Nuclear attack: "PRE-RU-SHE-A" mbinu ya kijeshi inayoweza kuokoa uhai wako wakati wa shambulizi la Nyukilia

Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
1,262
2,191
Moja Kati ya silaha inayotisha kwa sasa duniani ni nyukilia. Endapo utakutwa na shambulizi la nyukilia ni vyema ukatumia mbinu ya "PRE-RU-SHE-A' ili kupona shambulizi hilo.

Wakati wa vita endapo BOMU la nyukilia litapigwa wanajeshi na raia ushauriwa kutumia mbinu hii ya "PRE-RU-SHE-A" ikiwa ni muunganiko wa maneno manne yaani
PRE -Preparedness
RU -Running
SHE -Shelters
A -Aftermath

Kabla sijaanza kuelezea mbinu hii, ngoja nielezee kidogo kuhusu silaha za nyukilia.

Nafasi ya uwepo wa vita ya nyukilia ni ndogo sana kutokana na sheria kali zilizowekwa chini ya usimamizi wa tume ya nishati ya nyukilia chini ya International Atomic Energy Agency (IAEA) duniani, vita ya nuclear endapo itatokea ni wazi kwamba anayeweza kuanzisha ni mataifa yenye nguvu za kijeshi na silaha za nyukilia duniani na ikitokea itakuwa ni mauaji ya ulimwengu mzima.

Silaha za maangamizi za nyukilia zinatakiwa kuwa chini ya usimamizi wa mtu aliye imara kiafya na kiakili na asiye na maamuzi ya hasira, aliye tayari kupokea ushauri kwani zikiwa chini ya mikono ya mtu asiye sahihi zinaweza kupelekeaa madhara makubwa sana.

Ni nchi tisa tu duniani ambazo ni China, USA, Russia, North korea, Pakistan, India, UK, Ufaransa na Israel ndizo zenye makombora ya ballistic missiles yenye vichwa vya nyukilia (warheads) na uwezo wa kurusha kombora la la nyukilia kwenye sehemu/mtu aliyelengwa duniani kwa umbali wowote na bomu kufika.

Russia, USA na China ni nchi zenye uwezo wa kurusha kombora la nyukilia eneo lolote duniani na kombora hilo likafika.

Bomu la nyukilia la sasa ni imara na lenye nguvu sana ukilinganisha/kuliko lile lililotumika Hiroshima & Nagasaki wakati wa vita ya pili ya dunia 1945. Mabomu yaliyotumika katika miji hiyo yalikuwa na ukubwa wa tani elfu 12(12kt) ya TNT na yaliua karibia watu laki tatu 300,000. Baadhi ya warheads za sasa zina 1000kt. Silaha zozote za nyukilia ni silaha za maangamizi(mass destruction) na shambulio lolote la nyukilia ni catastrophe ambayo mtu anaweza kupona.

Hata bomu la Hiroshima & Nagasaki kuna waliopona, kwahiyo kwa mbinu hii unaweza kupona kabisa hata kama umekumbana na shambulio la nyukilia.

KUJIANDAA/KUWA TAYARI NA SHAMBULIO LA BOMU(PREPAREDNESS)
Kama umepewa tahadhari, eneo zuri la kujikinga na mshutuko wa wimbi, mlipuko wa joto na mionzi ya BOMU la nyukilia ni chini ya uso wa ardhi kwa sababu fireball na madhara ya vacuum uisha ndani ya dakika chache.

Lakini jambo la kukumbuka ni kwamba, kwa kutegemea BOMU limelipukia chini kwenye ardhi au juu angani litaweza kutoa nishati ya moto, hali hii siyo kwamba itakupelekea kuwa kipofu bali hata kuteketeza hadi kivuli chako mwenyewe na ukabaki majivu.

JE UNATAKIWA KUFANYA NINI & KUCHUKUA MAAMUZI GANI.
Nguvu ya uharibifu wa BOMU la nyukilia imegawanyika katika sehemu tofauti, bila kuchimba kabisa atomic physics, sehemu hizo ni hizi zifuatazo;
✓Thermal pulse/flash
✓Thermal heat/blast wave
✓Electromagnetic pulse(EMP)
✓Radiations

Thermal pulse
Baada ya kuwa BOMU la nyukilia limepiga, ghafla unatokea mwanga mkali sana (Visible Ultra light), mwanga huu kitaalamu unaitwa thermal pulse/flash, wakati huo huo kwenye kitovu cha mlipuko yaani epicenter utoa joto lenye 10,000,000 °C, joto hili linaitwa thermal heat, katika joto hili kiumbe yeyote ambaye hawezi kustahimili ugeuka majivu na kuyeyushwa kabisa.

Blast wave
Baada ya joto hili inatokea mlipuko wa wimbi lenye nguvu (blast wave) ambao upelekea mlipuko hewani/angani, hali hii inapelelekea kuharibika kwa sehemu mbali mbali za mwili na uweza kupasua mapafu. Blast wave ina uwezo wa kusomba na kupeperusha mtu, gari na majengo kwa umbali wa miles 300 kwa saa.

Electromagnetic Pulse
Hii inatokana na mlipuko wa nyukilia wakati ambapo hewa(air) inayozunguka blast inaanza kutoa cheche kwa sababu ya ionization. Usitegemee kutumia vyombo vya usafiri, simu,kompyuta au chochote kile ambacho ni non mechanical baada ya mlipuko huu.

Radiations
Huu ni uharibifu unaotokana na mionzi ya Nyukilia. Mionzi hiyo ni alpha,beta na gamma.
BOMU la nyukilia linapolipuka utoa mionzi hii inayokuwa inaelea hewani baada ya muda mfupi uanza kushuka chini kama vile uonavyo barafu inashuka chini(snowfall).

Alpha & beta ni mionzi isiyo na nguvu sana hivyo ili upate madhara yake ni lazima uvute hewa yake au skin contact. Gamma ndiyo mionzi hatari kwani uweza kupita moja kwa moja kwenye ngozi na kuingia mwilini, hivyo kuua seli za mwili. Kama utakuwa exposed with high doses, basi itakuchukua wiki 6 hadi 7 kufariki.

Marekani ili kujaribu kuzuia madhara ya mionzi hiyo tayari wametengeneza dawa za matibabu ya dharula ambazo ni POTASSIUM IODIDE & PRUSSIAN BLUE (ambayo imekuwa ikiuzwa kama Radiogardase), Kwahiyo hakikisha nyumbani kwako una potassium iodide & Radiogardase kama uchumi unaruhusu.

Vitu vinavyoweza kupunguza mionzi ya Gamma baadhi yake ni kama ifuatavyo

✓Chuma(steel) chenye ukubwa wa inches 6
✓Kizuizi cha mwamba(rock) chenye ukubwa wa 2-3 feet thick
✓Njia ya chini ardhini yenye dari ya udongo angalau 3 feet thick
✓Makazi ya barafu yenye angalau 7 feet thick
✓Kizuizi cha Ubao chenye angalau 8 feet thick

SURVIVING THE BLAST WAVE
Unatakiwa kuchukua hatua zifuatazo, ili kujinusuru na blast wave baada ya BOMU kulipuka.

✓Kabla hujapigwa na blast wave hakikisha umelala chini, ukifunga miguu, na uangalie uelekeo tafauti na ulipotokea mlipuko.

✓Endelea kufungua mdomo kwani endapo utafunga mdomo utafanya mgandamizo wa hewa kuongezeka na kupelekea mapafu kutanuka, hivyo mapafu kupasuka.

RADIATIONS
Hapa utaamua ukimbie au ukae kwenye makazi ya hifadhi. Baada ya kupona kutokana na mlipuko, basi itakubidi ukimbie au ujihifadhi mahali Ili kuepuka mionzi ya nyukilia inayoshuka chini.

KUKIMBIA(RUNNING)

Tafuta njia ambayo upepo unavuma kuelekea, kimbia katika nyuzi 90°perpendicular na uelekeo wa mawimbi ya upepo. Kwa kutegemea kasi yako ya kukimbia unatakiwa kuwa umbali wa miles 30 ili kuepuka lethal dose ya mionzi ya Nyukilia ambayo upimwa katika kipimo cha REMs .

•3000 REMs kwa umbali wa miles 30 kutoka kwenye mlipuko.
•900 REMs kwa umbali wa miles 90(900 REMs inasababisha kifo ndani ya siku 2-14)
°300 REMs kwa umbali wa miles 160(300 REMs usababisha uharibifu wa nerve cell, digestive tract & nywele kuisha)
•Umbali wa miles 250 kutoka kwenye kitovu cha mlipuko upunguza kabisa madhara ya mionzi ya nyukilia.
Screenshot_20220306-113857_1.jpg

NDANI YA HIFADHI/MAKAZI(SHELTERS)​

Sehemu nzuri zaidi ya kujihifadhi ni kwenye handaki ngumu yenye mifumo ya kuchuja na kufyonza hewa.

Russia ina handaki elfu 8 za kuhifadhi raia wake na nyukilia ambayo ni sawa na 11% ya watu wote nchini Russia, huku handaki zaidi ya elfu 5 ujenzi wake ukiwa unaendelea. China inafikiriwa kuwa na zaidi ya hizo, huku nchi ya Switzerland ikiwa na fallout shelters za kuhifadhi raia wake wote.

USA idadi kamili haijulikani ila wanazo hata zile zilizotumika miaka ya 1960s bado zipo. Kuna maeneo mengi sana yaliyotengwa maalimu kwa ajili ya viongozi wa Serikali na jeshi ambayo yanaweza kuwahifadhi kwa zaidi ya miezi 30.

Katika mbinu hii itakubidi ufanye yafuatayo;

✓Jaribu kuingia kwenye majengo yenye basement, kama unaishi kwenye nyumba/apartment yenye basement unatakiwa kwenda kwenye basement ya chini kabisa.

✓Kama nyumba/apartment haina basement panda kwenye ghorofa ya juu na uache ghorofa mbili kutoka kwenye dari ya mwisho. kumbuka kufunga ventilator yeyote kama vile kuzima kabisa air conditioning.

✓Ili kujikinga na mionzi ya Gamma hakikisha unajenga basement yako kwa kutumia cabinets, books,desks & doors, Gamma rays haziwezi kupiga kona kwahiyo hakikisha sehemu ya kuingia kwenye basement inakuwa na umbo la L(L shape).

✓Kama una muda chimba shimo lenye angalau urefu na upana wa futi 6 na utengeneze dari yake kwa kutumia corrugated metal inayoweza kufunikwa na udongo. Udongo una absorb mionzi kwa urahisi sana na hii itazuia mionzi ya Nyukilia isiweze kuingia mwilini mwako na kuleta madhara.​

Screenshot_20220306-113919_1.jpg

Aftermath of the blast

Labda uwe na kifaa kinachoitwa Geiger counter, hakuna njia unayoweza kutumia kupima radiations tofauti na hicho kifaa. Radiations hazionekani kwa macho, hazina alafu wala taste, lakini zinakiwepo.

Unatakiwa baada ya kusurvive ufanye yafuatayo hili kuondoa mabaki yote ya mionzi ya nyukilia

✓Uoshe mwili wako wote kwa maji ya chumvi au sabuni na maji.
✓Kama huna maji, tumia nguo safi au hata gazeti na taratibu anza kupangusa sehemu unayohisi ni contaminated.
✓Tumia udongo kupangusa na kusafisha mwili (udongo utakaotumia hakikisha hauna contaminations za radiations).
✓Vua nguo zote ulizokuwa umevaa wakati wa mlipuko na kuziweka kwenye kifaa cha plastiki na uzipeleke mbali kuzitupa.
✓Usitoke kwenye eneo lako la kujihifadhi hadi baada ya masaa 72, baada ya huu muda zaidi ya 90% ya radiations itakuwa imepoteza nguvu ila kama unaweza kuendelea kukaa, ni vizuri ufanye hivyo kwa usalama zaidi.
✓Hakikisha unakaa nje sehemu yenye hewa kwa dakika 60 kwa siku, na taratibu endelea kwa zaidi ya masaa 2-3 kwa week(hii ni baada ya kusurvive blast)
✓Unatakiwa uchukulie kwamba maji kutoka kwenye maziwa(lakes), mabwawa na vyanzo vingine vya maji ni contaminated.
✓Usile fresh food zilizopakiwa na kutunzwa kwenye plastiki kwani zitakuwa contaminated, isipokuwa utumie canned foods.

Siyo kwamba ni guarantee utapona ukifanya hivyo, Ila ukiwa unapambana kujiokoa ni vyema utumie hizo mbinu katika kusurvive blast wave ya kombora la nyukilia.

N.B Mimi siyo mtaalamu wa atomic physics, kwahiyo hiki nilichoelezea hapa ni uelewa wangu nilionao juu ya BOMU la nyukilia. Kama unajua zaidi ni vyema ukajikita katika kuelezea zaidi kile unachokifahamu ili watu wajifunze zaidi.

#DUNIA NI YETU SOTE TUISHI KWA AMANI.​
 
Moja Kati ya silaha inayotisha kwa sasa duniani ni nyukilia. Endapo utakutwa na shambulizi la nyukilia ni vyema ukatumia mbinu ya "PRE-RU-SHE-A' ili kupona shambulizi hilo.

Wakati wa vita endapo BOMU la nyukilia litapigwa wanajeshi na raia ushauriwa kutumia mbinu hii ya "PRE-RU-SHE-A" ikiwa ni muunganiko wa maneno manne yaani
PRE -Preparedness
RU -Running
SHE -Shelters
A -Aftermath

Kabla sijaanza kuelezea mbinu hii, ngoja nielezee kidogo kuhusu silaha za nyukilia.

Nafasi ya uwepo wa vita ya nyukilia ni ndogo sana kutokana na sheria kali zilizowekwa chini ya usimamizi wa tume ya nishati ya nyukilia chini ya International Atomic Energy Agency (IAEA) duniani, vita ya nuclear endapo itatokea ni wazi kwamba anayeweza kuanzisha ni mataifa yenye nguvu za kijeshi na silaha za nyukilia duniani na ikitokea itakuwa ni mauaji ya ulimwengu mzima.

Silaha za maangamizi za nyukilia zinatakiwa kuwa chini ya usimamizi wa mtu aliye imara kiafya na kiakili na asiye na maamuzi ya hasira, aliye tayari kupokea ushauri kwani zikiwa chini ya mikono ya mtu asiye sahihi zinaweza kupelekeaa madhara makubwa sana.

Ni nchi tisa tu duniani ambazo ni China, USA, Russia, North korea, Pakistan, India, UK, Ufaransa na Israel ndizo zenye makombora ya ballistic missiles yenye vichwa vya nyukilia (warheads) na uwezo wa kurusha kombora la la nyukilia kwenye sehemu/mtu aliyelengwa duniani kwa umbali wowote na bomu kufika.

Russia, USA na China ni nchi zenye uwezo wa kurusha kombora la nyukilia eneo lolote duniani na kombora hilo likafika.

Bomu la nyukilia la sasa ni imara na lenye nguvu sana ukilinganisha/kuliko lile lililotumika Hiroshima & Nagasaki wakati wa vita ya pili ya dunia 1945. Mabomu yaliyotumika katika miji hiyo yalikuwa na ukubwa wa tani elfu 12(12kt) ya TNT na yaliua karibia watu laki tatu 300,000. Baadhi ya warheads za sasa zina 1000kt. Silaha zozote za nyukilia ni silaha za maangamizi(mass destruction) na shambulio lolote la nyukilia ni catastrophe ambayo mtu anaweza kupona.

Hata bomu la Hiroshima & Nagasaki kuna waliopona, kwahiyo kwa mbinu hii unaweza kupona kabisa hata kama umekumbana na shambulio la nyukilia.

KUJIANDAA/KUWA TAYARI NA SHAMBULIO LA BOMU(PREPAREDNESS)
Kama umepewa tahadhari, eneo zuri la kujikinga na mshutuko wa wimbi, mlipuko wa joto na mionzi ya BOMU la nyukilia ni chini ya uso wa ardhi kwa sababu fireball na madhara ya vacuum uisha ndani ya dakika chache.

Lakini jambo la kukumbuka ni kwamba, kwa kutegemea BOMU limelipukia chini kwenye ardhi au juu angani litaweza kutoa nishati ya moto, hali hii siyo kwamba itakupelekea kuwa kipofu bali hata kuteketeza hadi kivuli chako mwenyewe na ukabaki majivu.

JE UNATAKIWA KUFANYA NINI & KUCHUKUA MAAMUZI GANI.
Nguvu ya uharibifu wa BOMU la nyukilia imegawanyika katika sehemu tofauti, bila kuchimba kabisa atomic physics, sehemu hizo ni hizi zifuatazo;
✓Thermal pulse/flash
✓Thermal heat/blast wave
✓Electromagnetic pulse(EMP)
✓Radiations

Thermal pulse
Baada ya kuwa BOMU la nyukilia limepiga, ghafla unatokea mwanga mkali sana (Visible Ultra light), mwanga huu kitaalamu unaitwa thermal pulse/flash, wakati huo huo kwenye kitovu cha mlipuko yaani epicenter utoa joto lenye 10,000,000 °C, joto hili linaitwa thermal heat, katika joto hili kiumbe yeyote ambaye hawezi kustahimili ugeuka majivu na kuyeyushwa kabisa.

Blast wave
Baada ya joto hili inatokea mlipuko wa wimbi lenye nguvu (blast wave) ambao upelekea mlipuko hewani/angani, hali hii inapelelekea kuharibika kwa sehemu mbali mbali za mwili na uweza kupasua mapafu. Blast wave ina uwezo wa kusomba na kupeperusha mtu, gari na majengo kwa umbali wa miles 300 kwa saa.

Electromagnetic Pulse
Hii inatokana na mlipuko wa nyukilia wakati ambapo hewa(air) inayozunguka blast inaanza kutoa cheche kwa sababu ya ionization. Usitegemee kutumia vyombo vya usafiri, simu,kompyuta au chochote kile ambacho ni non mechanical baada ya mlipuko huu.

Radiations
Huu ni uharibifu unaotokana na mionzi ya Nyukilia. Mionzi hiyo ni alpha,beta na gamma.
BOMU la nyukilia linapolipuka utoa mionzi hii inayokuwa inaelea hewani baada ya muda mfupi uanza kushuka chini kama vile uonavyo barafu inashuka chini(snowfall).

Alpha & beta ni mionzi isiyo na nguvu sana hivyo ili upate madhara yake ni lazima uvute hewa yake au skin contact. Gamma ndiyo mionzi hatari kwani uweza kupita moja kwa moja kwenye ngozi na kuingia mwilini, hivyo kuua seli za mwili. Kama utakuwa exposed with high doses, basi itakuchukua wiki 6 hadi 7 kufariki.

Marekani ili kujaribu kuzuia madhara ya mionzi hiyo tayari wametengeneza dawa za matibabu ya dharula ambazo ni POTASSIUM IODIDE & PRUSSIAN BLUE (ambayo imekuwa ikiuzwa kama Radiogardase), Kwahiyo hakikisha nyumbani kwako una potassium iodide & Radiogardase kama uchumi unaruhusu.

Vitu vinavyoweza kupunguza mionzi ya Gamma baadhi yake ni kama ifuatavyo

✓Chuma(steel) chenye ukubwa wa inches 6
✓Kizuizi cha mwamba(rock) chenye ukubwa wa 2-3 feet thick
✓Njia ya chini ardhini yenye dari ya udongo angalau 3 feet thick
✓Makazi ya barafu yenye angalau 7 feet thick
✓Kizuizi cha Ubao chenye angalau 8 feet thick

SURVIVING THE BLAST WAVE
Unatakiwa kuchukua hatua zifuatazo, ili kujinusuru na blast wave baada ya BOMU kulipuka.

✓Kabla hujapigwa na blast wave hakikisha umelala chini, ukifunga miguu, na uangalie uelekeo tafauti na ulipotokea mlipuko.

✓Endelea kufungua mdomo kwani endapo utafunga mdomo utafanya mgandamizo wa hewa kuongezeka na kupelekea mapafu kutanuka, hivyo mapafu kupasuka.

RADIATIONS
Hapa utaamua ukimbie au ukae kwenye makazi ya hifadhi. Baada ya kupona kutokana na mlipuko, basi itakubidi ukimbie au ujihifadhi mahali Ili kuepuka mionzi ya nyukilia inayoshuka chini.

KUKIMBIA(RUNNING)

Tafuta njia ambayo upepo unavuma kuelekea, kimbia katika nyuzi 90°perpendicular na uelekeo wa mawimbi ya upepo. Kwa kutegemea kasi yako ya kukimbia unatakiwa kuwa umbali wa miles 30 ili kuepuka lethal dose ya mionzi ya Nyukilia ambayo upimwa katika kipimo cha REMs .

•3000 REMs kwa umbali wa miles 30 kutoka kwenye mlipuko.
•900 REMs kwa umbali wa miles 90(900 REMs inasababisha kifo ndani ya siku 2-14)
°300 REMs kwa umbali wa miles 160(300 REMs usababisha uharibifu wa nerve cell, digestive tract & nywele kuisha)
•Umbali wa miles 250 kutoka kwenye kitovu cha mlipuko upunguza kabisa madhara ya mionzi ya nyukilia.

View attachment 2140850

NDANI YA HIFADHI/MAKAZI(SHELTERS)

Sehemu nzuri zaidi ya kujihifadhi ni kwenye handaki ngumu yenye mifumo ya kuchuja na kufyonza hewa.

Russia ina handaki elfu 8 za kuhifadhi raia wake na nyukilia ambayo ni sawa na 11% ya watu wote nchini Russia, huku handaki zaidi ya elfu 5 ujenzi wake ukiwa unaendelea. China inafikiriwa kuwa na zaidi ya hizo, huku nchi ya Switzerland ikiwa na fallout shelters za kuhifadhi raia wake wote.

USA idadi kamili haijulikani ila wanazo hata zile zilizotumika miaka ya 1960s bado zipo. Kuna maeneo mengi sana yaliyotengwa maalimu kwa ajili ya viongozi wa Serikali na jeshi ambayo yanaweza kuwahifadhi kwa zaidi ya miezi 30.

Katika mbinu hii itakubidi ufanye yafuatayo;

✓Jaribu kuingia kwenye majengo yenye basement, kama unaishi kwenye nyumba/apartment yenye basement unatakiwa kwenda kwenye basement ya chini kabisa.

✓Kama nyumba/apartment haina basement panda kwenye ghorofa ya juu na uache ghorofa mbili kutoka kwenye dari ya mwisho. kumbuka kufunga ventilator yeyote kama vile kuzima kabisa air conditioning.

✓Ili kujikinga na mionzi ya Gamma hakikisha unajenga basement yako kwa kutumia cabinets, books,desks & doors, Gamma rays haziwezi kupiga kona kwahiyo hakikisha sehemu ya kuingia kwenye basement inakuwa na umbo la L(L shape).

✓Kama una muda chimba shimo lenye angalau urefu na upana wa futi 6 na utengeneze dari yake kwa kutumia corrugated metal inayoweza kufunikwa na udongo. Udongo una absorb mionzi kwa urahisi sana na hii itazuia mionzi ya Nyukilia isiweze kuingia mwilini mwako na kuleta madhara.​

View attachment 2140874
Somo zuri
 
Hizo tabu zote za nini Russia warushe moja tu Ukraine tujifunze
Hapana usiseme hivyo ndugu yangu, Russia yeye ana fallout shelters za kutosha kuhifadhi raia wake ikitokea ameshambuliwa na Nyukilia ndiyo maana anajihami na Nyukilia sana, USA wanalitambua hilo ndiyo maana hawataki kujihusisha direct, sasa watakao kufa kama sisimizi ni raia wa Ukraine endapo Russia atatumia nyukilia kushambulia.
 
Mambo mengi sana
Mambo ni mazito kweli, wewe Afrika hakuna nchi hata moja yenye kinu au fallout shelters kwa ajili ya Nyukilia. Alikuwa nazo South Africa mwanzoni mwa miaka ya 90, makaburu walipomkabizi nchi Mandela, SA ikawekewe vikwazo vya kiuchumi hali ikawa tete, vinu vya nyukilia vika vanish. Kilichotokea Chemists wote na wataalamu wa atomic physics, wakawa recruited na nchi nyingine mojawapo Pakstan. Kwahiyo Nyukilia ikirushwa Africa ni vifo tu kwa raia.
 
Wabongo tukisikia mlipuko tutaukimbilia ili tufaham kulikoni
Hilo ndilo tatizo, Nchi za wenzetu mfano USA & Russia raia wanapewa elimu kabisa juu ya usalama wao. Ukienda nchi za wenzetu nyumba bila basement ni kama haijakamilika, kwa sababu basement ni for security purposes against the enermies ndiyo maana zinakuwa na outdoors za kutosha, sasa njoo huku kwetu tunaishi kwa normalcy bias tu.
 
dedication to pro ukraine.
Kupigana na Russia inabadi nchi hiyo ijipange kweli kweli, kwa sababu hata kigeografia nchi ya Russia ni kikwazo kwa adui, nchi ina fallout & ice shelters za kutosha ili kujikinga na Nyukilia ndiyo maana Putin anajihami sana dhidi ya majeshi ya NATO na nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom