Humu ndani, kuna watu wakiona Hayati Julius Nyerere, the First Preisdent wa URT anasemwa vibaya basi wanakuja juu!! Kinachonikera mimi, ni wengi wao kuhusisha na imani za dini! Kwamba, mtu akisema ubaya wa Nyerere, na hasa mtu huyo akihisiwa ni Mwislamu, basi hoja ya wapofu wa hoja watachukulia ukosoaji huo ni chuki ya waislamu dhidi ya Nyerere!! Hivi ni lini Waislamu wamepata kuwa na chuki na mwalimu?! Sasa haya mambo kwamba mtu akitaja mabovu ya Mwalimu basi ni chuki za waislamu dhidi ya mwalimu yanatoka wapi?! Binafsi, am muslim, na kama utaniambia nikutajie my favorite president sitasita kumtaja Julius Nyerere. lakini pamoja na yote hayo, kama nitaambiwa nitaje top two poorest presidents ever happaned in our history, basi Nyerere ni mmoja wapo, akiwa sambamba na mwinyi! Binafsi, nikimwangalia Nyerere, ni eneo moja peke yake ambalo linaweza kumweka kama best leader! hakuwa corrupt leader ingawaje serikali yake ilikuwa very corrupt government!! Na wala si kweli kwamba Nyerere alikuwa mkali kwa corrupt leaders, vinginevyo nchi hii Mwinyi asingeikuta alipoikuta! Sana sana ki2 ambacho labda Nyerere aliweza kuzuia ni kutokuwa na State House corrupt leaders...lakini ukitoka hapo, wengi walikuwa corrupts!
Serikali ya Nyerere ilijaa watendaji ambao walikosa kabisa uwajibikaji na ndio maana Mwinyi alikuja na kitu kilichojulikana kama Fagio La Chuma! Kwanini awe na fagi la chuma wakati uwajibikaji ulikuwapo?! Serikali isiyo corrupt, haiwezi kuwa na irresponsible leaders. Ni kweli, Nyerere hakuwa corrupt leader, lakini aliendesha corrupt government na anayebisha aniambie kwanini viwanda vyote vilifia mikononi mwake!!
Ni kweli JK ni goi goi! hata Nyerere alikuwa ni goi goi kupita kiasi!! hakuwa mkali kama tunavyoaminishwa watu ambao hatukuwa na ufahamu wakati wa utawala wake. Nyerer alikuwa mkali kwa wapinzani wake wa kisiasa, and not otherwise!! Kama alikuwa mkali kweli, umasikini tulionao ulitokea wapi?! Aliwafanya nini waliokuwa wanaharibu mali za umma zaidi ya kuwahamisha?! kama sio ugoi goi tuite nini hii?!
Kulikuwa na miradi kadhaa ambayo ilianzishwa wakati wa utawala wake, na vilevile ilikufa hata kabla haijafika kokote....sasa kama sio ubadhirifu huo tuite nini?! Siwezi kumsifia kiongozi aliye msafi yeye pekee na familia yake wakati serikali yake imejaa watu irresponsible!!
Amekaa Ikulu more than 20 years lakini ametoka akiwa ameachwa barabara zimejaa mahandaki kila mahali!! Bahati mbaya sana, sehemu ambazo zilikuwa na corrupt leaders toka kwenye serikali yake ndio sehemu pekee ambazo angalau zilikuwa na barabara nzuri kidogo! Sehemu ambazo walitoka honest leaders kama yeye, ndizo zikabaki balaa tupu!!! Hiyo ndio sababu kuu iliyofanya mikoa ya kusini kuwa hoe hae zaidi kwani viongozi wake wengi walikuwa honest kama yeye...hawa ni pamoja na akina Kawawa na Nnauye! Hivyo, umaskini wa kusini haukusababishwa na Nyerere kama Nyerere, bali ulisababishwa na irresponsible central government ambayo ugawaji wa keki ya taifa haukuwa the same! ilitegemea sana sehemu husika ana power gani serikalini and how corrupt s/he is!!!
Nyerere ameondoka akiwa ameacha vyuo vikuu viwili tu, UDSM na SUA na kuishia tu ktk kujenga vyuo vya kati ambavyo hata hivyo navyo productivity yake ilikuwa chini. Chuo pekee cha kati ambacho kilikuwa kinatoa elimu ya maana labda ni Mzumbe peke yake....na sababu kuu ni kwavile kilikuwa more political! Tena hata nina mashaka kama kweli kilikuwa kinatoa elimu ya maana!! tangu lini katibu wa nini sijui mwenye miaka 45++ akaweza kuhimili mikiki mikiki ya elimu ya juu?! Tunaambiwa enzi zake elimu ilikuwa na ubora kuliko sasa!! na hii ndio tabia ya wazee....kwamba kila ki2 chao kilikuwa bora!!! Huo ubora ulisaidia nini basi katika kutatua matatizo ya uchumi wa nchi hii?! Sana sana hao tunaoambiwa walikuwa wasomi wakati wa elimu bora ndio hao hao waliogeuka kuwa corrupts wasio na haya wakati wa Mwinyi.....bisheni!!! Kama ni kweli wakati huo elimu ilikuwa bora basi vilevile ilisaidia kuzalisha BEST CORRUPT LEADERS!!! Serkali corrupt haiwezi kuwa na jeuri ya kujenga vyuo vikuu vya kutiosha kwavile haina fedha.....kutokuwa na fedha ni dalili ya serikali corrupt!!!
MATATIZO ya umeme tuliyonayo hivi sasa source yake ilikuwa enzi za mwalimu!!! Serikali ya Mwalimu haiku-forecast mahitaji ya umeme over the next 50 years!! Ni kweli, wakati wa Nyerere, haukuwa wa mgao! Sasa mgao ungetoka wapi wakati nyumba zenyewe za umeme zilikuwa chache?! Mgao ungetoka wapi wakati hakukuwa na uzalishaji mkubwa wa kuhitaji matumizi ya umeme?! Mgao ungetoka wapi wakati hata kumiliki radio ilikuwa ni anasa?! Kwahiyo, si kwamba ni uongozi bora wa Nyerere ambao ulifanya nchi isiwe na mgao/upungufu wa umeme, bali hiyo ilikuwa ni matokeo ya serikali mbovu!
Tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Huduma gani za jamii?! hizo za kufuata zahanati kilometa 50 na shule ya msingi kilometa 10?! Dar es salaam yote hii aliacha shule saba tu za sekondari (za serikali, ambazo hata hivyo hakujenga yeye)-Jangwani, Azania, Tambaza, Forodhani, Kisutu na Kibasila!!! Nani atakayethubutu kusema kwamba shule hizo zilikuwa zinakidhi mahitaji ya elimu ya sekondari jijini? Huko mikoani ndo ilikuwa balaa tupu, unaweza kukuta mkoa mzima una shule moja au mbili za serkali.....bado tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Ni serikali gani ingeshindwa kuhudumia shule chache kama hizo?!
Ubovu wa serikali ya Nyerere ni mwingi kuliko uzuri wake, otherwise, wale wanaoona kwamba mgtu akisema basi ana chuki za kidini (styupid thinking) basi anitajie hapa mazuri yaliyofanywa na serikali yake ambayo natarajia yawe mengi kuliko mabovu!
wapo watakaosema kwamba Nyerere amewezesha nchi hii kuwa na amani! Kwani aliichukuwa wakati nchi haina amani?! Sifa kama hizo anatastahili kupewa Kagame aliyechukua nchi baada ya mauaji ya kutisha nchini mwake! Anyway, waliosoma historia wanisaidie kunitajia ni vita gani vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimepata kupiganwa Tanganyika katika karne ya 19! Kama hakuna au zilikuwa si za kutisha sana, basi inawezekana Watanganyika hatuna silika ya kupigana tangu zama hizo!!
Hivyo basi, mtu anavyotaja ubovu wa Nyerere inakuwa ni ujinga uliepitiliza kusema kwamba ni chuki binafsi...Na inakuwa sio ujinga, bali ni upumbavu mtu akisema ni chuki za kidini! Nyerere kama Nyerere alikuwa was a very good person BUT NOT A GOOD LEADER! He was a good person who was a poor leader! Kutokana na hayo, sipati kigumumizi hata chembe kusema wazi kwamba SI KWAMBA NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU, BALI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU! Ukweli wenyewe ndio huo, ukiona mgumu kuumeza, chukua maji ushushie!
Anayekataa, atoe data za mazuri yake kama kiongozi yenyewe manufaa kwa Tanzania!
Hakuna cha maana mnachotafuta zaidi ya kutafuta mchawi wa maovu yenye! Mnatafuta sababu ya kushidwa kwenu! Kama suala ni Nyerere alikwisha sema nakuwa malaika na mlitakiwa kuendeleza misingi na mambo mazuri aliyoyafanya na kuyaacha mabaya. Lakini msululu wote wa maraisi mmeishia kumlaumu bila kufanya la maana kwa watanzania zaidi ya kuuza nchi kwa wageni na kuturudisha katika utumwa. Ni kituko kuona hakuna mwananchi anayeweza kuwekeza katika nchi yake zaidi ya ninyi viongozi mliogeuka wajasiriamali na wageni kwa kigezo cha uwekezaji