Symptoms, Causes, Diagnosis, and Treatment

Medically Reviewed by Jabeen Begum, MD on September 27, 2023 Written by Susan Bernstein, Sarah Gleim
8 min read

Mbali na msaada wa ku google kuna kitu unachokijua kweli?
 
Ikiwa unatumia pilipili na Ina kudhuru, yaweza kuwa madonda uliyonayo yapo stage ya juu zaidi.

Pima ujue stage ya madonda Yako, Mimi niliambiwa kutumia pilipili na mhindi mmoja na sikuamini, nikaanza Polepole kutumia pilipili Ile yenye kupikiwa kwenye mboga yenye harufu nzuri, usitumie pilipili kichaa, na matumizi yawe pole pole.

Muhimu pia, hakikisha huvushi muda wa kula, asubuhi kula Kwa wakati, mchana kula Kwa wakati, na jioni pia.

Usile dagaa, tumia mboga za majani zaidi Hasa mlenda, Samaki nk nk.

Mimi nilikuwa na madonda ambapo nilikuwa nikivusha tu muda wa kula, napata shida sana.

Mimi ni mtumishi wa Mungu pia, Kwa kuwa nilikuwa na madonda, sikuweza KUFUNGA, niliepuka KUFUNGA.

Tangu nilipojiweka karibu zaidi na Mungu, na kupewa moyo wa kuachilia, kusamehe na kutoweka visasi moyoni, stress ziiniondoka ambazo ni chanzo kikuu Cha magonjwa ya tumbo.

Now naweza KUFUNGA bila shida yoyote, naweza kaa masaa zaidi ya 12 bila kula, hata Leo Jumamosi nimefunga na sipati shida yoyote,

Naweza kula maharage, dagaa, maziwa nk nk

Ninakuombea Mungu akuponye kama alivyonisaidia Mimi.

Ubarikiwe.
Rabbon, Asante Mungu akubariki vidonda vya tumbo ni miongoni mwa ugonjwa unaotesa sana ila hautiliwi maanani , Asante kwa ushauri wako mzuri nitaufanyia kazi maana vinatesa mno na kukatisha tamaa ya maisha
 
Attachments

  • IMG-20240125-WA0041.jpg
    IMG-20240125-WA0041.jpg
    299.1 KB · Views: 10
  • IMG20240120141012.jpg
    IMG20240120141012.jpg
    965.7 KB · Views: 13
Mimi nina connection na Marekani naagiza mara Kwa mara.

Hakuna Mmarekani anaweza kukwambia ana vidonda vya tumbo au kaambiwa asile pilau, dagaa au Maharage, huu ni ujinga upo Bongo/Africa.

Kama upo Dar pale Namanga Best bite kuna clinic inaitwa premier care Kwa Dr Pierre check kwenye pharmacy yao huwezi kukosa hizi anti acid tablets, ukitumia hizo huwezi kupatwa na vidonda vya tumbo na aliyepatwa atumie hizo anti acid atakula vyakula vyote na vinywaji vyote.
Mzee niaje naomba unicheki kwa namba hii 0744312003 au nitumie namba yako nkuulize kitu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Wenye H Pylori huwa wanaopewa triple therapy (Combination ya Omeprazole (20g),Amoxycilin ( 1g),na metronidazole 400g)
kwa siku 10-14 baada ya hapo wanaendelea na Omeprazole kwa wiki 6.

Ikifeli wanaingia kwenye tetracycline,metro ,Omeprazole na bismuth citrate.
Habari Hance.
Nikienda Pharmacy niseme nataka dawa gani.
Nianze kutaja hiyo list ya kwanza pamoja na hizo gram zake?

Yaani tuseme nataka nikanunue mwenyewe dawa nianze kumeza (sina cheti cha Maabara)

Nikienda pharmacy nisemeje, na amount (dozi) iwe ya kiasi gani
 
Back
Top Bottom