On Mtwara: Kikwete, Muhongo na Bunge - Mnayakumbuka haya?

Status
Not open for further replies.
Binafsi hiyo Ripoti ya juu kabisa ambayo inazungumzia suala la kujenga njia za umeme kutoka Mtwara hadi Singida sizani kama ni ripoti ambayo ilifanya utafiti wa kutosha kiuchumi!!

Hilo moja, lakini vile vile nazani wengi wetu hapa tunachukulia suala la Gesi kama raw material ya umeme peke yake, lakini gesi ni zaidi ya umeme! Kama tutaamua kutekeleza project ya hapo juu (kuzalisha umeme Mtwara) hapo manake Gas is just for electricity unless hapo baadae serikali iingie gharama zingine za kujenga njia kwa ajili ya matumizi ya gesi kama gesi! Unapojenga bomba la gesi kimsingi ni kwamba unaua ndege wawili kwa jiwe moja at the same time minimizing cost! HOW? Coz' the same transported gas itakuwa ni raw material for production of electricity baada kufikishwa kwenye processing plant and another portion for domestic and industrial use!

Economically, always goods zina-flow to places where there's higher demand, na ndio maana popote utakapoenda gas inakuwa transported to urban areas where there's higher demand and large number of consumers. So, tukichukua gas kama gas, haina enough consumers in Mtwara, and probably in many areas of Tanzania! Lakini Dar es salaam, demand hiyo ipo; not only for industrial but also for domestic use!

Hoja yangu hapa ni kwamba, hata kama tutalazimika kuifanya Mtwara ndiyo processing and production centre ya umeme kisha usambazwe sehemu zingine nchini, bado ulazima wa kujenga bomba utabaki pale pale endapo tunataka kuwa rational kwenye matumizi ya raslimali! Dar es salaam and other cities need gas for industrial and domestic use! So, suala la kujenga bomba is inevitable!

Vile vile kiuchumi huwezi kusema kwamba Gesi ikibaki pale pale kwavile ita-stimulate viwanda! Nasema huwezi kuweka hiyo hoja coz' suala la zima linahusu large investment! Huwezi kuwekeza Millions of Dollars kisha ndipo usubiri wateja watakaotumia gesi husika! Hicho kitu hakipo kwenye uchumi wowote duniani!

From economic point of view, Gas need to be transported to regions where's there's high demand and not otherwise! Na kwavile gas inayosafirishwa inakuwa imeshasafishwa, then sioni kama ndugu zangu wa Mtwara wana cha kupoteza. Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba ni lazima gesi isafishwe Mtwara na vile vile pawe na outlet pale Mtwara ili ukifika wakati wa Gas demand, iweze kutumika hata Mtwara.

Wana mtwara ni masikini sana,kama kutajengwa viwanda vya ku-process Gas wana Mtwara watapaka kazi watapata kipato cha kusaidia familia zao.

Kama ulivyoeleza Gasi kama gasi ina matumizi mingi,matumizi kuanzia umeme,matumizi ya nyumbani,inaweza kuwa bidhaa ya kusafirishwa na kuuza nje ya nchi kama petroli na kadhalika.

Kama Gas isafirishwe tu na kutolewa nje ya Mtwara na process zote kuanzia kuisafisha kuifanya gesi iwe katika hali ya kutumika,iwe katika hai ya bidhaa zifanywe nje ya Mtwara sioni kama wana Mtwara watafaidika na Gasi yao,Kama bandari ya kusafirishia gasi ijengwe bagamoyo na sio Mtwara sioni kama wana Mtwara watafaidika na Gasi yao,sioni kama wana Mtwara wataondokewa na umasikini unaowaandama

Mawazo yangu serikali ijenge viwanda vya kusafishia Gesi Mtwara,Iboreshe bandari Mtwara,Mambo ya kusafirisha Gesi yatafatia baadae lakini kwanza serikali ihakikishe kila kitu kinafanyika Mtwara gesi ikitoka Mtwara iwe imetoka kama bidhaa kamili.
 
Muda mwingine tunaweza kufikiri kuwakata watu mapembe kumbe mapembe ni sisi wenyewe na tumekuwa tukiyakuza na matokeo yake tumeyaona wazi.
 
Naona kila hatua mheshimiwa rais anatajwa kuhusika kuanzia kupokea ripot hadi uzinduzi. Na hii U turn ya Singida mpaka Dar kumbe zile tetesi za bagamoyo si za bure.
 
Sijaelewa ugumu wa serikali kuelewa nini wananchi wa Mtwara wanahitaji. Ndio maana inaonekana hakuna kutoka gesi coz Kuna sintofahamu nyingi kuanzia kwenye matamshi yao mpaka maoni mbalimbali yaliyotolewa bila kufanyiwa kazi ukweli.

Nadhani rahisi kabisa kusini ilisahauliwa kitambo na hivyo hakukuwa na tumaini lolote kwao sasa tumaini Lao ni gesi Kuna uzito gani kujenga mitambo ya kuzalishia gesi pale kama swala ni kuingia gharama marambili kusafirisha gesi na umeme swali je na Hizo 10% zilizofanya gharama ya kuweka bomba za gesi kuwa Mara tatu ya gharama halisi ni kwa faida ya nani kwanini haizingatiwi mahitaji ya wengi zaidi inaangaliwa faida za wachache hapo Ndipo naona Kuna utata yote tisa Kuna tabia ya kuona wengine hawajui chochote kuhusu gesi na manufaa yanayotakiwa kupatikana kutokana na maliasiri hii Kuna tabu gani kushirikisha wananchi kwa ukaribu ikiWaPo kuweka wazi mikataba na faida zake kwa mapana zaidi? Kwani Ile sera ya uwazi na ukweli iliishia wapi,?

Hivi sasa Kuna vipindi pekee ndivyo vinatumika kutoa elimu kuhusu maswala ya gesi mtwara lakini ni wananchi wangapi wanaweza kufuatilia vipindi hivyo vya tbc toka mtwara na vitongoji vyake naamini sio tuu watu wa hali ya chini kimaisha Kuna wengi hawafahamu nini serikali inafanya kuhusu gesi na Ndio maana upinzani unaonekana ni mkubwa sana pia lugha zinazotolewa na viongozi kuhusu utata huu hazijengi sana kama kusema KUNA WATU WAKO NYUMA YA MGOGORO WA GESI MTWARA SIO SAHIHI ni sawa na kusema wananchi wa mtwara wajinga hawajui kusema mpaka wafundishwe na wengine kudai kile wanachoona na kuamini ni haki Yao.

Kuna haja ya kuliona hili suala la gesi kama msaada wa kupunguza makali ya kiuchumi katika mikoa ya kusini badala ya kuliaangalia kibiashara zaidi kama wengine humu JF akina NasDaz na salaama nilivyoona michango Yao tukumbuke hizi ni project za serikali kwa niaba ya wananchi wote.
 
hakika siamini kama muhongo hakuwai kusoma hizi report au jk aliziweka tuu.
Ningependa kuona sentensi mbili za Nape Nnauye.
Kwani tunazungumzia kadi mbili za Dr Slaa? maana ninavyo jua mimi Nape kwenye mada kama hizi huwa hasogezi pua lakini kwenye mada za kadi mbili ataingia kwa ID zake zote 7 ili kujijibu na kujipongeza...
 
Alafu mama Hawa Ghasia alishawai zomewa kwenye mkutano wa hadhara huko huko Mtwara.

Sikutarajia hili kama mbunge kwako unazomewa sasa ukienda ugenini si unaweza pigwa bakora!
 
Unaweza kunitajia viwanda vikuu vitano vilivyopo Dar? By viwanda namaanisha viwanda hasa na siyo TBL.

Chifu, nilishiriki zoezi moja la kuangalia namna mradi wa SongoSongo - gas to electricity - umeweza kuwa na manufaa kwa viwanda vinavyotumia gesi na taifa kwa ujumla.

Kwa kweli kama viwanda hivyo nilivyoenda ndivyo serikali inavisemea, hakika sioni kwanini viwanda vya aina hiyo visijengwe Mtwara pale pale. Kwani katika viwanda vyote vinavyotumia gesi ya Songas, ni kiwanda cha Wazo Hill tu ndicho naweza kusema ni kikubwa na kinachotumia gesi zaidi.

Unavijua vingine? Ngoja nikutajie:
1. OK Plast Limited
2. Kioo Limited
3. TCC (TZ Cigarette Company)
4. ALAF Limited
5. Murzahi Soap and Detergents
6. Kamal Steel Limited
7. Bakhresa Food Products Limited
8. YUASA Battery (EA) Limited
9. Bora Industries Limited
10. TBL
11. Serengeti Breweries
12. Simba Steel
13. NIDA Textile
14. Urafiki Textile
15. Nampak (T) Limited
16. Silafrica (T) Limited
17. East Coast Oil and Fats Limited
18. Murzah Oil Mills Limited

Hivi ndivyo navyovikumbuka; lakini kama kuna nilivyovisahau, haviwezi kuzidi vitano.

Matumizi makubwa ya gesi katika viwanda hivyo ni kwa ajili ya boilers, metal preheating, glass melting na drying and dehumidification. Kwa maana nyingine, gesi haitumiwi katika shughuli kubwa za uzalishaji katika viwanda hivyo. Yaani gesi inachangia kwa asilimia ndogo sana (kama energy) katika uzalishaji kwenye viwanda hivyo. Ingawa ni ukweli ulio wazi kwamba, matumizi ya gesi katika processes hizo za uzalishaji, yamesaidia sana upunguzaji wa gharama za uzalishaji katika viwanda hivyo.
 
Mmakonde gani una tumbo kubwa hivyo?
Kumbe chamaki nchanga wana protein???

OMBI KWA MODS,

Kwa heshima ya hii thread, umuhimu na uzito wake; ingekuwa vyema kama mngemwadabisha kidogo huyu Lukosi kwani inaonekana wazi kuwa anataka kuvuruga mtiririko mzima wa hili bandiko.

Najua ana ID nyingine nyingi lakini kwa hiyo yenye jina lake naomba kama inafaa iadabishwe kwa kufungiwa ili wengine waweze kuchangia kwa amani zaidi.
 
aisee kumbe ndio maana lazima gas ije dar.mkuu TandaleOne natamani leo nione busara zako za kila siku
 
Last edited by a moderator:
OMBI KWA MODS,

Kwa heshima ya hii thread, umuhimu na uzito wake; ingekuwa vyema kama mngemwadabisha kidogo huyu Lukosi kwani inaonekana wazi kuwa anataka kuvuruga mtiririko mzima wa hili bandiko.

Najua ana ID nyingine nyingi lakini kwa hiyo yenye jina lake naomba kama inafaa iadabishwe kwa kufungiwa ili wengine waweze kuchangia kwa amani zaidi.

mkuu Chris Lukosi leo hana cha kusema, hivi unategemea ataandika nini? labda atwambie kama mpangon wa kukata pembe walizo zikuza wenyewe kama hupo.
 
Last edited by a moderator:
Duh! Sikujua kama kuna haya! Kumbe CCM 'zipo za aina nyingi?' Pia, utamtengaje Nyerere na CCM kipindi chake?! Hao wanaowaza hivyo, wapo sawasawa kweli?! Hapa ndipo CCM inaponifurahisha; mambo mabaya ya kipindi cha nyuma yaliyofanywa na viongozi waliopita wa serikali ya CCM, uwa yanazungumzwa katika misingi ya kiongozi husika, kama mtu binafsi! Lakini kwa mambo mazuri yaliyofanywa na viongozi hao waliopita, utasikia hayo ni mafanikio ya CCM!!

Kazi ipo!

Nzi umempandia bus NazDas....i like the conversations.
 
Tatizo ni kuchukulia mambo kirahisi kama wakati wa awamu ya kwanza vile, huku wakisahau ni wao walioamua kujenga shule za kata kila kata ambazo zimesaidia angalau watoto kujua utamu wa waliosoma kiukweliukweli.
 
OMBI KWA MODS,

Kwa heshima ya hii thread, umuhimu na uzito wake; ingekuwa vyema kama mngemwadabisha kidogo huyu Lukosi kwani inaonekana wazi kuwa anataka kuvuruga mtiririko mzima wa hili bandiko.

Najua ana ID nyingine nyingi lakini kwa hiyo yenye jina lake naomba kama inafaa iadabishwe kwa kufungiwa ili wengine waweze kuchangia kwa amani zaidi.
Mkuu mbona unahangaika sana ukiona Jina langu?
 
Kimiundo mbinu mtwara haijawa tayari kwasababu kwanza kama itazalisha umemene ina maana mradi wa kilimo kanda ya kusini na mradi wa chuma mchuchuma utakuwa kwa kiasi kikubwa lakini mtwara haina reli,bandari ni ndogo na kiwanja cha ndege ni kidogo hivyo hatakama itakama gesi itabaki mtwara nakuzalisha umeme na pia kutumika kutengeneza plastiki,mbolea,magunia na vitasafirishwaje kutoka mtwara? Hivyo basi serikali imechukua atua ya kuipunguzia mzigo mtwara wakijisahau kuwa mradi wa 300MW bado unaendelea ambao nao utakuwa na yenyewe itaongeza uzalishaji na kusababisha mtwara kulemewa kwahiyo chakufanya ni kuwajenge mtwara miundo mbinu ili wasilimewe na mzigo wa bidhaa zitakazozalisgwa alafu na gesi iendelee kusafirishwa lakini sio kuletwa dar es salaaam gesi ni raw material sio bidhaaa hivyo ibaki hukohuko
 
Chifu, nilishiriki zoezi moja la kuangalia namna mradi wa SongoSongo - gas to electricity - umeweza kuwa na manufaa kwa viwanda vinavyotumia gesi na taifa kwa ujumla.

Kwa kweli kama viwanda hivyo nilivyoenda ndivyo serikali inavisemea, hakika sioni kwanini viwanda vya aina hiyo visijengwe Mtwara pale pale. Kwani katika viwanda vyote vinavyotumia gesi ya Songas, ni kiwanda cha Wazo Hill tu ndicho naweza kusema ni kikubwa na kinachotumia gesi zaidi.

Unavijua vingine? Ngoja nikutajie:
1. OK Plast Limited
2. Kioo Limited
3. TCC (TZ Cigarette Company)
4. ALAF Limited
5. Murzahi Soap and Detergents
6. Kamal Steel Limited
7. Bakhresa Food Products Limited
8. YUASA Battery (EA) Limited
9. Bora Industries Limited
10. TBL
11. Serengeti Breweries
12. Simba Steel
13. NIDA Textile
14. Urafiki Textile
15. Nampak (T) Limited
16. Silafrica (T) Limited
17. East Coast Oil and Fats Limited
18. Murzah Oil Mills Limited

Hivi ndivyo navyovikumbuka; lakini kama kuna nilivyovisahau, haviwezi kuzidi vitano.

Matumizi makubwa ya gesi katika viwanda hivyo ni kwa ajili ya boilers, metal preheating, glass melting na drying and dehumidification. Kwa maana nyingine, gesi haitumiwi katika shughuli kubwa za uzalishaji katika viwanda hivyo. Yaani gesi inachangia kwa asilimia ndogo sana (kama energy) katika uzalishaji kwenye viwanda hivyo. Ingawa ni ukweli ulio wazi kwamba, matumizi ya gesi katika processes hizo za uzalishaji, yamesaidia sana upunguzaji wa gharama za uzalishaji katika viwanda hivyo.

kimiundombinu mtwara italemewa na mzigo hizo bidhaa zitasafirishwaje kutoka hapo mtwara hamna reli banndari ni ndogo na kiwanja cha ndege ni kidogo kwahiyo waboreshe miundo mbinu kwanza ndo hivyo viwanda viende huko pia ikumbukwe bila miundo mbinu imara mtwara italemewa tu kwasababu huo mradi wa hizo 300 MW utaboresha mradi wa kilimo wa kusini na mradi wa chuma mchuchuma na liganda
 
Invisible many thanks mkuu na asante kwa hili ni moto wa gas asilia ya Mtwara wataungua sana na ndiyo maana no Lumumba boys kwenye hii thread .CCM teknolojia inawatesa mno
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom