Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Mheshimiwa Mrema,
Najua kuna wengi watasema kuwa hili haliwezekani au halitakiwi kuwezekana. Najua kuna wengi watakataa kabisa kulipa hili jambo nafasi. Najua kuwa wapo pia wengi ambao watasema kuwa huu ni upotevu wa muda.
Hii imekuwa kawaida ya wengi wetu kuangalia yasiyowezekana zaidi ya kuwa na muda wa kuangalia yanayowezekana. Wakati nikiwa kitoto kichanga, mama yangu alitumia muda kabla ya kulala kuniambia ni jinsi gani yanayooneka kuwa magumu yanaweza kufanyika. Hajachoka kunikumbusha waliosema kuwa yeye kama Mhaya asingeweza kuolewa na kijana wa kichaga na wakaishi kwa raha na amani maisha yao yote. Maisha yote haya yeye na dadi wamewathibitishia ma-naysayers kuwa mengi sana yanawezekana.
Mheshimiwa Mrema AKA mzee wa kiraracha AKA mzee wa pilau AKA mzee wa mabomu AKA (tena muhimu sana) mkombozi wa wanawake Tanzania, naomba sana tena sana ufikirie sana ombi langu hili kwako. Kwa miaka yote hii familia yangu imekuwa inakuunga mkono katika juhudi zako za kupigania demokrasia na maendeleo tena. Familia yangu imekuwa nawe katika kutetea masilahi ya wanawake Tanzania. Na zaidi sana, sisi na watanzania wengi sana tumekuwa nawe katika misukosuko yote (ukiwemo ule ambapo mimi na dada zangu wote kwa pamoja tulipigwa mabomu ya machozi na polisi Tanzania bila sababu ya msingi tukihudhuria mkutano wako).
Mheshimiwa Mrema, mengi umeyafanya kwa ajili ya hii nchi yetu. Wengi hapa watakuita kichaa (kama alivyofanya mkapa na usalama wake wa taifa), chizi, au jina lolote lile watakalopenda. Hata hivyo historia ya Tanzania itakumbuka ulivyomsimamia Mama Siti na wezi wenzake pale Airport ili kuzuia dhahabu na vingine vilivyokuwa tayari kutoroshwa. Wengi tunakukumbuka kwa kupigana na mafisadi wakati ule ambao wengi tukiwa bado tunamuogopa baba wa taifa na kifimbo chake.
Kwa haya yote na mengine mengi ambayo nimekuwa nayasema hapa, naomba sana ufikirie mwelekeo na hatima ya nchi yetu sasa hivi zaidi kuliko mwaka ule wa 1994 ulivyojiunga rasmi na upinzani na ukaleta nguvu na hamasa kubwa na ya pekee.
Nakuomba sana uungane nguvu na wadogo zako na watoto wako kina Zitto, Dr Slaa, Mbowe, Mwera, na wapenda maendeleo ambao wanaendeleza yale yote ambayo umekuwa unapigania. Nakuomba ujiunge na CHADEMA ili ujenge chama chenye nguvu zaidi ya kuwaletea watanzania maendeleo. Kuna watu wenye chuki za kikabila watasema kuwa kujiunga kwako na CHADEMA kutakifanya kiwe cha wakasikazini. Jibu la swali hilo liko kwenye speeches za Barack Obama ambazo amekuwa anasema hapa USA kwenye kampeni zake, kama wewe ni mzungu na unazama baharini, je kama akitokea mtu mweusi kwenye boti akakurushia life line ili kuokoa maisha yako, je utaikataa kwa vile tu huyo mwokozi wako ni mweusi? Mama yangu alishalijibu hili swali pale alipokubali kuanza maisha na mchaga. Haijalishi rangi au kabila ya mtu inapokuja kwenye suala la maisha na kifo.
Haijalishi asili au kabila pale inapokuja kwenye masuala ya maendeleo. Zaidi sana, haitajalisha sana yaliyotokea huko nyuma kama kitakachofanyika sasa hivi ni kitu muhimu sana kwa watanzania wote. Mheshimiwa Mrema, tafadhali sana jiunge na wenzako ili kuongeza nguvu mapambano dhidi ya mafisadi wa Tanzania.
Asante