Ombi kwa Ras Magufuli: BRELA imeshindikana, iweke chini yako

BRELA sio sekta,ni kitengo kidogo tu.
Na kwa nini unafikiri ikiwekwa chini yake ndio itafanya vizuri?
Mheshimiwa Rais.

Unahangaika kutaka kuifikisha nchi hii kwenye uchumi wa kati na wa viwanda kutimiza mipango ya maendeleo tuliyojiwekea kama taifa.

Moja kati ya sekta ambayo ni muhim kutekeleza hayo ni BRELA lakini kwa bahati mbaya sana wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwenye kusajili na pia kufanya malipo.

Kwa kifupi mtandao wa BRELA hauruhusu u yoyote yule kufanya yafuatayo:

1. Ku search jina la biashara au kampuni (Name search)....hii wanataka ufanye manually and it takes 2 weeks kupata majibu

2. Kujua wamiliki wa hizo kampuni ni akina nani na wanamiliki asilimia ngapi (shareholding structure)

3. Kufanya malipo kwa njia ya Simu au benki kupitia kwenye mtandao wa e-payment wa Serikali

4. Kufanya returns online


Mheshimiwa Rais, Waziri husika na viongozi husika watakwambia hayo yote yapo lakini sio kweli. Mhehsimiwa Rais, naomba uingie kwenye mtandao wa Brela kisha jaribu kutafuta jina la kampuni yoyote kwa kifupi hutopata hizo taarifa.

Kwa kumalizia na kukufanyia wepesi hawa ndio wahusika wakuu BRELA:

Waziri wa Biashara, Ndugu: Joseph Kakunda
Naibu Waziri wa Biashara, Ndugu Stella Manyanya
Katibu Mkuu wizara ya Biashara, Ndugu JosephBuchweishaija
Waziri wa Uwekezaji ,Ndugu Angelina Kairuku
Mkurugenzi Mkuu BRELLA ...................


Ushauri. Mheshimiwa naomba kama imeshindikana ichukue hii uiweke chini yako maana hao uliowapa majuku wameshindwa


ushahidi wa haya ninayosema huy hapa:

BRELA ORS

Loyalty To country Always,To government When it deserves
 
Brela ni kichefuchefu

sijui kweli wanaofanya kazi pale huwa wanaaga wanaenda brela??

inahitaji ubunifu, ukali, na ufuatiliaji
 
nimeona nguvu ya mitandao ya jamii,hasa JF kaimu mtendaji mkuu ametoa taarifa kwa umma kuhusu hizi tuhuma kwenye gazeti la leo UHURU NA MWANACHI ,Mtendaji amejitetea vema kabisa kulinda ugali wake na heshima ya taasisi.
ila ukweli unabaki palepale software ya usajili iboreshwe kuondoa malalamiko haina ufanisi wa kutosha ndio maana kila kukicha vishoka ,third party wataendelea kuwepo.... igeni mfumo wa sumatra kukata leseni umekuwa rafiki mpaka umeondoa ukishoka

pia nawashauri waanzishe cal centre wameandika namba feki kwenye website yao ukipiga hazipatikani wa email hawajibu,msidhani kuwa wote ni wakaazi wa dsm ,tanzania ni kubwa sana.

kwa wanaJF Watakao shindwa kununua gazeti ,mkiwa na malalamiko CEO wa Brela ametoa namba yake 0754565908 Kama ukiona kuna ukiukwaji kwenye kupata huduma
Magufuli fumua brela wakukosesha mapato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora mmenifungua macho,naskiaga tu BRELA,kumbe inahusika na usajil wa makampuni!?ss cc wamiliki genge tutasajilia wap?
 
Brela kweli imekuwa ni tatizo kubwa sana .na imekuwa wanatukwamisha sana sisi wakopaji kwenye mabenki.wanapotaka official seach.ukiingia kwenye mtandao wa Brela mtandao una sumbua kwelikweli.na wana kosesha fedha serekali .kwa matatizo yao ya kimfumo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama wanashindwa jambo dogo kama website what makes you think idara zingine ndani ya BRELA ziko sawa?
 
Hivi vitu unaweza ukaviona rahisi lakini vinagharimu sana uchumi wa nchi
Niko ughaibuni nimekutana na investors wana hamu kuja kuwekeza Tz kwenye sector 4 tofauti wanataka kujua conditions
Nikasema ngoja niende TIC, kwenye upande wa inquiry nikaainisha matakwa yangu
Pale unaacha email na number ya simu na nilifanya hiyo shughuli jana kabla ya saa 12 asubuhi nikitegemea labda kabla ya saa 4 asubuhi nitapata jibu mpaka hii leo ni kiiiiiiiiimya

No way out jamaa wameishaona labda the best way nije nao huko Bongo na watakuwa na siku 3 tu. Lakini walikuwa wanataka kujua vitu vingi kabla hawajafika ili wajipange na wakifika iwe ni utekelezaji tuu
Hawa watu ninavyowaheshimu natamani niwapekeke Rwanda. Maana hawaniambii lakini najua watanitathmini kulingana na haiba ya kitaasisi za nchi ninayotoka

Kujibu Email tuu jamani inachukua more than 30 hours

Kwa taasisi kama TIC hii ni zaidi ya MSIBA

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfumo wa BRELA online ni upigaji wa hatari.
Vijana wanapewa facilitation kwa kupitia vibanda vya wakala wa pesa/MPESA/TIGO ETC , hawatumiwi tena kwenye simu, kazi inatoka ndani ya siku moja huku ikiacha kazi zenye miezi pending.
mh Magufuli hii rushwa ya BRELA ni zaidi ya bandari na TRA.
 
b8b7d751-64a7-4f60-aba9-e26ef1a41fd4.jpg
 
Back
Top Bottom