Gudboy
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 867
- 77
Julius Samwel Magodi
RAIS Barack Obama wa Marekani, wiki hii alifanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika, waliokuwa wakihudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, aliwapasulia jibu linalowasumbua viongozi hao kwamba hakuna uwekezaji mzuri katika nchi inayokumbatia ufisadi.
Aliwataka viongozi hao akiwamo Rais Jakaya Kikwete, ambaye alihudhuria hafla hiyo kuondoa ufisadi katika nchi zao ndipo watakapoona manufaa ya uwekezaji.
Alisema mazingira yaliyopo sasa ni kuwa, uwekezaji umeshindwa kuzinufaisha nchi za kiafrika, kutokana na rushwa kutumika kuingiza wawekezaji feki.
Kwa hakika maneno haya ya Obama nilipoyasikia yalinikuna sana, nadhani Rais Kikwete alishtuka sana aliposikia kauli hiyo. Nasema atakuwa alishtuka kutokana na ukweli kwamba onyo hilo lilikuwa likiilenga serikali ya Tanzania.
Ingawa hakuwa akimanisha Tanzania pekee, lakini Obama kama vile mtabiri, kila alichokuwa akikizungumza kilikuwa kikiihusu serikali ya Kikwete.
Hakuna mtu asiyejua kwamba Tanzania sasa, imegeuzwa kuwa shamba la bibi na wawekezaji kutoka nje, ambao wamekuwa wakiingia nchini kuchuma na kuondoka na utajiri mkubwa.
Kuna wakati fulani mwekezaji mmoja kutoka nje aliwahi kusema kwamba,Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo unaweza kuingia na kuwekeza ukiwa huna kitu, halafu ukatoka ukiwa miongoni mwa matajiri wakubwa duniani.
Obama alitukumbusha watanzania matatizo makubwa ya mikataba feki ya uwekezaji, ambayo sasa inatutesa na kutufanya tubaki watumwa katika nchi yetu.
Hotuba ya Obama itakuwa ilimkumbusha Rais Kikwete, uwekezaji mbaya ambao mpaka sasa umetutesa, kutokana na maafisa wa serikali kushirikiana na wawekezaji kuiibia nchi.
Mikataba hii ni ile ya Kampuni ya Rites na Shirika la Reli Tanzania (TRC), mikataba ya migodi ya madini, jinsi ambavyo wawekezaji wanachukua madini na kutuachia mashimo. Mgodi wa Mkaa ya mawe ya Kiwira, Richmond, TICTS na mingine mingi.
Hata hivyo Rais Kikwete ambaye kabla ya kuondoka kwenda Marekani, alikaririwa akisisitiza hakuna uchumi wa nchi yoyote duniani unaoweza kukua kwa uwekezaji wa serikali peke yake, bila wawekezaji binafsi.
Aliwataka maofisa wa serikali yake, kuchukua maamuzi ya haraka kutimiza mahitaji ya wawekezaji, mara zinapojitokeza nafasi za wawekezaji kutaka kuja nchini na sio kuwazuia.
Kwa hakika, kama Rais Kikwete anasema uwekezaji ndio njia muhimu ya kuleta maendeleo kwa wananchi, bila ya kutoa onyo kwa watendaji wake wa serikali, kuhusu kuingia mikataba feki ambayo imeipotezea nchi mabilioni ya shilingi, bado tuna matatizo makubwa.
Ni kweli kuwa maendeleo yanaweza kuchangiwa na wawekezaji wa nje. kwa vile wataingiza teknolojia mpya, kupanua ajira na kuongeza mapato ya nchi. Lakini kwa uwekezaji tuliona hapa nchini, wawekezaji kugeuka kuwa milija ya kunyonyea raslimali zetu, bado hawawezi kuwa ni suluhu ya matatizo yetu.
Kitu kibaya ambacho kimejengeka kwa viongozi wetu, ni kuugeuza uwekezaji kuwa miradi yao ya kujipatia utajiri na pengine kutafuatia fedha za CCM, kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Hii ni hatari sana kwa ustawi wa nchi, viongozi wetu wanachekelea kuendelea kuwepo kwa udhaifu wa sheria ya mikataba ya uwekezaji wakijua kwamba, wataendelea kujinufaisha wao au kundi lao.
Leo hii kila mwekezaji ambaye tumeingia naye mikataba feki, nyuma yake yupo kigogo wa serikali au aliyekuwepo katika uongozi wa serikali zilizopita.
Kwa mahesabu ya haraka haraka, mpaka sasa fedha ambazo zinadaiwa kukombwa serikalini kwa njia ya ufisadi, ama kupitia mikataba feki ya uwekezaji na wizi mwingine, ni zaidi ya shilingi trilioni moja, ambazo ni sawa na bajeti za wizara sita kubwa.
Kama viongozi wetu wangekuwa makini ambao hawana ubinafsi, wanaopenda nchi yao, leo fedha hizo zingekuwa ziko salama, zingeweza kujengea barabara na hospitali karibu nchi nzima na hivyo wanachi wakapata maisha bora, kama Rais Kikwete alivyoahidi wakati akiingia madarakani.
Hii ndio Tanzania yetu ambayo inatajwa kuwa moja ya nchi maskini kabisa duniani, ambayo inakosa uongozi madhubuti wa kulinda maliasili zake.
Mwandishi mashuhuri duniani Robin Sharma katika kitabu chake cha 'lead without title' anasema, "kila mtu anaweza kuonyesha tabia za kuwa kiongozi, lakini hiyo haimaanishi kuwa kila mtu anaweza kuwa kiongozi."
Tatizo letu hapa ni kwamba tunao viongozi wengi hususani maafisa waandamaizi na wanasiasa lakini hawana sifa za uongozi kutokana na kujiingiza katika kuifilisi nchi badala ya kulinda rasilimali zetu.
Tatizo tulinalo si wawekezaji, ni sisi wenyewe tunaowaruhusu hao wawekezaji kuchukua faida kubwa katika huo uwekezaji, kwa mikataba feki isiyo na manufaa kwa nchi. Kinachofanyika hapa nchini, ni uporaji wa mali ambao umebarikiwa na viongozi wetu.
Kinachotakiwa sasa tuwe na mapinduzi ya fikra, tutumie uchaguzi ujao kuchagua viongozi ambao wataiongoza nchi, kutufikisha katika nchi ya asali na maziwa badala ya kutupeleka na kutuacha jangwani.
Mwandishi wa safu hii anapatikana kupitia baruapepe; juliusmagodi@yahoo.com
Simu; 0754 304336
source: mwananchi