Mwishoni mwa wiki ilhyopita 3 Dec 2010 bondia wetu kwa jina la Karama Nyilawila wengi mnamfahamu aliishangaza dunia kwa kutwaa taji la dunia la World Boxing Federation (WBF) uzani wa middleweght huko Czech kwa kumtwanga bondia anayeitwa Qato toka Albania. Cha kushangaza hakuna 'Publicity' ya nguvu kwenye media na viongozi wenye dhamana ya michezo pamoja na ngumi wapo kimya. Hii haipendezi kabisa kwa wazalendo wanaoliletea sifa Taifa hili. Au mpaka iwe ni mwana ukoo wa Matumla ndiyo tubumbuluke toka usingizini? Tumpatie Karama Nyilawila heshima yake! Kama Matumla alivyotwaa ubingwa middleweight wa dunia unaotambuliwa na WBU.