Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 950
- 2,866
Hayati Rais Magufuli alinunua mitambo miwili kwa ajili ya bandari ya Dar es Salaam, ambayo ni World first class yenye thamani ya trillion 3.2 na imefungwa juzi tu wakati ameshafariki,ajabu katika maelezo ya mkataba uliopitishwa na bunge,wanasema Dp World wataleta mitambo na kuendeleza bandari!? hivi sisi tumeshindwa kununua mitambo hiyo kidogo kidogo kuweza kuendesha bandari yetu sisi wenyewe,nilipata kusoma juu ya mkataba wa kilaghai aliosaini babu yangu Chifu Mangungo wa Msovelo,kwa kuwa alilaghaiwa na Dr Karl Peters aka mkono wa damu,nilimsamehe,leo siamini kusikia bunge letu lenye wasomi wamepitisha mkataba unaosema "kuhusu muda,makubaliano haya yatakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na mikataba ya miradi" kama kweli bunge limepitisha mkataba wenye maneno hayo basi tumsamehe sana Chifu Mangungo wa Msovelo.
Katika mkataba huo,ibara ya 23(1) ni jambo la hatari kwa taifa kukubali na kiridhia mkataba ambao hauna ukomo wa utekelezaji wake,kifungu kinaeleza kuwa ukomo wa mkataba ni mpaka hapo shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika au muda kwisha wa Host Government Agreement (HGAs),sasa Intergovernmental Agreement (IGA) inachukua maeneo yote ya bandari nchini kama inavyofafanuliwa katika ibara 1,ibara ya 2 na ibara ya 4,haya ni mamlaka makubwa sana anayopewa Dubai rasilimali ya nchi yetu haiwezekani mkataba kutokuwa na muda,rejea tena ibara ya 22,hii ndio ibara inayoruhusu marekebisho,ibara hii inaipa mamlaka nchi ya Dubai kukataa baadhi ya marekebisho ya Tanzania kama nchi ambayo ndio wenye rasilimali za bandari na hivyo Tanzania itaendelea kupata hasara ikiwa haina la kufanya,nini faida ya IGA? Ubinafsishaji uliliathiri taifa la Tanzania na kuua viwanda, uchumi,mashirika ya reli TRL, TTCL,Tanesco,NBC ATCL,kupokonya ajira na kuwapa wa-Asia viwanda na sasa vimegeuzwa kuwa magodown,tuliona Tanesco walivyopewa makaburu,ikaja symbion,iptl na tukapata jibu kwenye kashfa ya Richmond na Escrow.
Azimio la bunge kuridhia mkataba wa IGA,kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendeshaji na uboreshaji wa Utendaji kazi wa Bandari za bahari na maziwa makuu ya Tanzania unakwenda kinyume na sheria za nchi na unakinzana na sera na msimamo wa nchi yetu katika mahusiano ya kimataifa,hakuna utafiti wala tathmini ya kina iliyofanyika kubaini mahitaji ya uwekezaji na fedha zinazohitajika kuboresha bandari zetu na kwa kuwa mkataba huo haujaweka wazi kiasi cha fedha inachokwenda kuwekezwa na pia jukumu la nchi ya Dubai halijawekwa wazi katika mkataba huu,rejea ibara ya 20 kutokutumia sheria za Tanzania kwenye usuluhishi wa migogoro,usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika kusini na kwa kutumia sheria za usuluhishi za kamisheni ya Umoja wa mataifa juu ya sheria zinazohusika na biashara za kimataifa (Unicitral arbitration rules) kifungu hiki kinakwenda kinyume na kifungu cha 11 cha sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa rasilimali na maliasili ya mwaka 2017 (the natural wealth and resources (permanent sovereignty) Act no.5 of 2017) ambapo inaelezwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili ya nchi ya Tanzania,hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje,bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
Ibara ya 25(1) inaeleza kuwa shughuli za awali za kufanya upembuzi yakinifu na kufanya tathmini itafanyika baada ya mkataba wa IGA kusainiwa,hii si sawa maana tunao uzoefu wa kubinafsishwa kwa benki ya Taifa ya biashara,tuliambiwa benki ina madeni mengi,jibu lipo kichwani kama nanunua kampuni yako yenye madeni basi gharama za ununuzi nitatoa madeni kinachobaki ndio nakupa kisipobaki basi unanipa bure, Mkataba unahusisha maeneo yote ya bandari za bahari ya Hindi na maziwa makuu,Dubai walipaswa kupewa eneo moja tu phase 1,badala ya kumpa maeneo yote,kwa mujibu wa sheria ya bandari na 17 ya mwaka 2004 lazima Dubai ataje aina ya uwekezaji anaokwenda kufanya kwenye mkataba sio kutaja kiujumla eti kuendeleza,kusimamia na kuendesha bandari,lazima mkataba ueleze Tanzania itanufaika vipi,sio kusema DP World inakuja kuwekeza kibiashara,kama ni hivyo hakuna umuhimu wa IGA,Dp World ilipaswa kupewa kazi kwa utaratibi wa kawaida tu kupitia TPA na kwa sheria za Public private partnership (PPP) act na public procurement act,no 7 of 2011 badala ya kupitia mgongo wa IGA,
Nimalizie kwa kusema IGA inayoingiwa ni kwa ajili ya kuwekeza katika bandari za Tanzania na sio makubaliano ya uendeshaji wa bandari za Tanzania na bandari za Dubai, kwenye mkataba huu jukumu la nchi ya Dubai halijafahamika bayana ukiondoa makampuni yake yanayokuja kuwekeza nchini,utiaji sahihi unamuonesha Waziri wa Tanzania na CEO wa mamlaka ya bandari wa Dubai,hapa hatujazingatia ibara ya 28 ya sheria za mikataba(International Laws) nashauri kuvunja mkataba wa IGA na badala yake mamlaka ya bandari Tanzania (TPA) na kampuni ya DP World waingie makubaliano HGAs kwa kufuata taratibu zote na tuone,nawaona Chadema mkirudi kumsafisha Hayati Rais Magufuli kwa alivyovipigania na baada ya kuondoka vinatokea,hivi tumeshindwa kuboresha au kuendesha bandari,Mwalimu Nyerere alisema "Nia tunayo,Hali tunayo na Uwezo tunao" kipi ambacho tukitia nia tunashindwa!? ndugu zangu wabunge msiongee kwa tumia hamasa na kufukuzia kurudi kwa jina kwenye uchaguzi 2025 nawasihi kutumia weledi maana huku mitaani kuna WASOMI wa kila aina kuliko huko bungeni hivyo lazima mjue kuwa kila mnachoongea na kuchambua watu huku mitaani wanafanyia performance appraisal kwa maslahi mapana ya Tanganyika.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.