DOKEZO Ocean Road Cancer Institute acheni ukatili, tumelipia dawa halafu tunaambiwa eti kiwanda kinachotoa dawa kimesitisha kuzalisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

moonlightj12

Member
Dec 6, 2022
33
90
Kwa huzuni sana Hawa watu hawana huruma yaani ni wakatili mno.

Kweli tumelipia dawa miezi yote hii halafu tunaambiwa eti kiwanda kinachotoa dawa kimesitisha kuzalisha nyie watu nyie muogopeni Mungu.

Dear mama Samia sijui kama unapitiaga social media ila kama unapitia tunaomba tusaidie mama.

Tumelipa pesa nyingi lakini dawa hatupewi na ni miezi Sasa inapita.

Tunajinyima hata kula kuwatibu wazee wetu afu wao wanachukulia masihala.

Naombeni watu wa JF tusaidieni kuwahoji hao madaktari yaani kiwanda kisitishe utoaji dawa kwamba hamna kingine? Aisee inaumiza.
 
Poleni sana hospital za TZ ni kama zipo near jehanam ...nimemuuguza baba mdogo hadi anafariki hospital zote kubwa za tz nayajua maumivu hayo. Badoo tuna safari ndefu sana.
 
Hospitali sikuhizi ni sehemu ya biashara hakuna tiba tena, tulinde na kujali afya zetu.

Juzi niliona hospitali fulani inashehereke wiki ya huduma kwa wateja wakaenda mbali mpaka na kukata keki yenye sukari na kuwapa wagonjwa waliolazwa.

Nilishtuka sana.
 
Kwa uzuni sana Hawa watu hawana huruma yaani ni wakatili mno

Kweli tumelipia dawa miezi yote hii afu tunaambiwa eti kiwanda kinachotoa dawa kimesitisha kuzalisha nyie watu nyie muogopeni Mungu

Dear mama Samia sijui kama unapitiaga social media ila kama unapitia tunaomba tusaidie mama

Tumelipa pesa nyingi lakini dawa hatupewi na ni miezi Sasa inapita

Tunajinyima ata kula kuwatibu wazee wetu afu wao wanachukulia masihala

Naombeni watu wa jf tusaidien kuwahoji hao madaktar yaani kiwanda kisitishe utoaji dawa kwamba hamna kingine? Aisee inaumiza
Hii Habari ingekuwa kamili kama ungeweka na majina ya Dawa.

Anti cancer drugs ni kipengele sana mkuu.
 
Kwa uzuni sana Hawa watu hawana huruma yaani ni wakatili mno

Kweli tumelipia dawa miezi yote hii afu tunaambiwa eti kiwanda kinachotoa dawa kimesitisha kuzalisha nyie watu nyie muogopeni Mungu

Dear mama Samia sijui kama unapitiaga social media ila kama unapitia tunaomba tusaidie mama

Tumelipa pesa nyingi lakini dawa hatupewi na ni miezi Sasa inapita

Tunajinyima ata kula kuwatibu wazee wetu afu wao wanachukulia masihala

Naombeni watu wa jf tusaidien kuwahoji hao madaktar yaani kiwanda kisitishe utoaji dawa kwamba hamna kingine? Aisee inaumiza
Lah!
lightjl
Pole sana mkuu 'moonlightjl',

Mada yako mtu akiisoma ambaye majanga ya aina hii hayajampata, atadhani huu ni ulalamishi usiokuwa na msingi wowote. Na hasa inapoonekana sasa, ulalamishi juu ya kila jambo ni kama jadi ya waTanzania.
Huwezi kukosa kusikia malalamiko, juu ya umeme, maji, ufisadi na mambo mengi mengine.

Sasa kwenye jambo kama hili lako, inasikitisha sana kama mmestukiziwa tu, kwamba dawa mlizozoea kuzitumia hazipo tena, kutokana na matatizo ya kiwanda?
Kwani madaktari wenu, angalau hawakuwapa taarifa mapema kuhusu tatizo hilo, ili kuwaandaa na mabadiliko ya dawa? Hakuna dawa mbadala wa hizo mlizozoea ambazo sasa mnaweza kuzitumia?

Nyinyi mmeambiwa tu, kuwa kiwanda kimesitisha, na hamkupewa ushauri zaidi ya hapo?

Lakini, pamoja na kukupa pole na mkasa huu, nashangaa sana kwako kuanza tena kumlilia Rais. Huyo Rais afanye nini? Watu wa aina yako ndipo panapoanzia matatizo yetu sote. Mnafanya kana kwamba uhai wenu na kila kitu kinachowahusu ni huyo huyo Rais wenu ndiye atamaliza kila shida zenu?
Je, na kama matatizo ya aina hii yanaanzia kwake, bado mnamlilia yeye kama mungu wenu?

Akili ya namna hii imekuwa ni akili ya kipumbavu sana ndani ya nchi hii. Ni kana kwamba hakuna chochote kinachoweza kufanyika bila ya huyo mnayemlilia kwa kila jambo, isipokuwa hamjui kuwa ubovu unaanzia kwake!
 
Kweli tumelipia dawa miezi yote hii afu tunaambiwa eti kiwanda kinachotoa dawa kimesitisha kuzalisha nyie watu nyie muogopeni Mungu

Dear mama Samia sijui kama unapitiaga social media ila kama unapitia tunaomba tusaidie mama
"Kiwanda kusitisha kuzalisha dawa", kwa sababu mbalimbali siyo jambo la kipekee sana.

Kiachokosekana hapa ni mawasiliano 'communication', kati yenu (wagonjwa), na wahudumu wanaowapa huduma. Hapa sioni ni kwa nini pawepo na tatizo.

Siamini pia, kwamba hizo pesa mlizotakiwa kulipia ili mpate dawa, kwamba zimeliwa, pamoja na kuwepo ukosefu wa ubinaadam miongoni mwetu kwenye nyakati hizi.
Kinachotakiwa, ni kwenu, badala ya kulalama kiasi hiki, tafuteni taarifa sahihi toka kwa wahudumu wenu.
Wagonjwa hawaachi kuhudumiwa, kwa vile tu, dawa aina moja imeacha kutengenezwa. Karibu kila dawa kuna mbadala wake, hata kama haziwezi kuwa sawasawa kwa kila hali.

Achana na hiyo akili ya kukimbilia kwa Rais, hana msaada huyo; jitahidi kufanikisha matibabu ya mgonjwa wako kwa kushirikiana na hao wanaompa huduma.

Na usianze kulalama kwamba sijui matatizo ya hospitali zetu. Ninayajua sana. Badala ya kwenda kwa huyo Rais, kwa nini usijihusishe na utawala wa hospitali husika, kwenye ngazi mbalimbali za uongozi, ili angalau upate taarifa sahihi kuhusu hatma ya matibabu ya mgonjwa wako.
 
Back
Top Bottom