Ofisi ya CHADEMA Morogoro Mjini yafurika waombolezaji wa kifo cha Mh. Regia Mtema

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Habari kutoka Morogoro zinaeleza kuwa "Watu mbalimbali wamefika ofisi za Chadema wilaya ya Morogoro mjini kutoa pole kutokana na msiba wa Mh. Regia Mtema, baadhi ya wakazi wa Morogoro walikuwa wakitoa michango ya rambirambi na wengine wakiulizia utaratibu wa usafiri wa kwenda Kilombero kuhudhuria mazishi.

Habari zimeendelea kudai kuwa Mh. Abood Aziz mbunge wa Morogoro mjini CCM amewaambia viongozi wa CHADEMA kuwa yuko tayari kutoa basi lake bure kusafirisha wanachama wa CHADEMA wataopenda kwenda kumzika marehemu Regia Mtema.

Habari zimeendelea kudai kuwa uamuzi wa mbunge huyo wa kujitolea basi uliibua mjadala mkubwa kwa wanachama wa CHADEMA kwani baadhi walionekana katakata kukataa msaaada huo kwa madai kuwa huenda ni mtego kwao wa kisiasa ili kuzima mashambulizi ya shutuma ambazo chama hicho kimekuwa kinatoa kwake kuwa amekuwa anatumia kutoa basi la kuzika wafu kila unapotokea msiba kama mtaji wa kisiasa badala ya kuibana serikali kuboresha huduma za afya ili kupunguza vifo".
 
Kwangu mimi sioni tatizo kuchukua huo mchango wa Abood kwenye huu msiba wa Taifa letu..kukataa msaada wa Abood sidhani kama itakuwa na maana maana unaweza ukakataa wa Abood ukachukua wa Lowasa au JK au Makinda nk.Tusikubali wana CHADEMA tukaingia kwenye mtego kuamini kuwa kifo cha REGIA ni hasara kwa chama tu au ni msiba wa chama tu.Tukubali kuwa Regia alikuwa mtu muhimu kwenye level ya Taifa pia,kwa hiyo tuwe radhi kupokea msaada au rambirambi kwa mtu yoyote atakayeguswa na tukio hili..

Nakukumbuka mum Regia!!!
 
weka picha ya watu tuone. halafu maswala ya mazishi huwa watanzania tunaondoa tofauti zetu za kichama, kidini na kikabila. Mia
 
weka picha ya watu tuone. halafu maswala ya mazishi huwa watanzania tunaondoa tofauti zetu za kichama, kidini na kikabila. Mia

hilo nalo neno tena sisi tulio mbali tupate uhakika kwamba hizi habari za kweli..
 
aina shida kuchukua mchango kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya mama yetu mpendwa hata ,mimi binafsi natoa gari yangu ndogo kwa ajili ya kwenda kwenye mazishi kilombero
 
Mimi binafsi sioni tatizo kwa aboud kutoa mchango wake ktk msiba wa kitaifa kama huu. In maana hawako tayari kupokea mchango kutoka vyama vingine? Jaribuni kuwa na uelewa kwa mambo ya msingi na msiwe na mawazo kama hayo muda wote. Yeye kasaidia wale wananchi ambao hawawezi kulipa kuja kwenye mazishi ya aliyekuwa mbunge wetu. Viongozi wa chadema pokeeni huo mchango wa aboud.
 
Hata mimi sioni tatizo kwa Abood kama kaamua kutoa basi lake,naamini wapo wana Morogoro wengi tu ambao hawana uwezo kwa sasa lakini wanatamani kwenda kumsindikiza mwana Morogoro mwenzetu,kipenzi chetu,dada yetu,mpigania haki za wote Regia E Mtema!kifupi mwenyewe najipanga kuanza safari jumanne kwenda Ifakara kumsindikiza dada yetu,ila kwa mwana jamvi mwenye kujua ni Ifakara sehemu gani dada yetu ndipo atakapo pumzishwa naomba anijuze mapema!Tunakushukuru Mungu Baba kwa maisha ya hapa duniani ya kipenzi chetu Regia,tunashukuru sana baba!tangulia dada yetu Regia!katuandalie makazi,tutaonana Paradiso
 
Watanzania pamoja na tofauti zetu kiitikadi, kiuchumi au kijamii tumekuwa na tutakuwa wamoja. Tuishinde mitego yote yenye nia mbaya kwa kutenda yaliyohaki mbele ya ya jamii yetu. Tuushinde ubaya kwa kutenda yaliyo mema. Abood katoa msaada kwa jamii na taasisi iliyo na itikadi tofauti na yeye, lakini Abood na hawa waliotofauti naye bado ni watanzania. Katika mambo yanayotuunganisha kama jamii moja ya kitanzania hatuwezi kutengana, moja ya mambo ambayo yameweza kutushirikisha pamoja katika nyakati mbalimbali ni pamoja na misiba.

Katika hili sidhani kama Abood amefanya jambo baya bali nadhani kafanya jambo jema kijamii na CDM wana wajibu kama taasisi kuheshimu jambo hili.
 
Mh! kwa hili wakuu tuangalie mazingira ya hyo michango kwani ni mazingira ya kifo,kwa hyo litakua jambo la ajabu sana kama Mh Abood au chama chake waje kujigamba juu ya hili baadae kwani waTz hatupo hivi kwenye masuala mazito kama haya kwa hyo nafikiri hakuna tatizo wao waupokee tu huo mchango as long as Mh Regia alikua anawakilisha hata mawazo ya wana CCM,R.I.P hon Mtema
 
Ninavyo wafahamu chadema, siamini kama ni kweli wamekataa rambirambi kutoka kwa Abood! Cdm ni chama makini na hakuna ubaguzi wa kiitikadi, kidini, kijamii. Ninawasiwasi na ukweli wa swala hili.
 
sijui itakuwaje jnne msafara ukiwa unapita pale morogoro...wanahitaji kuwa na mipango otherwise itakuwa kazi sana kudhibiti waombolezaji
 
kwa hilo la kutoa basi mbunge wangu namkubari huwa hana hiyana kwa kweli na hajaanza leo wala jana hata kabla ya ubunge alikuwa akifanya hivyo
nakupongeza Mh Mbunge,tuache siasa na tulitumie basi kusafirisha wachama kwenda kumzika Mh MBUNGE
 
Mimi nahisi hilo bus likubaliwe ila liende na magari mengine yaliyotolewa na Chadema au wanachadema ili kuonyesha uhitaji finyu!
 
chadema kila siku kinahubiri kujitegemea na kuondokana na hali ya kuwa ombaomba lazima kuonyesha mfano ktk hili
kuwa ktk mshikamano wenu kila kitu kinawezekana ikiwemo kukataa misaada ambayo nyie wenyewe mnaweza kuunganisha nguvu zenu na kufanya bila kuhitaji nguvu nyingine ambazo hamjui lengo lake ni nini? People's power is more than abood, in our unity we can do anything we put our mind on. kama vipi msaada huo augeuza monetary assistance to his consistuency ambao naamini wana shida kuliko CDM.
 
chadema kila siku kinahubiri kujitegemea na kuondokana na hali ya kuwa ombaomba lazima kuonyesha mfano ktk hili
kuwa ktk mshikamano wenu kila kitu kinawezekana ikiwemo kukataa misaada ambayo nyie wenyewe mnaweza kuunganisha nguvu zenu na kufanya bila kuhitaji nguvu nyingine ambazo hamjui lengo lake ni nini? People's power is more than abood, in our unity we can do anything we put our mind on. kama vipi msaada huo augeuza monetary assistance to his consistuency ambao naamini wana shida kuliko CDM.

lakini huu msiba si wa wanachedema pekeyao,huu msiba ni wa Taifa zima ndio maana hata ataagwa kitaifa kama mbunge na bunge likiwa ndio mhimili wa tatu umeamuwa iwe hivyo,lakini kumbuka kuwa Mh Abood ni mbunge so kutoa gari ni mchango wake kama mbunge mwenza na marehemu na ukumbuke kuwa Mh Regia alikuwa mbunge wa Kilombero mkoa wa moro ambako pia Mh Abood anatokea so hakuna mantiki ya kukataa michango

labda awe amekufa mwanachama wa CDM hapo hata mkikataa michangu mtajiju lakini kwa hli hatukubaliani nalo kabisaaaaa
 
wana moro wapenzi wa chadema kamwe hawawezi kubaliana na msaada wa abood, hii ni kwa sababu abood hupenda tumia loop holes kama hizi ili aweze pata imani kwa watu, kama anataka saidia atangaze safari ya bure kuelekea ifakara, wenye shida na huo usafiri wataenda upanda, awaache wana chadema na mipango yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom