Annina
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 437
- 57
Naomba nikiri katika viumbe ninavyoviogopa, nyoka anashika nafasi ya kwanza. Unaweza usiamini hata kuandika jina lake imenigharimu sehemu kubwa ya ujasiri wangu - naogopa hata picha yake!
Pamoja na ukweli huo, nimeshuhudia picha ya nyoka ikitumika kama kielelezo katika sekta ya afya na fedha. Kwa mfano nembo ya hospitali ya taifa Muhimbili ina picha ya nyoka aliyejizungusha kwenye fimbo, kwenye noti ya sh 500 pia kuna picha ya nyoka again akiwa amejizungusha kwenye fimbo.
Ikumbukwe kuwa si muda mrefu sana toka picha za wanyama zianze kutumika kwenye noti zetu badala ya picha za viongozi kama ilivyokuwa awali, nyoka alianza kutumika kabla ya mabadiliko haya. Cha kushangaza watu wa maliasili kwenye matangazo yao ya vivutio vyetu sijawahi kuona wakitangaza nyoka kama kivutio kama twiga, tembo, simba nk wanavyotangazwa.
Sasa nimekuwa nikijiuliza nyoka ana uhusiano gani na tiba na fedha kwa taifa letu kiasi cha kutumika kama kielelezo?