Ole Mushi:Nchi ya ajabu hii ivi kuwa na bahari, mito na maziwa tunaagiza samaki toka china? Mawaziri kazi kuchoma nyavu tu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kuna vitu vinenifikirisha sana wiki hii:-

Na Thadei Ole Mushi

SAMAKI TOKA CHINA.

Sikuwahi kufikiria kwamba kwenye Super Market zetu kuna Samaki toka nchi nyingine. Mimi nilifikiri Samaki wote wanaouzwa nchini kama hawajatoka kwenye maziwa yetu Makuu yaliyo kila pembe ya nchi hii basi wanatoka kwenye eneo letu la bahari. Narudia tena sikuwahi kufikiria kama kuna Samaki wanatoka mbali kiasi hicho kuja kuuzwa hapa nchini kwetu.

TWENDE SAWA HAPA.

Tanzania ni Moja ya nchi zilizobarikiwa duniani wana maeneo mengi na makubwa ya maji ambayo ni makazi ya samaki. Hivyo sidhani kama tuna upungufu mkubwa kiasi cha kuagiza njee samaki tena toka china. Haya ni maajabu ya Tanzania.....

Ukimuona waziri au Naibu waziri anakutana na wavuvi wa Tanzania basi jua kashakamata nyavu za kuchoma au wamebeba Rula ya kupimia ukubwa wa Samaki.

Huwezi kumkuta akisikiliza Kero za wavuvi Na kuwajemgea uwezo wavuvi wetu wavue Kisasa. Bado tunaendelea na uvuvi wa Ndoano na mtumbwi Tanzania. Wachina wanatuuzia Samaki hii ni aibu kubwa sana..... Tunawezaje Ku link tatizo la ajira kwa vijana wetu nchini rasilimali hii ya Samaki waliopo nchini? Tunajiuliza kinachofanya Dola kupanda ni nn?.....

Mh Rais alisema Wizara hii inahitaji mtu kichaa kama Mpina,natarajia ukichaa wa Mpina uhamie kwenye kuhakikisha Samaki waliopo nchini wanatutosha kwa Chakula na ziada tunauza njee.... Ukichaa wake usiishie kuchoma tu nyavu na kuharibu Samaki.

2. KOROSHO BADO IPO ICU.

BOT na TRA wametoa chati inayoonyesha mazao ya biashara tunayouza nje. Wamefanya Comparison kati ya mwaka Jana na mwaka huu.

Kwenye chati hapo chini Rangi ya blue inaonyesha mauzo ya mazao hayo kwa mwaka Jana na rangi nyekundu inaonyesha mauzo ya mwaka huu.

Mwaka Jana Korosho ilituingiza Dola za kimarekani Milioni 578.4 huku mwaka huu korosho ikiingiza Dola Milioni 25 tu. Hili ni anguko kubwa mno.

Kwa sasa Dr Mpango atakuwa anaelewa ile kauli ya wabunge wa kusini kuwa asifike Mikoa ya Mtwara na Lindi. Kwa sasa wataelewa kwa nn yule Mbunge alilia Bungeni kwa sasa sote tunamwelewa Nape na washirika wake.... Na kwa sasa tunamwelewa Hawa Ghasia kwa nini alijiuzulu kwenye kamati za Bunge.

Kwa sasa Serikali isipochukua Hatua wakulima wa mazao Haya wanaenda kuwa walalahoi Daraja la kwanza. Pale mtwara na Lindi ukiacha Korosho nn kingine wanachoweza kukifanya wakapata fedha? Tunajiuliza kwa nn Dola inapanda? Tumeshindwa Ku link kilimo chetu na tatizo la ajira kwa vijana?......

TANZANIA NI YA TATU AFRIKA KWA KUWA NA MIFUGO.

Tanzania ni ya tatu kwa kuwa na mifugo mingi Afrika, lakini mchango wa mifugo hiyo kwenye pato la taifa ni asilimia 7 tu.

Ukimsikia Waziri au naibu waziri kawatembelea wakulima ni kwamba aidha kuna wafugaji wamepigana na Wakulima au Luna wafugaji wamevamia hifadhi ya Taifa, au tunakwenda kupiga Mihuri kwenye mifugo.

Hakuna Link kati ya mifugo na Ajira kwa vijana.... Sijui tunakosea wapi.....

Ole Mushi
0712702602(
 
Mleta mada fursa hiyo changamkia.Samaki tunao wengi sana tatizo wavuvi hawana meli kubwa za uvuvi za kufanya uvuvi mkubwa wa kutosheleza mahitaji makubwa ya samaki.Jitose kwenye sekta ya uvuvi badala ya kukaa unabweka hapa
 
Back
Top Bottom