Ole Medeye ondoa boriti lilo kwenye jicho lako kwanza ndio uondoe la mwenzio

kijenge

Senior Member
Mar 9, 2012
179
164
Gudluck ole medeye naibu waziri wa maendeleo na makazi. anawahada wananchi wa arumeru mash kuwa sioi akipata ubunge atowapatia wananchi aridhi.wakati kwake amechukua shamba la luck luck yeye na mkapa kwa kisingizio wamempa mwekezaji agha khan.awape kwanza wananchi wa arumeru magh mashamba hayo ya luck luck ndio azungumzie mashamba ya valeska.
 
Huyu MP Medeye hajui hata anachokisema.Ni mbunge wangu na sie tuna shida sana ya asrdhi mbona hajatupugania sie kwanza.Aache ulimbukeni wa mawazo..CCM wote propaganda, bada ya uchaguzi wote KIMYAAAAAAAAA KAMA VILE HAWAKUWEPO KWENYE CAMPAIGN.........
 
Huyu MP Medeye hajui hata anachokisema.Ni mbunge wangu na sie tuna shida sana ya asrdhi mbona hajatupugania sie kwanza.Aache ulimbukeni wa mawazo..CCM wote propaganda, bada ya uchaguzi wote KIMYAAAAAAAAA KAMA VILE HAWAKUWEPO KWENYE CAMPAIGN.........


Wakawaulize wana igunga walivyoingizwa mjini na Magufuli wakati wa kampeni. CCM wameona issue ya ardhi itawapa shida ndo wanapeleka mawaziri kudanganya kwa ahadi hewa. Nadhani watamtuma hata na Professor TIBA kwenda kuwahadaa wananchi. Wananchi wasikubali maana ardhi ni haki yao siyo mpaka wakati wa uchaguzi tu ndo waje kuwadanganyia walikuwa wapi siku zote?
 
Hata mimi namshangaa sana huyu Olemedeye, kuna kipindi wananchi wa jimbo lake wa kata ya Nduruma walimfuata kuhusina na mashamba ya mkonge yaliyopo kata ya jirani ya Bwawani ili awasaidie wapate hayo mashamba. baada ya wananchi kumtafuta kwa muda mrefu alipokutana na tume iliyotumwa na wananchi akawaambia kuwa yeye ni kiongozi wa ngazi za juu mno na asingependa kujihusisha na jambo hilo. Wananchi walirudi na hatimae wakamfuata mkuu wa mkoa ati ndipo mkuu wa mkoa akamwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Arumeru magaharibi ashuhulikie jambo hilo, hatimae mkurugenzi alishuhulikia jambo hilo kikamilifu na wana nchi kupewa ekari 60tuu tena kwa bei ya juu ya sh 1400,000/-kwa eka jambo ambalo kwa kipato cha wakazi wa kata ya Nduruma hawawezi kumudu. Binafsi nina imani kuwa Medeye kama naibu waziri wa Ardhi na mwakilishi wa wananchi angeweza kushuhulikia hili jmbo bila urasimu na wananchi wakapata hayo mashamba kwa bei wanayoweza kumudu, Medeye asiwadanganye wananchi wa Arumeru mash kwani hata jimbo lake amelitelekeza hasa kuhusiana na masuala ya ardhi kwa mfano mgogoro wa jeshi kata ya Mlangarini. MSIDANGANYIKE
 
Back
Top Bottom