Ombi la Haraka la Uchunguzi wa Ushindani wa Haki katika Ligi Kuu ya NBC

Ningeiona barua ningeamini coz sitaki kukubali kama Jemedari amekua mpuuzi kiasi hiki.

Pia angeanisha kwa huo udhamini wa timj nyingi nani ni mnufaika na kwa namna gani?

1. Miaka kadhaa nyuma Sportpesa walidhamini simba na yanga, pia nadhani bia ya kilimanjaro ilidhamini simba na yanga, nani alionewa na nan alinufaika?
2. Kuna timu za JKT Tanzania na Mashujaa zote ni za jeshi mbona hilo halioni?
3. Azam media wanadhamini ligi yote na wanafamilia ya azam wanamiliki timu mbona huo mgongano hauoni?
Kama ni kweli ameandika barua hiyo basi amejishushia heshima kwangu mimi.
TBL au SPOTI PESA WALIKUA VIONGOZI WA TIMU GANI WAKATI HUO NA NANI ALIKUA KWENYE JOPO LA MAAMUZI.
 
Yupo sahihi Ila alichokosea ni kuiambia tff ijichunguze, mwigulu ni mdhamini halafu mmiliki wa Ihefu, mavunde yupo yanga wakati huo huo yupo Dodoma jiji.
Jambo jingine timu zote hizo Kama wanadhaminiwa na sportpesa ni wote, gsm ni wote, hero ni wote .
 
Yupo sahihi Ila alichokosea ni kuiambia tff ijichunguze, mwigulu ni mdhamini halafu mmiliki wa Ihefu, mavunde yupo yanga wakati huo huo yupo Dodoma jiji.
Jambo jingine timu zote hizo Kama wanadhaminiwa na sportpesa ni wote, gsm ni wote, hero ni wote .
Mwigulu ni mdhamini wa timu gani?
 
Kuna sehemu sijaelewa, yaani pamoja na kujikuta una jicho la tatu kwenye kuona mambo bado unatwambia tafsiri ya TFF(Tanzania football federation) ni chama cha mpira wa miguu Tanzania? Hauko serious
 
GSM ni mmilki wa Yanga au ni mdhamini? Kama ni mdhamini tu mgongano wa maslahi unatoka wapi?
Tuangalie wenzetu wanafanyaje kuhusu sonsorship na ownership. UEFA kwa mfano wanaruhusu mtu mmoja au kampuni moja kuwa kit sponsor kwa zaidi ya timu moja lakini hawaruhusu mtu mmoja kumiliki timu zaidi ya timu moja kwenye mashindano yao ingawa kuna dalili wanaweza kulegeza msimamo huo.
Shirt sponsor hahusiki na day to day running of the club.

Kuna kitu amvacho kila mtu anajua kwamba Simba ana matawi yake(timu). Lakini katika mechi nne zilizopita Ihefu kaifunga Yanga mara mbili. Msimu huu ndiyo timu pekee iliyoifunga Yanga. Swali la kujiuliza why now? Tumuulize Jemedari Said.
Umeandika upupu mtupu.... UEFA anasimamia soka barani Ulaya na TFF anasimamia na kuratibu soka nchini Tz pekee.
Leta mifano la kutoka kwenye mashirikisho yaliyochini ya EUFA ilitujifunze kama wana udhamini wa namna hii (uliopo NBC PL) kutoka huko barani Ulaya.
 
Machi 10, 2024

Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania
[TFF]

KUMB: Ombi la Haraka la Uchunguzi wa Ushindani wa Haki katika Ligi Kuu ya NBC

Mpendwa Mheshimiwa/Bibi,

Tunakuandikia kukuletea jambo linalotia wasiwasi mkubwa kuhusu uadilifu na usawa wa Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania. Kama wadau na watetezi wa usawa katika nyanja ya soka, tunaamini ni muhimu kushughulikia masuala yanayoweza kuhatarisha uadilifu wa ligi.

Imefahamika kuwa mmoja wa wanahisa wa klabu ndani ya Ligi Kuu ya NBC pia anafadhili vilabu vingine sita vya ligi hiyo hiyo. Klabu hizo ni pamoja na Namungo, Coastal Union, Ihefu, Tanzania Prisons, Singida Fountain Gate, na Young Africans, zote zikifadhiliwa kupitia kampuni tanzu au ubia wa chapa.

Uhusiano wa karibu wa mfadhili mmoja na vilabu vingi huibua wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa migongano ya kimaslahi na uadilifu wa ushindani wa haki ndani ya ligi. Kuna hatari kwamba uhusiano kama huo unaweza kusababisha ushawishi usiofaa katika matokeo ya mechi, na hivyo kuhatarisha uadilifu wa ligi na kudhoofisha ari ya mchezo wa haki.

Zaidi ya hayo, tumezingatia miungano kuu ifuatayo:

Rais wa Young Africans ndiye Mkurugenzi wa uwekezaji wa wafadhili wa timu hizo (GSM) na chapa yake shirikishi na rais wa chama cha vilabu Afrika.

Abbas Tarimba, Mkurugenzi Mtendaji wa Sportpesa, anahudumu kama mdhamini wa Young Africans, na Sportpesa inafadhili baadhi ya vilabu katika Ligi Kuu ya NBC.

Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha, pia ni mdhamini wa Young Africa lakini mtoa maamuzi mkuu ikiwa si mbia wa Ihefu na Singida Fountain Gate.

Anthony Mavunde ni mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya Jiji la Dodoma lakini pia ni mdhamini wa Young Africa.

Kutokana na matatizo hayo, tunaomba kwa heshima Chama cha Soka Tanzania kuanzisha uchunguzi wa kina na huru kuhusu suala hilo. Uchunguzi unapaswa kulenga kubainisha iwapo kuna matukio yoyote ya upangaji matokeo, kula njama, au aina nyingine za ushawishi usio wa haki wakati timu hizi zinachuana dhidi ya nyingine au vilabu vingine ndani ya ligi.

Aidha, tunashauri Chama cha Soka Tanzania kuwashirikisha wadau husika wakiwemo viongozi wa klabu, wachezaji, waamuzi na wataalam wa kujitegemea katika mchakato wa uchunguzi ili kuhakikisha uwazi na kutoegemea upande wowote.

Kwa kuzingatia athari zinazoweza kuathiri uaminifu wa soka la Tanzania, tunaomba pia nakala za barua hii zipelekwe kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa ufahamu wao na kuzingatiwa.

Ni muhimu kuzingatia kanuni za haki, uwazi na uadilifu katika soka katika ngazi zote. Kwa hiyo, tunaamini kuwa Chama cha Soka Tanzania kitachukua hatua za haraka na madhubuti katika kushughulikia masuala haya na kulinda uadilifu wa Ligi Kuu ya NBC.

Asante kwa umakini wako kwa jambo hili. Tunatazamia majibu na hatua zako za haraka katika kuhakikisha uadilifu na usawa wa soka nchini Tanzania.

Kwa dhati,

BOB_Esq✍️✍️✍️✍️✍️

CC:
Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA
Huu ni uubwabwa.
 
Ana hoja ya msingi sana! Ila mashabiki wengi kutokana na kuwa na shule ndogo ukijumlisha na ujinga na ushamba hawawezi kumuelewa,wataishia kumtukana tu.

Ujinga na siasa za kipumbavu zilizojaa kwenye michezo ndio zipo kwenye sekta nyingine!
Kama hamto badilika na kuanza kujenga timu yenu mtaendelea kulalamika mpaka 2030 wakati Yanga anachukua ubingwa back to back
 
Rais wa caf pia ni mmiliki wa Mamelodi Sundowns klabu ya South Africa inayo shiriki Mashindano ya Caf hassa klabu bingwa.
Klabu kadhaa zimelalamika kuhusu hilo hassa kuhusu waamuzi wanaochezesha mechi zao huko South Africa.
 
bro ukitaka conflict of interest isiwepo hapo hersi saidi kama kiongozi wa yanga ajiuzu cheo chake pale yanga na asiratibu mambo ya timu,abaki kama mfadhili tu chini ya kampuni ya baba yake 'GSM' Otherwise hayo yote uliyoyasema ni porojo tu
Hersi ajiuzulu
Labda ungesema GSM asizamini timu zingine ibaki kwa Yanga tu,, hizo timu ndogo ndogo ziendelee kuteseka
 
Umeandika upupu mtupu.... UEFA anasimamia soka barani Ulaya na TFF anasimamia na kuratibu soka nchini Tz pekee.
Leta mifano la kutoka kwenye mashirikisho yaliyochini ya EUFA ilitujifunze kama wana udhamini wa namna hii (uliopo NBC PL) kutoka huko barani Ulaya.
Castore - Newcastle na Astonv Villa
Bet365 - Newcastle na Wolves
Adidas - Arsenal, Man U, Fulham, Nottingham Forest
Nike - Chelsea, Liverpool, Tottenham, Brighton
 
Rais wa caf pia ni mmiliki wa Mamelodi Sundowns klabu ya South Africa inayo shiriki Mashindano ya Caf hassa klabu bingwa.
Klabu kadhaa zimelalamika kuhusu hilo hassa kuhusu waamuzi wanaochezesha mechi zao huko South Africa.
Sio kweli
 
bro ukitaka conflict of interest isiwepo hapo hersi saidi kama kiongozi wa yanga ajiuzu cheo chake pale yanga na asiratibu mambo ya timu,abaki kama mfadhili tu chini ya kampuni ya baba yake 'GSM' Otherwise hayo yote uliyoyasema ni porojo tu
Hiki ndicho mnachofanya?? Si mlimuona muhuni now mnataka aondoke Yanga, haendi kokote. Nenda polisi sasa
 
Back
Top Bottom