Nyie Wabunge wetu Hayati Dr.Magufuli aliwahi kusema Watanzania si Wajinga! Tumepigwa na Mwarabu!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,126
Ebu tuelezeni kwa nini uwekezaji au ubinafsishaji wa DP World kupitia Serikali ya Dubai uwekewe fensi kupitia Azimio la Bunge!?

Ikitokea Watanzania haturidhiki na kazi za DP World, je Bunge litakaa tena kuondoa Azimio la Bunge kuridhia makubaliano haya!

Wabunge mmekazana huu si mkataba wa kazi lakini hii hatua ni fensi ya kutoweza kuja kuiondoa DP World kirahisi kama mlivyofanya kwa TICS ya akina Karamagi !

Jambo hili lina usiri sana na kuna maslahi binafsi hata mjinga anaona wazi!

Nani alimfuata mwenzake kwa ajili ya deal hili , je ni Serikali ya Tanzania au Serikali ya Dubai?

Je Bunge mmejiridhisha kupitia migogoro aliyonayo DP World kwingine Duniani tatizo lao ni nini na how different are you?!

Pamoja na uzuri wa Magufuli lakini ubaya wake ni kuua upinzani Bungeni, leo hatupati mawazo mapya yenye akili !

Bandari ingeweza kuendelea tu kuwa chini ya TPA na kama kuna kazi zifanyike kupitia competitive tendering tu na sio kupitia maazimio ya Bunge!

Hii ni STATE CAPTURE!
 
Back
Top Bottom