NMB na TANESCO ninaomba maelezo

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,066
Nimekuwa nikinunua umeme wa luku kwa kutumia NMB mobile account.Kuna wakati nimekua napata maelezo yanayonionyesha voucher ya umeme nilionunua lakini bila kupata message ya NMB.Imani yangu ilikuwa kama hakuna NMB message basi na makato hayakufanyika,leo nimegundua ya kuwa makato yanakatwa.
Naomba NMB na TANESCO watuelimishe kuhusu hili,je fedha zangu nitazipata vipi?
 
Pole sana mkuu. Tanesco wamemwajiri NMB na wewe ni mteja wa NMB. Kwa vile umenunua product ya Tanesco through employee wao (NMB) maelezo unayo taka NMB ndio wanatakiwa kujibu. Usijisumbue kwenda Tanesco bcoz huku nunua umeme kwa moja kwa moja kwao. Pambana na huyo agent wa Tanesco ambaye ni NMB.
 
Piga simu call center ya NMB Mobile wakusaidie, ni kitu kidogo sana, ila kwa uwakika kwanza kapate statement ya accaunt yako ili ujue nilini ulinunua na akupata umeme na waka kata hela.
 
Sijaelewa kidogo, huo ununuzi uliufanya wewe au haukuufanya? Na hizo voucher ulizidumbukiza kwenye LUKU au haukuzidumbukiza?
 
FEEDBACK!
Wadau, nashukuru kwa ushauri wenu na naona niwajulishe maendeleo ya jambo hili.
Nilikwenda branch ya NMB nao wakanihakikishia kuwa pesa zimekatwa kwa ajili ya LUKU na wakanishauri niende ofisi ya Tanseco.
Leo saa saba kasoro dakika ishirini nikawakilisha malalamiko yangu na kutoa namba ya LUKU na jina,baada ya masaa mawili nikapata voucher number ya umeme niliokatwa pesa.
ANGALIZO:Unapotumia NMB mobile au ATM tafadhali uliza kwanza salio lako.Naamini watu wengi wamepoteza pesa zao kwani bila kufuatilia sidhani kama Tanesco wangenipatia umeme.
 
Back
Top Bottom