Uchaguzi 2020 Ole Sendeka anahaha na ubunge wa Simanjiro,awatumia Mzee Mangula,Malecela na mkewe kumsaidia kutokatwa jina lake

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Wakati vikao vya ngazi za juu ndani ya Ccm vikiendelea na mchakato wa kupitia majina taarifa za ndani zinaeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Christopher Ole Sendeka ameanza kuhaha kutafuta msaada kwa baadhi ya vigogo ndani ya Ccm ili waweze kumnusuru na panga la kukatwa jina lake baada ya ripoti kutoka vyombo vya usalama TISS na TAKUKURU kuelezea namna alivyotumia rushwa,ukabila na matumizi mabaya ya Madaraka katika kushinda nafasi ya kura za maoni za Ccm katika jimbo la Simanjiro .

Chanzo cha habari hii kinasema baada ya Bw. Christopher Ole Sendeka kufanya Tadhmini na kusikia kwamba repoti zake kuhusu rushwa alizotumia katika mchakato wa kura za maoni kabla na baada ya tarehe hiyo ya kura za maoni timu ya Ole Sendeka imepanga mikakati kadhaa ikiwepo;

1. Kumuendea Mzee Mangula, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa ili kutokana na historia ya Ole Sendeka huko Njombe akiwa Mkuu wa Mkoa huo na pia mahusiano yao ya muda mrefu katika kazi za kiuongozi ndani ya CCM, Mzee Mangula aweze kumtetea katika kuteuliwa na kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa Novemba 2020.

2. Mkakati mwingine uliyoandaliwa na Ole Sendeka na wapambe wake ni kutumia fedha yeyote ili kushawishi watu wenye maamuzi ya chama miongoni mwao akiwemo Mzee Mangula na kazi hii ya kumsaidia Ole Sendeka katika Uteuzi unafanywa pia na Mke wa Mzee Malecela Mama Anna Kilango Malecela na Mzee Malecela mwenyewe ili kumsaidia rafiki yao wa muda mrefu katika harakati za CCM miaka ya hapo nyuma.

3. Ni vema ikumbukwe kwamba familia ya Mzee Malecela imekuwa Karibu na Ole Sendeka kwa muda mrefu kutokana na Ole Sendeka kuwa miongoni mwa vijana ambao walitamani sana kuona Mzee Malecela akishinda kura za uteuzi wa kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2005 hivyo inasemekana timu ya Ole Sendeka wanajaribu kila mbinu za kumtetea Ole Sendeka katika uteuzi kupitia kila mtu aliyekaribu naye ili makosa yake yote yaliyoandikwa kabla na wakati wa kura za maoni yatupwe mbali na wenye mamlaka ya Uteuzi.

4. Kwa vyanzo Hivi vya uhakika vinakiri pia kwamba tarehe 12/07/2020 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliyofanyika jijini Dodoma Mzee Malecela akisukumwa na tamaa za Ole Sendeka za kutaka kushiriki kwenye kura za maoni za CCM za Jimbo la SIMANJIRO walifanya kila juhudi za kumtafuta Mwenyekiti wa CCM wa Taifa, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili amruhusu Ole Sendeka kwenda SIMANJIRO kugombea Ubunge na kuacha nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa.

5. Jitihada zote hizi za Ole Sendeka na timu yake ni ili Mzee Mangula na watu wenye ushawishi ndani ya vikao vya maamuzi vya CCM watumie nafasi zao kukataa ripoti za kiusalama na TAKUKURU dhidi ya Bw. Christopher Ole Sendeka zinazoonyesha rafu aliyoitumia kushinda uchaguzi.

6. Pamoja na kwamba Mzee Mangula ni mtu anayeaminika sana na mtu mwadilifu na ni kati ya WAZEE wachache wanaotegemewa kukitetea CCM katika mazingira haya magumu ya baadhi ya watu kuaminisha umma na Wana-CCM kwamba ili kushinda kura za maoni za CCM ni lazima utumie rushwa, tunamuomba ajihadhari na utapeli wa Ole Sendeka na akumbuke kwamba, Ole Sendeka huyu huyu na kundi lake wamekataliwa na watu wa SIMANJIRO Mwaka 2015 kwa kura Nyingi sana kutokana na Ole Sendeka kuchokwa na wananchi na kundi lake kuingia kwenye migogoro mikubwa na wananchi kwa kuuza Ardhi ya Wananchi.

7. Leo kundi la Ole Sendeka wakijaribu kushawishi Viongozi waandamizi wazikatae ripoti za vyombo vya Ulinzi na USALAMA vya maeneo husika, wanataka wazee hawa na Viongozi wa Chama Tawala waamini kwenye nini? Vyombo hivi havina mgombea na vyenyewe vinasimama katikati ili kulinda USALAMA wa nchi yetu na kutetea ukweli siku zote. Tunaomba WAZEE kama kina Mzee Mangula na Mzee Malecela wasiingizwe kwenye uchochoro huu wenye masilahi ya kutetea tamaa za Ole Sendeka na kundi lake ambao wamechokwa sana na watu wa SIMANJIRO ili kukinusuru Chama Cha Mapinduzi Wilayani Simanjiro kwenye uchaguzi huu Mkuu Ujao unaotarajiwa kufanyika Novemba Mwaka Huu.

Mwisho
 

Attachments

  • BB1E57A8-03B7-4253-8756-136773ABF134.jpeg
    BB1E57A8-03B7-4253-8756-136773ABF134.jpeg
    50.5 KB · Views: 2
Hivi huyu hawezi kufanya shuguli nyingine

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Kuna siri kubwa kwenye ubunge ambayo kama hujawahi kuwa mbunge kamwe huwezi kuijuwa

Mkuu wa mkoa na mbunge mkuu wa mkoa ndio mkubwa, sasa ukiona watu wanaacha nafasi hiyo kwenda kucheza kamari ya kugombea cheo cha kuchaguliwa ujiulize sana kuna nini?
 
Ugomvi wa Milya na Sendeka ni wa muda mrefu sana nakumbuka hawa walishawahi hadi kutishana bastola na kufikia kupelekana mahakamani pale mahakama ya mkoa Arusha.
 
Kwangu mimi namchukulia ile Sendeka kama mbunge wa kitaifa sijuajua huko Simanjiro mnamchukuliaje
 
Tangu awali nilisema Ole sendeka alitoa rushwa na alivuruga uchaguzi simanjiro.wengine ni prof muhogo,sajini Kule butiama,sashisha Kule hai,Ibrahim shayo na priscus kimaryo Kule Jimbo la Moshi mjini, tulia Kule mbeya mjini,Jimbo la rombo Prof Adolf mkenda,gambo Arusha mjini,mathayo David Jimbo la same, mwandri na mollel Jimbo la siha,Hawa wote walikuwa vinara wa kutoa rushwa kwa wajumbe.ccm waepukeni Hawa watu.pia walishirikiana na makatibu wa CCM wilaya zao na wenyeviti wa CCM mkoa na wilaya.
 

Attachments

  • VID-20200806-WA0003.mp4
    14.9 MB
Pamoja na mapungufu yao, Sendeka na Mwanri ingependeza wapitishwe wakachangamshe bunge.
 
Tangu awali nilisema Ole sendeka alitoa rushwa na alivuruga uchaguzi simanjiro.wengine ni prof muhogo,sajini Kule butiama,sashisha Kule hai,Ibrahim shayo na priscus kimaryo Kule Jimbo la Moshi mjini, tulia Kule mbeya mjini,Jimbo la rombo Prof Adolf mkenda,gambo Arusha mjini,mathayo David Jimbo la same, mwandri na mollel Jimbo la siha,Hawa wote walikuwa vinara wa kutoa rushwa kwa wajumbe.ccm waepukeni Hawa watu.pia walishirikiana na makatibu wa CCM wilaya zao na wenyeviti wa CCM mkoa na wilaya.
Vipi kuhusu kigambonino.
 
Kadhia za hivi ni NYINGI na bila shaka CCM wanajitafakari ateuliwe nani sasa, maana sidhani kama miongoni mwa walioshinda na hawana tuhuma za rushwa wanazidi 5% ya washindi. Mwisho wa siku tutaweka kwenye mzani wa gharama kukata washindi na kuweka wasiotoa rushwa lakini hawana ushawishi au twende mbele na watoa rushwa. Hapo ndio utakiri kuwa hata malaika apewe uenyekiti, haitawezekana kuitenganisha CCM na rushwa. Rushwa na CCM na CCM ni rushwa.
 
Back
Top Bottom