Nyumba inauzwa Ununio Beach

Mkuu mbn una hasira sana? Biashara haitaki hasira hata kidogo hao unaowaona sio serious buyers ndio buyers wenyewe mtu anayetaka kununua kitu kwako lazima akuchallange nimeshawahi kuuza gari yangu aina ya prado humu humu jf walikuwa wananiita mimi ni dalali but at the end of the day yule niliyemuuzia alikubali ile gari ilikuwa ni yangu baada ya kumkabidhi kadi ya gari yenye jina langu,sasa wewe
unakuwa mkali huku unataka hao hao wanunue hiyo
nyumba yako, mkuu biashara huwa haiendi hivyo coz hapa
jf watu wana maudhi balaa lakini ndio wanunuzi
hao!
Sina hasira tatizo ni kureveal my identity. The moment I put the picture hapa my identity will be out there. Bado nahitaji kuhide identity yangu kuweza kutoa maoni yangu kuhusu mustakabali wa taifa letu. That is my only problem bro
 
Sina hasira tatizo ni kureveal my identity. The moment I put the picture hapa my identity will be out there. Bado nahitaji kuhide identity yangu kuweza kutoa maoni yangu kuhusu mustakabali wa taifa letu. That is my only problem bro
Unatutatanisha mkuu. Unataka kuuza kitu chako halafu unaogopa? Au hiyo nyumba ina mgogoro?
 
hivi mkuu ununio unayo iseme ni ile ya tegeta unaenda bunju au ipo nyingine?mi hiyo ununio ndo naifahamu ambayo ina bandali bubu ya kuvushia magendo kwenda zanzibar.au ipo nyingine?ambayo ina viwanja ambavyo havijaendelezwa?mimi sioni unaogopa nini.hata ukisema iwe siri mwisho utajulikana tu.unafikiri nani utamuuzia nyumba kwa maficho?utatufuata viongozi wa sehemu husika na majirani zako tu so huna pakutukwepea usijulikane.
 
hivi mkuu ununio unayo iseme ni ile ya tegeta unaenda bunju au ipo nyingine?mi hiyo ununio ndo naifahamu ambayo ina bandali bubu ya kuvushia magendo kwenda zanzibar.au ipo nyingine?ambayo ina viwanja ambavyo havijaendelezwa?mimi sioni unaogopa nini.hata ukisema iwe siri mwisho utajulikana tu.unafikiri nani utamuuzia nyumba kwa maficho?utatufuata viongozi wa sehemu husika na majirani zako tu so huna pakutukwepea usijulikane.

Ununio ninayoisema ndio hiyo, sisemei kwenye bandari, na sina taarifa za hiyo bandari kuvusha magendo, seems news to me, najua tu kwenda kununua samaki kule wa mnada! Kwa taarifa tu eneo la Ununio ni kubwa sana na kama hujafika siku za karibuni, is one of the nice place kwa sasa, pamejengeka sana na ni maeneo mazuri ya kuishi, na most people wanaoishi kule ni young graduates ambao wengi ni middle class people, lots of kids etc. Nyumba yangu iko mbali kiasi toka ufukweni, maeneo yote ni surveyed na yana certificate of occupancy/Tittle. Kufika kule kuna njia tofauti, unaweza kupitia Kunduchi mtongani kule kweney mabwawa ya chumvi, infact ile barabara inajengwa kwa kiwango cha lami, au ukapitia tegeta-- Basihaya (Bus Hire). Umbali toka mjini hadi Ununio ni kilomita 28

Labda niclarify kuhusu identity. Watu wengi humu JF tunajitambulisha kwa majina sio yetu halisia, lengo ni kuficha tu identity yetu na kutupa uhuru mpana wa kusema kile kilichopo katika mawazo yetu pasipo kuogopa kujulikana, ndio maana kuna kina Malaria Sugu, Mwanakijiji, Nyani Ngoba, Ichondi, "Dubu" etc. Nyumba inaweza kumdentify mtu kirahisi, the moment mtu unaona picha ya nyumba, na anamjua mwenye nyumba ni nani, unasema oh, hii si nyumba ya mtu fulani, lets say Kibuli, (i am just making name here) oh kumbe Kibuli ndio anajiita "Ichondi" Then Ichondi anakuwa ameshajulikana ni nani. Haya ndio mawazo yangu, yumkini ninakosea but I am pretty sure kuna watu hapa JF wataijua hiyo nyumba na mwenye nayo the moment wakiona picha

Ni jambo la kawaida kwa muuzaji kuamua kutokuweka picha ya nyumba anayouza, only mtu akitaka picha anarequest. Kama kuna mtu anataka picha, send the text to the number iliyoonyeshwa hapo juu na urequest picha, na uspecify mode ya kutumiwa hizo picha, I will do that. Hili ni jambo la kawaida, kwa wale wanaoshop ebay etc kwa nchi za nje, sometimes picha is available on request. Hata magari ya Japan, sometimes picha is available on request. Sio kitu ambacho si cha kawaida, na mimi nimeona nifanye hivyo, kama kuna yeyote anayetaka kuona picha, send your request and the pictures will be sent to you directly.
 
Identity haiusiani na Biashara!!
Anaweza ku-hide identity kwa ajili ya sababu zingine kabisa mainly ziwe michango yake kisiasa humu jamvini, na kuuza iwe issue nyingine kabisa.
Ununio ni eneo zuri sana, viwanja vyake sio vya serikali hivyo watu wanaishi kama kwenye hekalu flani hivi yenye eneo kubwa tu (sifahamu ya huyu bwana ikoje),
Omary Mahita ana eneo lake kubwa na kalijenga vizuri tu pamoja na viongozi wengine wengi tu.
Bandari bubu kweli ipo maeneo yale, but sidhani kama inahusiana na mambo ya Nyumba!!.
Tatizo kubwa la yale maeneo ni moshi utokao Kiwandani Wazo Hill kuathiri makazi ya watu (sina uhakika na watu wenyewe pia kama wanaathirika na huo moshi), kwani nyumba ikikaa muda tu utaiona kuta na paa linaanza kubadilika rangi.
(Na-declare Nimesoma Ununio Isamic)
 
Kwa nini dalali hatakiwi? Mimi nadhani dalali anaweza kuwa msaada wa kukuuzia hiyo nyumba kwa haraka zaidi kuliko wewe kuiuza kivyakovyako. Binafsi nina kampuni ya udalali na baadhi ya kazi zangu unaweza kuziona katika kitomai.blogspot.com. Binafsi nina mteja mkononi mwenye budget hiyo lakini kwa sababu umeshaweka kizuizi ina kuwa haiwezekani. Nadhani pengine kutomtaka dalali inaweza kuwa dalili ya kutojiamini japokuwa siyo lazima. Mimi ninatoa ushauri watu kununua mali kupitia kwa dalali hasa aliyejisajili.Dalali mzoefu anao uwezo wa kung'amua kwa haraka uongo wa mtu anayedai kuuza mali au kupangisha ili hali mali hiyo si yake. Dalali mchanga au mtu wa kawaida ni rahisi sana kuingia katika mtego wa kitapeli. Anyway kabla sijaenda mbali sana ningependa kujua toka kwako kwa nini unasema dalali hatakiwi.
 
Kuwa na dalali ni jambo jema,ni jambo la muhimu, ni jambo la lazima. Fumbua macho ulione hilo itakusadia. Kuuza property ya bei hiyo peke yako peke yako siyo jambo lelemama. Ulizia waliowai kuuza property za bei hiyo wakwambie shughuli yake ikoje. Shughuli yake sawa na ile ya simba 10 kumuangusha nyati mmoja si mchezo.kuna kuwa na hekaheka kubwa sana.
 
Kwa nini dalali hatakiwi? Mimi nadhani dalali anaweza kuwa msaada wa kukuuzia hiyo nyumba kwa haraka zaidi kuliko wewe kuiuza kivyakovyako. Binafsi nina kampuni ya udalali na baadhi ya kazi zangu unaweza kuziona katika kitomai.blogspot.com. Binafsi nina mteja mkononi mwenye budget hiyo lakini kwa sababu
umeshaweka kizuizi ina kuwa haiwezekani. Nadhani
pengine kutomtaka dalali inaweza kuwa dalili ya kutojiamini
japokuwa siyo lazima. Mimi ninatoa ushauri watu kununua
mali kupitia kwa dalali hasa aliyejisajili.Dalali mzoefu anao
uwezo wa kung'amua kwa haraka uongo wa mtu anayedai
kuuza mali au kupangisha ili hali mali hiyo si yake. Dalali
mchanga au mtu wa kawaida ni rahisi sana kuingia katika
mtego wa kitapeli. Anyway kabla sijaenda mbali sana
ningependa kujua toka kwako kwa nini unasema dalali
hatakiwi.
Ndugu yangu kama wewe ni dalali mzoefu utakubaliana nami kuwa kuna pande mbili katika ununuzi wa nyumba. Kuna muuzaji na kuna mnunuzi. Nimeamua kuwa Mimi muuzaji Sitaki dalali I mean ulishasikia kitu kinaitwa "sell by owner" wewe Kama una mnunuzi huyo mnunuzi kwako ndio dalali wake na hiyo haikataliwi. Wewe Kama realtor wa mnunuzi unakaribishwa kuja kuongea na Mimi, Mimi sitokuwa na realtor. Ndivyo biashara ya kuuza nyumba inafanyika. Unachotaka Mimi nifanye ni kukuweka kama dalali wangu yaani as realtor wangu kuilist hiyo nyumba na kuiuza on commission. Mimi Sitaki kuweka realtor but Kama wewe una mteja mlete yeye ndo atakulipa commission. I hope umenielewa
 
Kwa nchi Kama za magharibi unaweza kuuza property with or without realtor. Au muuzaji akawa na realtor wake na mnunuzi akawa na wa kwake. Commission kwa household homes ni standard 6 percent ya sale price. Ikitokea kuna realtors wawili wanagawana Sawa 3 percent each. Tatizo la Tanzania dalali huyo mmoja anataka kula kote kwa muuzaji na kwa muninuzi. Kimsingi mnunuzi hapashwi kulipa commission ni wizi tu unafanyika Tanzania. Mtu anatafuta nyumba ya kupanga analipa fedha ya udalali, same dalali anakwenda kwa land lord anavuta tena. That is not right. Mpangaji anaumizwa sana.
So Mr Kitomali if that is your thinking kuwa dalali wa Mimi muuzaji na same time mnunuzi kwa hapa No! Kama unaye mteja mlete una haja gani kuogopa? I don't want you to be my realtor, but I can sell you my house for your customer.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom