mkara mshamba
Senior Member
- Jan 15, 2020
- 105
- 103
MAYALA, nashukuru sana kwa hoja yako nzuri, unatutaka tunao jitambua tuwe wakweli,tuchague mgombea uras aliye tuletea maendeleo. Sawa kabisa nami nakubaliana na ww. Lakini kama unadai unajitambua nakuomba kwanza tujadili hizo pesa zinazojenga miundombinu na nk, vyanzo vyake ni halali ?. Maendeleo ya haki tunayo yaomba tunataka vyanzo vyake viwe vya haki. Mfano, UNAPO MKAMATA MTU NA KUMPA KESI HISIYO NA DHAMANA, KISHA KUMUOMBA AJE MEZANI MKAKUBALIANE AKAACHIA MAMILIONI YA PESA UKAENDA HIZO PESA UKAJENGA KITUO CHA AFYA. Hayo pia ni maendeleo, ni ya haki ama batili ? Tumewasikia wagombea wote, Lakini kama kweli wewe nimkweli lejea sera zao, utaona kuwa LISSU NA CHADEMA ndio wana sera nzuri. Wanatangaza kutawala kwa UHURU , HAKI NA MAENDELEO. Wewe naamini ni mkristo nakuomba usome BIBLIA kitabu hiki1 Wafalme 3:4-12Naona Dictators wa JF wana jitahidi sana kukubeza, bring in more nyuzi sisi tunao enjoy alternative opinion. Wewe ndio kioo cha mawazo yetu upinzani, tunajitazama kupitia kwako kama suit, shirt, tie na weist belt imekaa vizuri kisiasa. Thanks, keep it on.
[4]Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
[5]Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe.
[6]Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.
[7]Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
[8]Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi.
[9]Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?
[10]Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili.
[11]Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;
[12]basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app