Mnyampaa
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 244
- 58
Linasomeka gazeti la Jamhuri katika kichwa chake cha habari Juni26, 2012, likufuatia kichwa cha habari kinachofanana na toleo lililopita. Hivi Kuna ukweli juu ya hili au ni fitna za kisiasa kwani maelezo ya ndani ya habari hii hayaonyeshi wazi juu ya usaliti huu isipokuwa sakata la TANAPA na 'Wawekezaji' wenye Hoteli za kitalii juu ya 'concession fee' ambapo inasemekana Nyalandu alishauri katika kikao kimojawapo juu ya utaratibu wa malipo hayo. Ninashawishika kuhoji hivi kutokana na ukweli kuwa habari hii imekuwa ikiandikwa na gazeti hili tu.