Omar Juma Kipanga amewaambia wananchi wa mafia baada ya kimbunga Hidaya

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
356
558
MHE QS KIPANGA SHIDA ZENU SHIDA ZANGU KIMBUNGA HIDAYA MAFIA

KILINDONI MAFIA

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Juma Kipanga amewaambia wananchi wa mafia kata ya Kilindoni Kijiji Cha kilindoni Vitongoji kumi na moja kuwa shida zao shida zake juu ya majanga ya Kimbunga HIDAYA,

Akizungumza wakati wa Ziara ya kuzungumza na Wananchi mbalimbali wenye nyumba ambao wameadhirika na Kimbunga Cha HIDAYA mnamo usiku wa 03/05/2024 ambapo Nyumba na Mazao mbalimbali yaliadhirika Wilaya Mafia,

"Nipo Hapa ndugu zangu wa mafia kuwafariji na kuwapa pole katika janga Hili Kimbunga Cha HIDAYA lakini pia mjue kuwa shida zenu ni zangu ndio maana ofisi yangu ikaamua kutoa mshahara wangu kwenu ili kusaidia machungu ya Kimbunga" alisisitiza MHE QS KIPANGA,

"Nina Imani nanyi Siku zote naomba mjue kuwa Serikali imeandaa utaratibu mzuri unakuja kwenu pindi ukikamilika Kupitia Kamati za Maafa za Wilaya hivyo muwe na Subira Endeleeni kutoa Ushirkiano kwa wenyeviti wa Vitongoji na wamatawi wa Chama"Alisisitiza MHE QS KIPANGA,

Mwisho ziara ya kutembelea na kuwapa Faraja waliopatwa na Maafa ya Kimbunga HIDAYA inaendelea kwa kata zote za mafia zilipopatwa na Maafa.
2a301e2439eb422faee681dcd0a367df.jpg
3ce3f4fed8a8471ca625281fa2c4a2dc.jpg
9f25fc54e95e4a6baaf2acf3975f300d.jpg
86e84271c40f4cb6bb90b252d0157bd4.jpg
80907905f2be46a1943b302bf2ade5e6.jpg
5c254e7363f94e6da53a4dfb9c63d828.jpg
234fb8459e9e4c36a65e0313e2488f58.jpg
432061d7ffd942e5866f49bb1f8a2a76.jpg
bb125595152446eb87fb2262fadf30dc.jpg
40cd1ed5291940d8b7f5e68269c4b71e.jpg
a2a28bbffbb3483eb2856c4f5f1319e4.jpg
298069993ae74c7691d90a2b264f5b5f.jpg
62de6df41c5b40258f617965d284c99b.jpg
fa16776e21e74feab4000f1fb11f9bde.jpg
e58faa1b1c41463281cd463ddd175566.jpg
293a436a35e34b799295c6ba3171ed94.jpg

Matukio mbalimbali ya Picha wakati wa Ziara ya kuzungumza kuwapa Pole na Faraja waliopatwa na Maafa Wilaya Mafia kata ya Kilindoni ya MHE QS OMAR JUMA KIPANGA Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia leo alasir 09/05/2024.
 
Back
Top Bottom