NSSF yaelekea kufilisika

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,923
31,166
Wanajamvi heshima mbele,

NSSF imeanza zoezi la kuwabembeleza/kulazimisha wateja wake wakubwa [waajiri] kutoa mchango yao ya kila mwezi kabla ya wakati.Ni kawaida waajiri kupeleka michango ya kila mwezi mmoja nyuma[mfano mshahara wa mwezi tano michango yake inatakiwa ipelekwe mwezi sita],sasa NSSF inawataka waajiri wakubwa [waajiri wenye idadi kubwa ya wafanyakazi] kupeleka michango ya wafanyakazi mwezi mmoja mbele au mwezi huu wa sita ili kukabiliana na hali mbaya ya fedha inayoliandama shirika hilo la wafanyakazi nchini.

Taarifa toka chanzo cha uhakika ndani ya shirika hilo zinadai serekali imechota fedha toka NSSF kwaajili ya kugharamia mishahara ya watumishi wake baada ya chanzo chake muhimu cha mapato TRA kushindwa kupata fedha za kutosha kulipa mishahara ya watumishi wa serekali pamoja na shughuli nyingine muhimu.

Zipo taarifa za uhakika serekali ina mkakati wa kuwalazimisha wanachama wote wa NSSF na mashirika mengine ya hifadhi ya jamii kutokulipwa mafao yao hadi wafikishe umri wa kustaafu. Mkakati utasaidia kukabilia na upungufu mkubwa wa fedha unaotarajiwa kutokea kwakuwa fedha zinazochotwa na serekali hazitarajiwi kurejeshwa.

Source: Ngongo - Arusha.

Ofisi ya CAG ilisha toa report juu ya ili swala... na tahadhari juu ya kufilisika kwa NSSF.


Na Reginald Miruko - Imechapwa 18 April 2012


MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uko hatarini kufilisika na kupoteza fedha za wanachama wake.

Hii inatokana na serikali kushindwa kurejesha katika mfuko huu, mabilioni ya shilingi iliyokopa au kudhamini katika miradi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya 2010/2011, fedha za wanachama, hata katika mifuko mingine ya jamii, ziko hatarini kupotea.

Mbali na NSSF, mifuko mingine inayotajwa kuwa katika hatari hiyo ni Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF); Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu (PSPF), Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).

Kulingana na taarifa ya CAG, sehemu kubwa ya fedha za wanachama ambazo hazijarejeshwa, zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Katika chuo hiki, NSSF peke yake iliingiza Sh. 234.1 bilioni. Mifuko iliyosalia ilitoa jumla ya Sh. 181.3 bilioni.

Katika ujenzi wa UDOM, PPF ilitoa Sh. 39.99 bilioni, PSPF (Sh. 105.9 bilioni), LAPF (Sh. 22 bilioni) na NHIF (Sh. 13.4 bilioni). Fedha hizo na riba yake hazijarejeshwa.

Ripoti ya CAG, Ludovick Utouh, inasema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo, iliyochukuliwa au kudhaminiwa na serikali, ni kinyume cha sheria ya udhamini ya mwaka 1974.

"Kutolipika kwa mikopo hii iliyodhaminiwa na serikali kunaiweka mifuko hii ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha uwezo wa mifuko kufanya uwekezaji zaidi," anasema na kuongeza:

"Kushindwa kulipa madeni taasisi hizi ambazo baadhi yake zilipata udhamini wa serikali, kunatia shaka iwapo upembuzi wa kina wa wakopaji ulifanywa na mifuko ya kijamii kabla ya kutoa mikopo hiyo."

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau hakupatikana kwa maelezo kuwa alikuwa kwenye mkutano mkoani Mbeya
.
Lakini Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume amesema mikopo kwa serikali imetolewa kwa uangalifu na inalipwa bila matatizo na kwa misingi ya kibiashara.

"Mikataba ya kisheria imesainiwa kukidhi mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na iwapo itacheleweshwa…. Hakuna hatari yoyote ya fedha kutolipwa wala kupoteza fedha za wateja," amesema Chiume.

Lakini CAG katika taarifa yake ya kurasa 183, anasema, "Ukubwa wa kibiashara kati ya serikali na mifuko unatia shaka kutokana na kusuasua kwa serikali katika ulipaji madeni yake. Hii inahatarisha uendelevu wa mifuko hii."

Katika ukaguzi wake, CAG amebaini kuwa NSSF ilitoa Sh. 234.1 bilioni kwa mradi wa UDOM, lakini mkataba uliosainiwa ni wa Sh. 35.2 bilioni tu. Hii ni hatari kwa fedha za wafanyakazi na wastaafu.

Akifafanua suala la fedha kwenye mkataba kutofautiana na fedha zilizotolewa, Chiume alisema mkataba ulitakiwa kuwa mmoja ambao ulisainiwa wakati wa awamu ya kwanza.

Chiume alisema kwa awamu ya pili, kilichotakiwa ni kusaini addendum (makubaliano ya nyongeza), ambayo "yako mbioni kukamilika."

Utouh anaripoti, "Majengo kwa ajili ya awamu ya kwanza yalikamilika na kuwekwa katika matumizi mwezi Septemba 2008. Mpaka wakati wa ukaguzi 2010/2011, mfuko ulikuwa haujafanikiwa kukusanya malipo ya pango kutoka serikalini.

Kwa msingi huo, hadi sasa limbikizo la riba limefika thamani ya Sh. 14 bilioni," anasema Utouh.

Mkopo huo ulitolewa kwa utaratibu wa kubuni, kujenga, kumiliki na kuhamisha ambapo mfuko ungepokea kodi iliyokokotolewa kwa riba ya asilimia 15 kwa kipindi cha miaka kumi.

Vilevile CAG amebaini kuwa majengo yaliyojengwa kwa mkopo huo, hayako kwenye vitabu vya UDOM wala katika vitabu vya NSSF, kutokana na uelewa tofauti uliopo kati ya pande mbili zinazohusika.

Kuna mikanganyiko katika uelewa kwa serikali na mifuko ya hifadhi, ameeleza CAG. Wakati mifuko inasema fedha zilizotumika kujenga majengo hayo zilikuwa mikopo kwa serikali, yenyewe serikali inadai fedha hizo ni uwekezaji wa kawaida wa mifuko hiyo.

Mbali na UDOM, serikali pia haijalipa jumla ya Sh. 19.77 bilioni zilizotumika katika ujenzi wa ukumbi wa bunge, ambazo hazilipwi kulingana na makubaliano. Hadi wakati wa ukaguzi, NSSF ilikuwa inadai Sh. 8.96 bilioni, PPF (Sh. 7.9 na LAPF Sh. 2.91.

Pia upo mkopo mwingine wa NSSF wa Sh. 5.33 bilioni na riba ya asilimia 15 kwa miaka kumi, uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa "taasisi ya serikali ya kiusalama" mwaka 2007.

Mfuko mwingine uliowekeza katika mradi huo ni PSPF uliotoa Sh. 6.4 bilioni.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, NSSF kwa udhamini wa serikali ilikopesha taasisi kwa shughuli mbalimbali.

Kwa mfano, ujenzi wa nyumba za polisi kwa Sh. 20 bilioni na Sh. 12. 9 bilioni kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 kwa ajili ya ujenzi wa Machinga Complex, Ilala.

"Hadi sasa hakuna malipo ya riba wala sehemu ya mkopo hiyo yaliyofanywa. Hii ni kinyume cha mkataba," inasema sehemu ya ripoti ya CAG.

Kwa upande wa Machinga Complex, hadi tarehe 30 Juni 2011, mkopo na riba yake ulikuwa umefikia Sh. 15.3 bilioni.

Ripoti ya CAG imeainisha pia mikopo mingine ambayo hailipwi kulingana na mikataba ya mifuko hiyo, bila ya kutaja viwango vyake.

Mikopo hiyo ni iliyotolewa kwa Continental Venture (T) Limited, Meditech Industrial Co. Ltd, General Tyre (GT), Kiwanda cha Sukari Kagera, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio amesema hajaona ripoti ya CAG na yuko safarini Tanga.

Hata hivyo amedokeza kuwa hivi karibuni walikaa na CAG kujadili suala hilo na kubaini makosa ya kifundi katika uhasibu baina ya mifuko na serikali katika ujenzi wa UDOM; hivyo CAG kuahidi kuyashughulikia kwa upande wa serikali.

Alipoulizwa ni makosa yapi hayo, Erio alimtaka mwandishi awasiliane na kaimu wake, Stephen Alfred ambaye ilielezwa kuwa yuko kwenye mkutano. Hadi tunakwenda mitamboni, Alfred hakupatikana.

Updated

Chini ni waraka uliotolewa na TAMICO Kupinga hili swala...
Tafadhari fuatilia hapo chini... na tungojee hatua zinazofuatia..





Comrades,
viongozi wa matawi ya Tamico,wanachama na wafanyakazi wote.
YAH:KURA YA MAONI KUHUSU MAREKEBISHO YA SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA 2012:
Rejea mawasiliano yetu ambayo tumekuwa tukiyafanya tangu ilipojitokeza taharuki kwa wafanyakazi wa sekta binafsi hususani wafanyakazi wa Migodi kutokana na uvumi wa kuwepo kwa marekebisho ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya 2012.
Kwa waraka huu napenda kukufahamisheni kwamba wafanyakazi wameamua kupiga kura ya maoni juu ya mabadiliko ya sheria hii ili waamue wenyewe kama wanaitaka au hawaitaki.Baada ya kupiga kura hii ya maoni,TAMICO tutapeleka maombi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kama sheria ameshaisaini apeleke Muswada wa marekebisho Bungeni na kama hajaisaini airudishe bungeni mara moja kwa ajili ya marekebisho ya kipengele ambacho kimeleta mtafaruko.
Katika marekebisho hayo tunahitaji kuona Kipengele cha kuzuia mfanyakazi kuchukua mafao yake apoacha kazi mpaka afikishe umri wa miaka 55 kikiondolewa mara moja kwani kinakandamiza maslahi ya mfanyakazi mnyonge wa nchi hii ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akichangia mapato ya nchi hii kupitia kodi kubwa anayokatwa.
Tunaomba zoezi hili lifanyike kwa haraka sana ikiwezekana Jumanne tarehe 24 Julai liwe limekamilika ili kukipa nafasi chama chenu cha wafanyakazi TAMICO kuwasilisha rasmi maombi hayo kwa Mheshimiwa Rais wetu.Kwa hiyo kupitia karatasi hizo zilizoambatanisha tafadhali wapeni wafanyakazi wapige kura hiyo ili waamue wenyewe wanachohitaji juu ya suala hili.


Tumeamua kuitisha Kura ya maoni baada ya kubaini mgongano wa kauli kutoka kwa mamlaka husika juu ya suala hili.NSSF na PPF wao wamekanusha kwamba sheria hii haipo na wataendelea na utaratibu wa zamani kulupa mafao hayo,SSRA wao wana kauli mbili tofauti,moja wanadai sheria ilishasainiwa tangu mwezi wa sita 2012,kauli ya pili wanadai imesainiwa mwezi huu.
Waziri wa kazi na Ajira yeye amekaririwa na Mbunge mmoja akidai kwamba sheria haijasainiwa na mheshimiwa Rais.Sasa kwa kauli hizo tata tumwamini nani yuko sahihi au tuamini uvumi kwamba serikali imeamua kutunga sheria hiyo ili iendelee kukopa pesa za wafanyakazi kutoka mifuko hiyo baada ya hata pesa ilizokopa awali kushindwa kuzirejesha inavyotakiwa.kwa hiyo wanataka kutugeuza shamba la bibi halina uchungu.
Sababu ya pili ni matumizi ya sheria yenyewe ukisoma marekebisho hayo katika kifungu cha 43 (6) nanukuu "This act shall apply to a person or employee employed in the formal or informal sector or self-employed in the mainland Tanzania and shall not apply to a person who has been insured or registered under any other law".
Hii inamaanisha kwamba sheria hii haitawahusu wabunge,viongozi wakuu wastaafu wa nchi na kadhalika.Kwa hiyo mbunge akimaliza miaka yake mitano anachukua mafao yake kilaini,na ndo maana wakaipitisha sheria hii kwa mbwembwe nyingi na makofi ya kwaa ! kwaa! Kwaa! Kwa kugonga meza maana walijua haiwahusu.kwa kufanya hivyo wametusaliti sisi wafanyakazi ambao tunawalipa posho na mishahara kupitia kodi tunayokatwa moja kwa moja.
Wito wetu kwao ili tuendelee kuwaamini inabidi warekebishe haraka sheria hii vinginevyo watakuwa wamepoteza legitimacy(uhalali) wa kutuwakilisha.Wakumbuke kuwa sisi ndo waajiri wao hivyo wanatakiwa kufuata Job description tuliyowapa ya kutetea masilahi ya wananchi na wala sio kutukandamiza.Ni bora tusiwe na wawakilishe kabisa kuliko kuwa na wawakilishi wanaotumika kukandamiza masilahi ya wapiga kura wao.

Zoezi hili la kura ya Maoni ni la siku mbili yaani leo Jumatatu pamoja na kesho Jumanne halafu jumatano maoni hayo yatahitajika kwa haraka yatufikie tutawapa viongozi utaratibu wa kuyaleta maoni hayo kwetu.Vilevile kesho tutawafahamisha viongozi wa matawi nini cha kufanya baada ya maoni hayo.
Hakikisheni Karatasi za maoni zinapelekwa kila Idara kupitia kwa wafanyakazi au mtu yoyote wa kuaminika ili zoezi liende haraka.Angalizo naomba maoni hayo yasiingilie muda wa kazi wa mwajiri ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.Tumieni muda wa Chakula,Change shift NK kukamilisha zoezi hili.
Mwisho nawatakia umoja na mshikamano katika kufanikisha zoezi hili kwani nguzo yetu pekee sisi wafanyakazi ni Umoja na Mshikamano.Na tukishikamana kwa pamoja haki zetu hazitagandamizwa wala kuchezewa kwa jinsi yoyote.Tuonyeshe mfano kwa hili maana sauti ya wafanyakazi ni sauti ya wana wa nchi waliojitolea kutumikia Taifa lao.
SI MCHEZO (IS NOT A JOKE) KAA MKAO WA KULA MAANA SAA YA UKOMBOZI WA MASILAHI YETU NI SASA.PIGA KURA YAKO UOKOE MASILAHI YAKO NA YA WENGINE.
SOLIDARITY FOREVER,
Amandla,
Benjamin Daudi Dotto
Katibu wa Tamico wilaya ya Geita,
SLP 335,
Geita – Tanzania.
Simu: ofisi +255 774 866635
Simu:mkononi + 255 767 715116 alt.+255 784 715116
Barua pepe: tamicogeita@gmail.com au mwanadotto@gmail.com

 
Hata mimi nimeisikia hiyo lakini mimi nakuwa na wasiwasi na hii issue kama itafanikiwa, je kama mimi mpango wangu labda ni kufanya kazi miaka mitano halafu naachana na kazi ya kuajiriwa naanza ujasiriamali kwa say labda nimeacha nina miaka 32 kwa hiyo itabidi nisubiri hadi nifike miaka 60 ndo nilipwe hela yangu?
 
Ni kweli NSSF iko taabani lakini sababu ni nyingi moja kubwa ni hili swala la kugharamia uendeshaji wa serekali lingine ni miradi yake mingi haina tija na kujikuta fedha zake nyingi zikipotea bure.Mradi wa ujenzi wa UDOM umechota fedha nyingi wakati hata mkataba haujasainiwa,miradi ya majengo mengi ni kwaajili ya ulaji wa wakubwa.Chama cha wafanyakazi wa sekta mbali mbali yafaa waungane kupinga uonevu wa wafanyakazi unaandaliwa chini ya mwavuli wa kuficha utawala mbovu wa serekali ya CCM.
 
Mkuu Masuke kama sheria itabadilishwa maana yake itabidi usubiri hadi utakapofikisha miaka sitini.Hapo hapo lazima utie akili wastani wa umri wa mtanzania ni chini ya hiyo miaka sitini ?.Jiulize serekali ina mpango gani na wafanyakazi wa nchi hii.

Hata mimi nimeisikia hiyo lakini mimi nakuwa na wasiwasi na hii issue kama itafanikiwa, je kama mimi mpango wangu labda ni kufanya kazi miaka mitano halafu naachana na kazi ya kuajiriwa naanza ujasiriamali kwa say labda nimeacha nina miaka 32 kwa hiyo itabidi nisubiri hadi nifike miaka 60 ndo nilipwe hela yangu?
 
Duh siasa za ccm kweli za ajabu, juzi kwenye mkutano wao kule jangwani wanasema Daraja litaanza kujengwa mwaka huu na NSSF ndo wamepewa hio kazi ya kutoa nusu ya gharama za mradi, kule Kiwira wanatakiwa wazalishe umeme 200 megawatt, kuondoa Mgao wa umeme na NSSF walipewa kazi hio, sijui UDOM kama NSSF wamemaliza kujenga na majengo yanavuja! Kweli ccm ni DHAIFU, "JJ Mnyika Ukweli ni Uhuru"
 
Na Mkurugezi si walimsifu sana wenzetu na wakasema anatungiwa sheria ili atoke, Duh! hii ni aibu, na Udhaifu mkubwa sana, Linamfia na utetezi wake wa kibaguzi
 
ikifikia serikali ikaanza kutumia fedha za wafanyakazi kwa miradi yake na mishahara Ngongo unategemea NSSF ittacha kufilisika ,halafu TUCTA wamekaa wakichekacheka nao makubwa
 
Ni wezi wakubwa vitega uchumi vyote wanakula pesa mipesa yetu tunaweka haiji na riba wakati wao wanafanyia biashara
Na mbaya zaidi huwezi kupewa pesa hatu mgongo uwe umepinda si adhabu hii!!Basi watoe kariba fulani kwa wateja wao angalau ionekane unajaliwa wao wanajinadi na pesa ya mazishi na wao wafiwe tukawape pesa zakuzikia,na pesa ya mamamjamzito!!wehu kweli na ni majangili siyo majambazi!!
 
Mkuu Froida,

Mkuu wangu hili zoezi lilianza wiki ilipita hapa Arusha maafisa NSSF wamezunguka kampuni zote zenye wafanyakazi zaidi ya 20 na kuendelea.Bahati nzuri maafisa wa NSSF walipokuja ofisini kwangu nilipata wasaa wa kuhojiana nao na wakanieleza ni zoezi la Tanzania nzima ingawa linafanywa kwa siri na kwa uangalifu mkubwa.

Fedha za NSSF ni kama shamba la Bibi hakuna uwazi wa kutosha,hakuna uangalizi wa kutosha,hakuna uadilifu.NSSF ni sehemu ambayo wanasiasa wanachota fedha hovyo kwa faida za kisiasa[miradi ya kisiasa eg daraja la kigamboni & UDom].Wafanyakazi [wadau au ukipenda wanahisa wakuu] hawana mwakilishi halisi ndani ya bodi ya shirika wajumbe wote wa bodi ni wateule wa waziri wa kazi na mwenyekiti ni mteule wa Rais.

Hakika tungewapata wanasiasa aina ya Mch Mtikila au wanasheria mahiri ningefungua kesi mahakama kuu kupinga fedha zangu kuchukuliwa kwa nguvu na kutokuwa na msimamizi mwenye uakilishi wa wafanyakazi.


ikifikia serikali ikaanza kutumia fedha za wafanyakazi kwa miradi yake na mishahara Ngongo unategemea NSSF ittacha kufilisika ,halafu TUCTA wamekaa wakichekacheka nao makubwa
 
Mkuu Masuke kama sheria itabadilishwa maana yake itabidi usubiri hadi utakapofikisha miaka sitini.Hapo hapo lazima utie akili wastani wa umri wa mtanzania ni chini ya hiyo miaka sitini ?.Jiulize serekali ina mpango gani na wafanyakazi wa nchi hii.
Sijui niache kazi kabla hakijanuka maana mwaka huu ni wa mwisho nijiajiri sasa nikisubiri si itakula kwangu.....
 
Ni kweli NSSF iko taabani lakini sababu ni nyingi moja kubwa ni hili swala la kugharamia uendeshaji wa serekali lingine ni miradi yake mingi haina tija na kujikuta fedha zake nyingi zikipotea bure.Mradi wa ujenzi wa UDOM umechota fedha nyingi wakati hata mkataba haujasainiwa,miradi ya majengo mengi ni kwaajili ya ulaji wa wakubwa.
Yes, absolutely, serikali kuchota fedha is only a tertiary reason for the NSSF books being the red, but primarily the core investment projects are misguided and incompetent.

NSSF imejiingiza kwenye miradi ya kujenga madaraja ya angani, sijui mara wanajenga mall la Wamachinga, mara sijui Chuo Kikuu, jamani, NSSF ina investment and financial expertise gani zaidi ya kukusanya hela za watu na kuwaorodhesha majina kwenye ma kaunta buku?

Kingine, uongozi wa NSSF hauko under pressure ya kutoa results, hakuna anaejali performance ya uongozi, ukishateuliwa wewe ndio CEO wa NSSF basi ndio imetoka, tena huwa wanafanya party, halafu una relax, kazi kutembea kwenye vijiwe vya vilabu vya PAN AFRICA kupiga picha na wachezaji wa zamani, lazima ubweteka!

rd.jpg
 
Sijui niache kazi kabla hakijanuka maana mwaka huu ni wa mwisho nijiajiri sasa nikisubiri si itakula kwangu.....

Shemeji hata ukiacha, kwa jinsi utakavyopata usumbufu kufatilia hiyo pesa mpaka utakasirika,nimeteseka kufatilia mafao ya uzazi, nikisikia mtu anaongelea habari za NSSF nasikia vibaya sana.
 
Shemeji hata ukiacha, kwa jinsi utakavyopata usumbufu kufatilia hiyo pesa mpaka utakasirika,nimeteseka kufatilia mafao ya uzazi, nikisikia mtu anaongelea habari za NSSF nasikia vibaya sana.

Shemeji mbona unanitisha hiyo NSSF naitegemea eti baada ya kuacha kazi karibuni sasa kama ni kimbembe kuipata unanifanya nichanganyikiwe na nizidi kuichukia zaidi serikali ya CCM....hivi chama cha wafanyakazi kiko wapi au wamesha katiwa chao..............
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom