OIC - Zanzibar kujiunga kivyake vyake

Sasa huyo mkulu anaongea nini wht is matrekta 50kwa Zanzibar???? Na kwa nini viongozi wetu wamejikita zaidi kwenye misaada ya wao kupewa na si kutoa pamoja na umasikini wetu?? Halafu bado eti ndani ya katiba tunasema Tanzania inafuat mfumo a ujamaa na kujitegemea.
Hivi wewe Mheshimiwa unataka kueleza nini. Matrekta Hamsini kwa Zanzibar is something else. Kuna majimbo Hamsini pale ya uchaguzi kila jimbo moja la uchaguzi litapata trekta lake. Jee? mangapi nyinyi mnapata msaada na kuyasambaza katika kila jimbo lenu la uchaguzi. Usibeze suala la misaada kwani Tanzania Bara ndiyo hiyo inakwenda kwa misaada tu. Unataka kuukataa ukweli hii leo?
 
Yaani Zanzibar haiwezi kujinunulia matrekta 50 mpake ipewe na OIC?
Jeernyinyi Tanzania Maunland kwanini hamuwezi kujinunulia matrekta na mkayasambaza katika majimbo yenu ya uchaguzi . Usishangae hilo sababu ni zilemzile zilizokufanyeni nyinyi mshindwe.
 
Zanzibar kujiunga na OIC kivyake

2009-01-27 10:14:33
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza kwamba itaiomba Serikali ya Muungano kuiruhusu Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiisalm(OIC) endapo mpango huo utashindwa kufikiwa na Serikali ya Muungano.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotaka kujua Serikali ina mikakati gani kuhakikisha Zanzibar inakuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.

Alisema kimsingi sula hilo bado linashughulikiwa na Serikali ya Muungano hasa kwa kuzingatia linahusu utaifa ``kwani Zanzibar ni nchi wakati taifa ni moja la Tanzania hivyo tutajiunga kama Nchi ,ndo maana yake.

Alisema Zanzibar haijuingi katika jumuiya hiyo kwa matakwa ya kidini bali inatetea kuchukua hatua hiyo kutokana na sababu za kiuchumi.

``Ikiwa itashindikana kwa Serikali ya Muungano kujiunga, Serikali ya Zanzibar tutaomba tujiunge kwa kujitegemea badala ya kuwa wanachama kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano,`` alisema Waziri Hamza.

Alisema kitendo cha kuchelewa kujiunga katika jumuiya hiyo kunachangia kutochangamsha maendeleo ya Zanzibar kutokana na misaada ya kijamii na kiuchumi inayotolewa na OIC.

Alitoa mfano kwamba endapo Zanzibar ingekuwa mwanachama ingesaidiwa matrekta 50 kupitia jumuiya hiyo na kusaidia katika sekta ya kilimo Zanzibar ambayo ingewanufaisha wananchi wote bila ya kujali imani zao za dini.

Ngoja nisuibiri kituko cha mwaka 2009. JMT itaweza kuruhusu hilo kwa kutumia sheria gani au katiba gani? Hivi Zanzibar ina uhusiano wa Kibalozi na Nchi gani au Taasisi gani? Itakuwa mpya na kwa Viongozi wetu wengi hilo hawawezi kuona hilo kuwa ni tatizo, wanaweza kuruhusu tu kama ilivyokuwa enzi za Mwinyi pale Dk Salmini alipoipeleka Zanzibar OIC na ikawa hadi pale Nyerere alipokuja juu. Ngoja tumsubiri Nyerer mwingine katika hili.
 
Zanzibar haiwezi kuruhusiwa kujiunga na OIC kwa sababu Zanzibar sio nchi. Kuiruhusu kujiunga itakuwa yaleyale ya uvunjaji katiba. Muungano wetu ni kama ndoa. Mke akililia sana kula chapati maji, ukamkatalia kwa vile wewe hupendi kula chapati hizo, akifikia hali ya kuomba kupika chapati hizo angalau ale yeye tuu na wewe usile. Kama mume mwenye busara, utamruhusu apike chapati maji na ili kumuonyesha unampenda, itabidi na wewe ukubali kula hizo chapati maji.
Katika suala la OIC, Zanzibar ni mke na OIC ni chapati maji. Ili kudumisha ndoa yetu ya muungano,itabidi URT ijiunge na OIC hata kama haipendi ili Zanzibar ipate chapati maji.
Ungekuwa uko kule kwetu Zenj. Ningesema mawazo haya ni kama ya wale (wanywa vinibu vya tende). Kumradhi Mheshimiwa - ulimi umeteleza.
 
Ngoja nisuibiri kituko cha mwaka 2009. JMT itaweza kuruhusu hilo kwa kutumia sheria gani au katiba gani? Hivi Zanzibar ina uhusiano wa Kibalozi na Nchi gani au Taasisi gani? Itakuwa mpya na kwa Viongozi wetu wengi hilo hawawezi kuona hilo kuwa ni tatizo, wanaweza kuruhusu tu kama ilivyokuwa enzi za Mwinyi pale Dk Salmini alipoipeleka Zanzibar OIC na ikawa hadi pale Nyerere alipokuja juu. Ngoja tumsubiri Nyerer mwingine katika hili.
Hapana kituko hapo. Kwa vyovyote vile JMT itabidi iingie katika OIC kwa kukidhi matakwa ya Zanzibar. Kwani JMT ni ya wote walio Bara na walio Zenj. Itabidi JMT itafute namna ya kukidhi matakwa ya wa-Zenj. Kinyume chake ni kuvunjwa kwa JMT yenyewe na kila mtu aende kivyake.
 
Ungekuwa uko kule kwetu Zenj. Ningesema mawazo haya ni kama ya wale (wanywa vinibu vya tende). Kumradhi Mheshimiwa - ulimi umeteleza.

Miye Zenj mbona kwangu, au jina la Pasco ndio limekuchanganya ukadhaniya miye machogo!. Ukimwona Ali Uki, Ali Abas, Mwantanga Ame au hata Farouk Karim, waulizie wakulete pale kwa Msukuma nyuma ya Masomo Bookshop utanipata. Sio siri siye Zenj tumeolewa tena ndoa iso talaka hata mke afanye vitimbi vipi haachiki. Mke Zenji aliwahi kutembea nje ya ndoa na mwanaume mmoja mwarabu aitwae OIC. Alikalishwa chini na kufungiwa ndani. Sasa mumewe ajiandaa kwa chuo cha pili, EAC. Uzuri wake Mke Zenj ataendeleza heshima ya kuwa mke mkubwa.
Sorry mod, leo nimeamkia vinibu vya tende pale Kibanda Maiti na saa hizi naelekea Mchambawima na ulimi haujatereza.
 
Jamani hapa tunabishania vitu ambavyo viko wazi kabisa, hivi zanzibar ni nchi kwa katiba gani ya zanzibar ambayo hakuna nchi hata moja ulimwenguni inaijua au kwa katiba ya JMT ambayo inatambulika kama nchi ulimwenguni.

Zanzibar itajiunga na OIC kwa kutumia katiba gani kama katiba yake inatmbulika tanzania tu, hata hao OIC wakiwaruhusu watakuwa hawajui sheria za kimataifa, kwani kwao zanzibar sio nchi unless waseme mkoa wa nchi unaruhusiwa kujiunga then zanzibar itaqualify kuwa mwanachama wao.

Kila siku watu wanrudia kitu kile kile zanzibar ni nchi mnapokuwa ndani ya tanzania mkivuka mipaka nyinyi sio nchi ni sawa na mkoa wowote wa tanzania ila mmekuwa mkipewa special treatment ambayo ndio mnayolingia sasa hivi otherwise hakuna cha tofauti na sehemu nyingine za tanzania
 
Hapana kituko hapo. Kwa vyovyote vile JMT itabidi iingie katika OIC kwa kukidhi matakwa ya Zanzibar. Kwani JMT ni ya wote walio Bara na walio Zenj. Itabidi JMT itafute namna ya kukidhi matakwa ya wa-Zenj. Kinyume chake ni kuvunjwa kwa JMT yenyewe na kila mtu aende kivyake.

Mh! Shughuli hapo ni pevu. JMT iingie OIC kwa Katiba gani? Labda katiba ibadilishe maana JMT ni nchi isiyo na dini.
 
Hivi wewe Mheshimiwa unataka kueleza nini. Matrekta Hamsini kwa Zanzibar is something else. Kuna majimbo Hamsini pale ya uchaguzi kila jimbo moja la uchaguzi litapata trekta lake. Jee? mangapi nyinyi mnapata msaada na kuyasambaza katika kila jimbo lenu la uchaguzi. Usibeze suala la misaada kwani Tanzania Bara ndiyo hiyo inakwenda kwa misaada tu. Unataka kuukataa ukweli hii leo?

Wewe sisi jimboni kwetu tulishaachanna na hayo mabo ya kutegemea serikali loong time..... Na kama ni matrekta yapo zadi ya 200 ya watu binafsi, zaidi ya hayo hamsini ya vikundi vya wakulima na ndio maana tunalishangaa hili!!!
 
Uvivu wa kufikiri na kufanya kazi ndiyo yanayotufanya kila wakati kuongelea kujiunga na OIC au zingine.Tufikirie namna ya kutumia rasilimali tulizonazo ili zitusaidie kwa maendeleo ya Nchi yetu.Tufanye kazi kwa bidii ili tuinue uchumi wa Nchi yetu.

Ndugu yangu nakuunga mkono asilimia 100, kisa chote cha kudai kujiunga na OIC ni kutaka mtelemko tuuu huu ndio udhaifu tulionao,tangui enzi za mwinyi wimbo wa OIC bado unaimbwa tu hivi kweli mpaka leo hatuwezi kurekebisha maeneo ya kiuchumi ambayo tumekwa mpaka tulilie misaada? mimi nafikiri changamoto tuliyonayo ni kuewaelimisha wazanzibari wavumile au wasahau suala la OIC na badala yake wachape kazi na kutengeneza fursa zaidi za vitega uchumi, pia suala la elimu linawagonga sana wasomi wao wengi wamekimbia nje ya zanzibar kutafuta kazi waliobaki ndio hao wanaccm wanamapinduzi feki. Mimi wasiwasi wangu ni kuvunjika kwa muungano au kuibuka kwa vikundi vitakavyodai kuwa vinatetea maslahi ya zanzibar kama vile wakina Nkunda wa DRC na wengine na kutekeleza mauaji, ambaye anawasiwasi na hili sawa lakini kumbuka kuwa hakuna situation ambayo ni ya kudumu.
 
Kama Zanzibar ni nchi au si Nchi hayo ni yenu huko bara ,ila wenyewe wanasema Zanzibar ni nchi mwenye wivu ajinyonge.
La pili naona mmetoka roho kwa matrekta 50 basi hayo ni kianzio zipo ahadi kibao ambazo Zanzibar imeahidiwa.
La Tatu mkuu wenu Kikwete juzi alijisifu kwa misaada waliyotoa watu wengine akisema serikali yake imeleta maendeleo basi hayo matrekta 50 yatampa tena mdomo mwengine wa kusifu maendeleo yanayoletwa na serikali yake.

Weka kando hilo maana naona hii topiki imechanganywa wakati kuna mambo mawili tofauti hapa. Niwaulize wanaJF hivi kama mnafahamu maendeleo nitawapa haya mambo ambayo ikiwa kati yenu kuna mtu alikuwepo Zanzibar kati ya kwenye mwaka wa 1980 hadi 1989 ataweza kuona tofauti .

Tuangalie Maendeleo yaliokuwepo Zanzibar natumai hata Tanganyika yalikuwepo maana nakumbuka lile bulga la saa nne kwa waliosoma Tanga wanaujua uji huo.

Tuangalie maendeleo yalikuwapo leo yako wapi??????

1. Tulikuwa na viwanda mbali mbali kama vile cha sukari, viatu, maziwa, sigara na viwanda vidogo vidogo lakini leo vyote leo haviko;

2. Tulikuwa na meli za kifahari kama vile MV. Mapinduzi, MV. Uhuru, MV. Ukombozi leo zimekuwa mzigo kwa Serikali na hutamani hata kupanda kwa girisi iliyojaa na wakati mwingi huwa hazifanyi kazi;

3. Skuli tulipokuwa tunasoma tulikuwa tunapewa vitabu mbali mbali vya kufanya marejeo nyumbani kama Modern Biology, Physics, Chemistry, Geography ...nk. Pia tulikuwa tunakaa kwenye desk kila Mwanafunzi lake lakini leo wengi wanakaa chini;

4. Skuli tulikuwa tunatumia vifaa vya maabara vipya kutoka Uingereza kama vile Bursen burner, test tube, beakers, measuring flasks ...nk lakini leo skuli nyingi hazina vifaa hivyo;

5. Hospitali ukipelekwa kwanza unapewa cheti lakini leo unaambiwa ukanunue buku nje utafikiri unakwenda kusoma. Pia baada kwisha kuonana na Daktari unakwenda kuchukua dawa ambazo zote huwepo bila matatizo lakini leo inabidi ukanunue nje kwa Utapoa;

6. Nyumba tuliokuwa tunakaa ilikuwa ukifungua maji basi lazima ukamate kikombe kwa uangalifu au kikombe hicho kinaweza kukutoka kwa pressure ya maji lakini leo tokea mwaka 1994 hadi leo hakuna maji yaliyotoka;

7. Rais wa Zanzibar alikuwa pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini leo hata cheo chake hatukijui ni kipi maana tumeambiwa kuwa si nchi. Sasa utakuwa Rais usiokuwa na nchi?

8. Wa-Zanzibari ilikuwa ni aibu kupita njiani kuomba lakini leo limekuwa jambo la kawaida kutokana na dhiki za maisha kutokana na dudu la TRA kutukaba rohoni.

Sasa nawauliza pamoja na huyu mmachinga wa Chalinze Mkwere Kikwete apime au ayaone hayo yaliopo hapo na kama anahitaji ushahidi awaulize CCM wenziwe waliopo Zanzibar kama hayo ni ya kweli au ni propaganda ? Je hayo ni maendeleo au si maendeleo ? Hayo ndio yanayohitajika ili Serikali na yeye Kikwete kama Kiongozi wa au Raisi wa Tanzania na Mwenyekiti wa AU basi ndio maendeleo ya kujisifia linganisha barabara na hayo hapo yepi ni muhimu ? Na hasa ilivyokuwa ya juu yote yamefanywa na serikali kama matunda ya mapinduzi ni hayo yaliopo juu na si haya maendeleo anayoyasifu mlinda mapinduzi mpya Mh.Kikwete ,ni lazima akae afikiri sana sio anakwenda Pemba na Unguja na kupandwa na jazba. WaZanzibari wanajua lipi bichi na lipi limeiva ,maendeleo ya Zanzibar chini ya awamu zote tatu za uongozi Tanzania ni sifuri,hivi Kikwete na kwenda kwake kote katika safari zake za utalii kutembea hajaona maendeleo ya Nchi nyingine au anakenua tu na kupiga miruzi anapoona vya watu vinang'ara.
Kikwete amewakosea adabu watu wa Zanzibar kwa kuwambia ni walevi wa tende kwani na kusema hakutapatikana uongozi unaotokana na ridhaa za wananchi huko ni kutokuheshimiana ,maana unaposema uongozi wa kuiongoza Zanzibar kwa upinzani itawachukua muda mrefu au usipatikane kabisa huko ni kuvuka mipaka ya utawala bora ukichanganya na demokrasia yake,ingawa huo uongozi bora haupo lakini inabidi ichomekewe hivyo hivyo. Kwenda kuwasifia watu tangi la maji wakati maji yenyewe hakuna huko ni kuwadharau na kuwafanya kama ni kuwadanganya watoto wadogo unaotaka kuwakimbia.
Zanzibar will prevail even under mkoloni mweusi.
 
Bwana Mwiba kuwakosea watu wa Zanzibar adabu ni kusema kuwa Mapinduzi hayana maana. Utu wetu upo hapo na kusema kweli Mapinduzi yametukomboa na wenetu. Sasa hao punguani kama wapo na wana tabia kama za wabugia vinibu- basi na wapashwe tu.
 
Miye Zenj mbona kwangu, au jina la Pasco ndio limekuchanganya ukadhaniya miye machogo!. Ukimwona Ali Uki, Ali Abas, Mwantanga Ame au hata Farouk Karim, waulizie wakulete pale kwa Msukuma nyuma ya Masomo Bookshop utanipata. Sio siri siye Zenj tumeolewa tena ndoa iso talaka hata mke afanye vitimbi vipi haachiki. Mke Zenji aliwahi kutembea nje ya ndoa na mwanaume mmoja mwarabu aitwae OIC. Alikalishwa chini na kufungiwa ndani. Sasa mumewe ajiandaa kwa chuo cha pili, EAC. Uzuri wake Mke Zenj ataendeleza heshima ya kuwa mke mkubwa.
Sorry mod, leo nimeamkia vinibu vya tende pale Kibanda Maiti na saa hizi naelekea Mchambawima na ulimi haujatereza.
Wewe Pasco waambie wenyeji wako wakupeleke Mwembe-mchomeke pale tende mjarabu. Lakini ununue Nusu yako ukae pembeni ukigida. na usikubali vi-ofa vya kinibu ukipokea hizo utaongea kama hao wanaosema eti Mapinduzi hayana maana. Msalimie Mwantanga. Lakini acha tabia ya kutaja majina ya watu hapa mtandaoni.
 
Ndugu yangu nakuunga mkono asilimia 100, kisa chote cha kudai kujiunga na OIC ni kutaka mtelemko tuuu huu ndio udhaifu tulionao,tangui enzi za mwinyi wimbo wa OIC bado unaimbwa tu hivi kweli mpaka leo hatuwezi kurekebisha maeneo ya kiuchumi ambayo tumekwa mpaka tulilie misaada? mimi nafikiri changamoto tuliyonayo ni kuewaelimisha wazanzibari wavumile au wasahau suala la OIC na badala yake wachape kazi na kutengeneza fursa zaidi za vitega uchumi, pia suala la elimu linawagonga sana wasomi wao wengi wamekimbia nje ya zanzibar kutafuta kazi waliobaki ndio hao wanaccm wanamapinduzi feki. Mimi wasiwasi wangu ni kuvunjika kwa muungano au kuibuka kwa vikundi vitakavyodai kuwa vinatetea maslahi ya zanzibar kama vile wakina Nkunda wa DRC na wengine na kutekeleza mauaji, ambaye anawasiwasi na hili sawa lakini kumbuka kuwa hakuna situation ambayo ni ya kudumu.
Wewe Bwana acha porojo zako hizo mbona huko Bara ndio mko mbele mnashadidia misaada. Sasa tukitafuta sisi unaleta nyimbo za kujitegemea. Anzeni nyinyi Bara. Au mnaona choyo pengine tunaweza kupata misaada zaidi ya nyinyi. - kivyetu vyetu.
 
Yaani Zanzibar haiwezi kujinunulia matrekta 50 mpake ipewe na OIC?

Tatizo siyo Zanzibar peke yake, hata bara mentality ya watu wengi ni kupenda vitu vya bwerere .... ask yourself, are we really poor or are we just short of cash?? ..... my answer to that is, most people are not short of cash, but poor ... which is a state of mind.
 
Wewe Pasco waambie wenyeji wako wakupeleke Mwembe-mchomeke pale tende mjarabu. Lakini ununue Nusu yako ukae pembeni ukigida. na usikubali vi-ofa vya kinibu ukipokea hizo utaongea kama hao wanaosema eti Mapinduzi hayana maana. Msalimie Mwantanga. Lakini acha tabia ya kutaja majina ya watu hapa mtandaoni.
Yakhe, ushauri wako nimepokea na nimekubali yaishe. Lengo la majina ni uthibitisho wa Uzanzibara wangu toka kwa Wazanzibari. Wote niliowataja hapo hukutania Komba wwakati Garage, kabla bado. Tanzania nchi yetu sote na Zanzibar pia yetu sote na wabara wote maana ni sehemu ya JMT. Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania.
 
Kulingana na hali ya kisiasa nchi nadhani hili litakuwa wazo zuri sana.. Ni bora sana Zenji ijiunge na OIC kivyake kwa sababu wananchi wake ndicho wanachokitaka.. haya maswala la trekta 50 sijui ngapi hayawezi kusaidia mgogoro wa OIC hata kidogo kwani hata sisi bara tumepewa vyandarua na Bush ktk kuzuia Maleria..Kwa mwenye kufikiria ule ulikuwa uchuro mkubwa!
Na kibaya zaidi hadi leo fungu kubwa la msaada aliotuahidi kutupa haukupitishwa na bunge lao hadi kaondoka madarakani...

Kimsingi mimi sioni sababu hasa kwanini Zanzibar isiruhusiwe kujiunga na OIC. Ni vema tukaangalia mahitaji ya wakati badala ya kufumba macho na kuziba masikio kana kwamba hatuoni ukweli kuwa wazanzibari wanahitaji kujishirikisha huko.
Labda nimalizie kwa kuuliza swali, je Tanzania itaathirika kwa kiasi gani endapo zanzibar itakuwa mwanachama wa OIC?
 
#
Nafikiri ni suali zuri tu hili. Waache OIC iishie Chumbe na Wa-Zenj waendelee na ndoto zao. Na mimi nauliza hivi Jee pale T/Bara watakapotaka kujiunga na sehemu fulani, na sisi tukaweka ngumu-wasiitumie JMT yetu kujiunga huko watajisikia vipi? Nikueleze wa-Zenj wanatabia ya ushindani - na hili Haki ya Mungu litawa-cost waBara - tusuburi.
 
Kimsingi mimi sioni sababu hasa kwanini Zanzibar isiruhusiwe kujiunga na OIC. Ni vema tukaangalia mahitaji ya wakati badala ya kufumba macho na kuziba masikio kana kwamba hatuoni ukweli kuwa wazanzibari wanahitaji kujishirikisha huko.
Labda nimalizie kwa kuuliza swali, je Tanzania itaathirika kwa kiasi gani endapo zanzibar itakuwa mwanachama wa OIC?

Si tu waachiwe wajiunge na OIC, wapewe uhuru wao kamili kama nchi inayojitegemea kwa kila kitu, nadhani tutakuwa tumepunguza matatizo mengi sana
 
Back
Top Bottom