Nyumba ndogo

Jan 4, 2012
61
23
Kwa wale wapenzi wa Nyumba Ndogo angalia Shairi hili:


Nyumba ndogo si fahari,si pendo ulimbukaji,
Pendo lisilo nadhari, daima unyatiaji,
Mara nyingi ni kaburi, la kufukia mitaji,
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.

Sababu ya nyumba ndogo, sisaliti Ndoa yangu,
Mke simpi kisogo, nikenda jivisha pingu,
Katu siwanii kago, kwa mwendo wa vanguvangu,
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.

Ina pendo la mizungu, na mzo mzo hadaa,
Kusudi ugawe fungu, wana washinde na njaa,
Ndipo hapo Mcha Mungu, sishiriki nakataa!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.

Asonazo hupumbaa, kwa zile stihizai,
Akawa kama kichaa, kwa penzi la ulaghai,
Kwake huona kinyaa, japo sekunde hakai!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.

Tatizo jitumbukize, kumuoa kwa papara,
Mkeo umfukuze, yeye atwae kitara,
Atakuja akulize, ukabaki na izara!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo

Zamani alikubeba, kama mwana mbelekoni,
Kukuganda kama ruba,ukadhani umewini,
Uchao sasa adhaba, na ya kale huyaoni!
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.

Kaditama kina baba, tangu leo jifunzeni,
Ya nje sio mahaba, na hilo jiepusheni,
Tuyakidhi matilaba, ya familia nyumbani,
Sisaliti Ndoa yangu, sababu ya nyumba ndogo.

Lambert F. Chialo (Mhadhiri wa Malenga)
Magogoni, Dar es Salaam
0713961860
 
shairi zuri!!Bora uwaambieee wanaume wenzio watulie na wake zao!! Lakni cjui ka wataelewa somo hilo mana wengne weshaleweshwa, ngoja waje!!
 
wewe mshairi kaa ukijua sasa hivi ni mwendo wa wawili akiwemo na kiunganishi mfano!
1.ugali/wali na mboga halafu moto ndo kiunganishi!
2.mwalimu na mwanafunzi halafu jengo la darasa ndo kiunganishi!
3.mlevi na pombe halafu kilabu/bar ndo kiunganishi!
4.muumini na mungu halafu biblia/kuraan ndo kiunganishi!
5.nyumba kubwa na nyumba ndogo halafu na mimi ndo kiunganishi!
umenipata hapo!!!
 
pamoja na mashairi yote hayo keep in mind nyumba ndogo ndo tunawanyoshea hao wake zenu!!!!
 
wewe mshairi kaa ukijua sasa hivi ni mwendo wa wawili akiwemo na kiunganishi mfano!
1.ugali/wali na mboga moto ndo kiunganishi!
2.mwalimu na mwanafunzi jengo la darasa ndo kiunganishi!
3.mlevi na pombe kilabu/bar ndo kiunganishi!
4.muumini na mungu biblia/kuraan ndo kiunganishi!
5.nyumba kubwa na nyumba ndogo na mimi ndo kiunganishi!
umenipata hapo!!!

hiyo namba 5 unatukwaza tuliolewa. mi nakuunganishaje na nyumba ndogo? shindwaaaaaaaaaaaa!
 
smol+hausicopy.jpg
 
hahha,kuna jamaa kafanyiziwa na small house,kashtukia analetewa kadi ya sendoff,small house kumbe inaolewa,jamaa alikuwa anahonga kinyama.Kadata kaachwa kwenye mataa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom