Ofisi na Taasisi za Umma zimekuwa ni Taasisi za unyanyapaa Sana hasa kwa Watu wenye Ulemavu

Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
562
433
Kuna Jambo linauma Sana hasa kwenye Jamii zetu tunazoishi. Ofisi za Taasisi za Umma zimekuwa ni Taasisi za unyanyapaa Sana hasa kwa Watu wenye Ulemavu. Unakuta wewe mlemavu unakuja kutaka Huduma kwenye ofisi hizo unakuta kabla hujasalimia Mkuu wa Taasisi anakuambia leo sina Hela. Kabla hata hamjasalimiana.

Naomba niwaambie kitu kimoja nilichokutana nacho Mwaka 2017 pale CRDB BANK- MBINGA BRANCH Kwanza kabisa Mimi ni mlemavu natumia Baiskel ya matairi manne yaani Wheel Chair.
Ok let's Go!

Baada ya kumaliza Chuo nilikuwa natafuta sehemu ya Volunteer nikawa nimevutiwa na Bank ya CRDB iliyopo Mbinga Mjini. Nikaamua niende Pale kwa minajili ya Kujua vigezo na Mashart ya Kufanya Kazi Pale. Kama Nina vigezo Nijaribu kuomba. Kwani Imani yangu nilikuwa naamini Mimi Kama Mimi Siwezi kuipata Kazi Pale kutokana na nilivyo halafu Sina Mtu mkubwa wa kuniunganisha. Hii ni kwa Sababu Watu wengi wanaofanya Kazi kwenye Taasisi hizo wengi wana watu wao ambao ni wakubwa.

let's Go with our Story!
Baada ya kufika Pale akaja Mtu (Mmoja wa wafanyakazi) akaniuliza nahitaji Nini nikasema naomba nionane na meneja. Akanambia niingie Ndani hapo nilikuwa Nje tu, nikaingia ofisi ya meneja ipo kwa mbele Yaani anakuona kwani Kuna Vioo.

Meneja alituona akamtuma mfanyakazi Mmoja aje amuite yule Dogo aliyekuwa anani-support kwenye Baiskel yangu akaanza kumzukia "....…kwa nini umemleta huyu hapa Mimi leo Sina hela, Hawa wanakuja kuomba omba Hapa. Kwani mnakaa wapi? Dogo akasema Mtaa wa Misheni - Mbinga.

Yule Mama meneja wa Bank akaongea maneno makubwa na ya kufedhehesha.... Baadae akamwambia haya nenda kamchukue Mimi Sijui Nini ameongea. Dogo akanipeleka Pale Ofisi yeye akatoka. Mimi nipo mle Ndani nikaanza kwa salamu akaitikia vizuri nikamweleza Shida yangu, akanielekeza nmna ya Kufanya katika kuomba Kazi.....

Akanipa Address ya Human resource Management wa CRDB tukaagana vizuri nikatoka baadae nikaondoka. Nilipofika Nje barabarani Dogo kaanza kunieleza jinsi Yule MAMA (Meneja) Alivosema.

Hakika iliniuma Sana Sana na nikataka nirudi ili nimuulize na nimwelekeze jinsi Maisha yanaovyoenda. Ulemavu sio ugonjwa Bali ni Hali ya Mtu yeyote anawez akawa. Na Wala Sio umaskini Kama wanavodhani Wewe Meneja, Mkuu wa shirika Fulani unaweza ukawa mlemavu at any time....

Unaenda kwa lengo lingine Mtu akudakie juu juu sina Hela what does it mean?

MKASA MWINGINE
Mwaka Jana Niliingia pale VODA-SHOP MBINGA kwa lengo la Kusajili Simu yangu kwa Alama za Vidole ile naingia tu
Jamaa kabla sijaeleza Nini nataka akadakia LEO SINA KITU Ndugu yangu.... Nilishangaa Sana jamaa anasemaje leo Hana kitu! Nikamuuliza Tena unasemaje! kwa ukali kidogo.,.. Akasema leo Sina Hela.... ila huyo Naomba anasamehe nilimtukana Sana mpaka aliomba msamaha kwa kukurupuka yule mwamba nilimsamehe nikasajili Laini yangu nikasepa zangu ila Kweli nilimtukana Sana.

Kwa Sababu nilikuwa na Hasira Sana Yani
Sisi walemavu tunapitia Changamoto Nyingi Sana Sana. Mpaka kuja ku- succeed Hakika tunakuwa hoi.

Hata Kama una Elimu ile %3 Haitekelezwi
NITAKUJA KUSHEA KITU KINGINE KUTUHUSU.
ASANTENI SANA
 
Kuna Jambo linauma Sana hasa kwenye Jamii zetu tunazoishi. Ofisi za Taasisi za Umma zimekuwa ni Taasisi za unyanyapaa Sana hasa kwa Watu wenye Ulemavu. Unakuta wewe mlemavu unakuja kutaka Huduma kwenye ofisi hizo unakuta kabla hujasalimia Mkuu wa Taasisi anakuambia leo sina Hela. Kabla hata hamjasalimiana.
Naomba niwaambie kitu kimoja nilichokutana nacho Mwaka 2017 pale CRDB BANK- MBINGA BRANCH Kwanza kabisa Mimi ni mlemavu natumia Baiskel ya matairi manne yaani Wheel Chair.
Ok let's Go!
Baada ya kumaliza Chuo nilikuwa natafuta sehemu ya Volunteer nikawa nimevutiwa na Bank ya CRDB iliyopo Mbinga Mjini. Nikaamua niende Pale kwa minajili ya Kujua vigezo na Mashart ya Kufanya Kazi Pale. Kama Nina vigezo Nijaribu kuomba. Kwani Imani yangu nilikuwa naamini Mimi Kama Mimi Siwezi kuipata Kazi Pale kutokana na nilivyo halafu Sina Mtu mkubwa wa kuniunganisha. Hii ni kwa Sababu Watu wengi wanaofanya Kazi kwenye Taasisi hizo wengi wana watu wao ambao ni wakubwa.
let's Go with our Story!
Baada ya kufika Pale akaja Mtu (Mmoja wa wafanyakazi) akaniuliza nahitaji Nini nikasema naomba nionane na meneja. Akanambia niingie Ndani hapo nilikuwa Nje tu, nikaingia ofisi ya meneja ipo kwa mbele Yaani anakuona kwani Kuna Vioo tupu.
Meneja alituona akamtuma mfanyakazi Mmoja aje amuite yule Dogo aliyekuwa anani-support kwenye Baiskel yangu akaanza kumzukia kwa nini umemleta huyu hapa Mimi leo Sina hela, Hawa wanakuja kuomba omba Hapa. Kwani mnakaa wapi? Dogo akasema Mtaa wa Misheni - Mbinga. Yule Mama meneja wa Bank akaongea maneno makubwa na ya kufedhehesha.... Baadae akamwambia haya nenda kamchukue Mimi Sijui Nini ameongea. Dogo akanipeleka Pale Ofisi yeye akatoka. Mimi nipo mle Ndani nikaanza kwa salamu akaitikia vizuri nikamweleza Shida yangu, akanielekeza nmna ya Kufanya katika kuomba Kazi..... Akanipa Address ya Huma resource Management wa CARD tukaagana vizuri nikatoka baadae nikaondoka. Nilipofika Nje barabarani Dogo kaanza kunieleza jinsi Yule MAMA (Meneja) Alivosema.
Hakika iliniuma Sana Sana na nikataka nirudi ili nimuulize na nimwelekeze jinsi Maisha yanaovyoenda. Ulemavu sio ugonjwa Bali ni Hali ya Mtu yeyote anawez akawa. Na Wala Sio umaskini Kama wanavodhani Wewe Meneja, Mkuu wa shirika Fulani unaweza ukawa mlemavu at any time.... Mtu akaudakie juu juu sina Hela what does it mean?

MKASA MWINGINE
Mwaka Jana Niliingia pale VODA-SHOP MBINGA kwa lengo la Kusajili Simu yangu kwa Alama za Vidole ile naingia tu
Jamaa kabla sijaeleza Nini nataka akadakia LEO SINA KITU Ndugu yangu.... Nilishangaa Sana jamaa anasemaje leo Hana kitu! Nikamuuliza Tena unasemaje! kwa ukali kidogo.,.. Akasema leo Sina Hela.... ila huyo Naomba anasamehe nilimtukana Sana mpaka aliomba msamaha kwa kukurupuka yule mwamba nilimsamehe nikasajili Laini yangu nikasepa zangu ila Kweli nilimtukana Sana.
Kwa Sababu nilikuwa na Hasira Sana Yani
Sisi walemavu tunapitia Changamoto Nyingi Sana Sana. Mpaka kuja ku- succeed Hakika tunakuwa hoi.
Hata Kama una Elimu ile %3 Haitekelezwi
NITAKUJA KUSHEA KITU KINGINE KUTUHUSU.
ASANTENI SANA
Pole kwa changamoto Mkuu.

Sasa avatar yenye chama cha mbogamboga ya nini ?
 
Kama bado huna kazi njoo ofisi za CCM makao makuu Dodoma kuna vijana walipewa ukuu wa wilaya na Udas nafasi zao bado hazijazibwa.

Wasiliana na Polepole au Mpogolo.
 
Tanzania Tuna Safari Ndefu Sana
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Sasa Hivi Watu Wanawaza Tofauti Mno
Wakitazama Mtu Wanahukumu Bila Kujua Ukweli
Hasa wakibahatika kupata Nafasi ya Ajira na kuwa Katika ofisi Fulani wanajiona wamefiika
 
Kama bado huna kazi njoo ofisi za CCM makao makuu Dodoma kuna vijana walipewa ukuu wa wilaya na Udas nafasi zao bado hazijazibwa.

Wasiliana na Polepole au Mpogolo.
Bado Kazi ngumu Mkuu,kwenda kuomba Kazi kwenye hizo office ni Changamoto. Kama nilivosema wanavotuchukulia hata kabla hatujasema neno. Pia ni tunaogopa Sana.
Nitajaribu kuwasiliana na Mheshimiwa polepole au Mpogolo wanaweza nisaidia maybe
 
Watakupa kazi ondoa hofu.
 
Hasa wakibahatika kupata Nafasi ya Ajira na kuwa Katika ofisi Fulani wanajiona wamefiika
Yaani Hao Wenye Aina Hiyo Ni Wengi Sana
Unakumbuka Wengine WalikuwA Wanasema Vijana Wavivu
Hamtaki Kujiajiri Lakini Mwenyewe Anayesema Kaajiriwa Na Serikali
 
Back
Top Bottom