Nyerere na mtizamo hafifu wa kusini

dubwela

Member
Oct 23, 2012
28
2
Mengi yalifanyika kipindi cha Nyerere ambayo leo ndio tunaona matunda yake. Wapo wanaosema enzi za Nyerere ufisadi haukuwepo lakini tujiulize wameandaliwa na nani? Utaona wengi wao walizaliwa na kukuzwa na yeye ndo maana hila alizofanya kwa waswahili wa Mafia kubandua lami uwanja wa ndege na kuahidi kujenga nyingine mpaka leo, Mtwara ameng'oa reli akajengea ya Tanga, Kigoma Tabora ni hivyo hakuna kiwanda cha tumbaku na badala yake kipo Morogoro. Hili la gesi wananchi wanakumbuka yasiwakute ya mababu na mabibi zao au yawenzao wa kilwa. Athai ya kuwadharau ni hujuma ktk mradi
 
Teh teh teh.... dubwela, kwahiyo na gesi nayo aliwatuma Nyerere waipeleke Dar badala ya Ntwara? Kama korosho zinazingua, gasi lazima ichukuliwe kwa umakini...hakuna atakayeweza kwenda kuitoa huko kilomita 200 ndani ya bahari.
Last but not least, waswahili wanasema kikulacho ki nguoni mwako.
 
Last edited by a moderator:
Nyerere anahusikaje hapa? Ni Nyerere ndiye alikuwa mlinzi wa rasilimali za madini,mipaka na watu wa Taifa lake.
Ni Nyerere alisema wasichimbe madini mpaka watanzania wawe na akili.
JE,HII NDIO AKILI? JE UAMINIFU WAKE KWA TAIFA ALIPWE KWA UDHAIFU WA VIONGOZI WA SASA?
Mwacheni Babu yetu apumzike.Tusimtupie lawama ktk matokeo ya uzembe wetu
=
 
Mengi yalifanyika kipindi cha Nyerere ambayo leo ndio tunaona matunda yake. Wapo wanaosema enzi za Nyerere ufisadi haukuwepo lakini tujiulize wameandaliwa na nani? Utaona wengi wao walizaliwa na kukuzwa na yeye ndo maana hila alizofanya kwa waswahili wa Mafia kubandua lami uwanja wa ndege na kuahidi kujenga nyingine mpaka leo, Mtwara ameng'oa reli akajengea ya Tanga, Kigoma Tabora ni hivyo hakuna kiwanda cha tumbaku na badala yake kipo Morogoro. Hili la gesi wananchi wanakumbuka yasiwakute ya mababu na mabibi zao au yawenzao wa kilwa. Athai ya kuwadharau ni hujuma ktk mradi

Kwa kuwa sipo hapa kumtetea marehemu,ila napenda nikwambie kwamba, ni bora hata mungu angekunyima hiyo gesi ila akupate japo kakijiakili kadogo tu ka kujifunza na kuitambua historia angalau kidogo tu ya nchi hii.Kwani reli ya kwenda Kigoma imejengwa lini na nani?Najua unaweza usiwe mfuatiliaji wa hotuba za Nyerere ila unaonaje kama ukimuuliza hata jirani yako akwambie Nyerere mwenyewe anasemaje kuhusu rushwa na ufisadi ktk kipindi chake?

Anyway,siwezi kubadili mtazamo wako juu ya marehemu ila ni vema ukatambua kwamba shida na umasikini wako utaondolewa na bidii zako ktk kuchapa kazi na sio kukaa kijiweni kumlalamikia marehemu ambaye kwa namna yoyote ile hawezi kumaliza matatizo yako.
 
Nyerere, Nyerere, hamchoki kumtaja huyu hayati? Hamchoki kumtaja au ndiyo upuuzi mliajazwa na waadhili wenu? Yapo mengi aliyoyafanya mbona hamuyasemi.
 
Kwa hiyo kwa kuwa MUNGU alimuumba SHETANI basi uovu wa shetani ni matokeo ya MUNGU??
Think big...na kwa nini utolee mifano ya TANGA, KIGOMA na TABORA?? kwa nini usitolee mifano ya MARA,SHINYANGA na KAGERA???
Wenye akili tushakusoma akili yako........
 
Back
Top Bottom