NMB BANK: Mikopo yenu kwa wastaafu haina tofauti na ile ya kausha damu

MtuHabari

JF-Expert Member
Oct 16, 2020
321
1,019
Bank ya makabwela ambayo wastaafu hasa wale wa zamani serikalini walilazimika pension zao kulipiwa katika bank hiyo inawaumiza sana watumishi hao wastaafu kwa kuwanyonya kupitia mikopo yao ambayo wameitengeneza kwa mfumo wa ile Kausha damu ya mitaani.

Bila huruma kwa wazee hao ambao wanapokea pension ndogo sana kutokana na pension set up ya miaka hiyo wanajikuta wakiomba mikopo katika mpango ulio andaliwa na NMB Bank kwa hao wastaafu. Lakini hiyo mikopo sio yenye nia ya kuwasaiddia wazee hao bali kuwanyonya visenti vyao tuu.

Inakuwaje mzee akope milioni mbili uweke vipengele vingi vingi hadi anajikuta anarudisha deni kwa kulipa mikioni zaidi ya tano?

NMB hebu kuweni na huruma na hawa wazee ambao wengi hako ka pension ni kadogo mno na ndio mategemeo yao.
 
NMB haitendi haki ni wezi wakubwa, ukienda ku top up mkopo, wana clear deni kwa mkopo mpya ila ile riba wanaiacha yaani wanaihamisha.

Unabisha njoo nikupe details zangu uende ukahakiki

Wamenenepa tu hovyo hovyo , acha bp na sukari ziwakomeshe, wezi nyie.
 
Ni deni la miaka mingapi ? Isije kuwa deni la miaka 8
Unaweza kuta ni miaka mitatu au mitano tuu.
Nijuavyo ule mpango wa Pensionable loans ulikuwa maalum katika kupunguza makali ya maisha ya wazee wastaafu na sio ya kibiashara kama mingine.
Sasa unakuta wapo wazee wana miaka 70 wanapokea monthly laki moja hadi mbili halafu wanamkamua hivyo na ni bank inayopewa facilities kibao na serikali zinazoibust kupata faida kubwa kuliko bank nyingine.
NMB wakae haraka na ku review msaada kwa wazee hao waliotumika kwa kwa maendeleo ya nchi ikiwamo hata hiyo bank.
 
Ile ni bank sio taasis ya misaada, kama wazee watasaini mkataba wa muda mrefu watapigwa tu, and after all riba ni za kawaida tu, 15-20
 
BANKS Nyingi Ni Majizi Ukipewa Mkopo Lazima Ukate Cha Juu Kwa Afisa Mikopo
Tazama Riba Kubwa Mpaka Unajuta, Tanzania Kila Eneo Shida Sana
Tena Hao Wa Topup Ndiyo Wanapigwa Wanachakaa Mno
 
NMB haitendi haki ni wezi wakubwa, ukienda ku top up mkopo, wana clear deni kwa mkopo mpya ila ile riba wanaiacha yaani wanaihamisha.

Unabisha njoo nikupe details zangu uende ukahakiki

Wamenenepa tu hovyo hovyo , acha bp na sukari ziwakomeshe, wezi nyie.
Dah....
 
Kuna wizi wa riba unaendelea kwenye hizi Bank.
Wateja walio kopa wanalia sana kuhusiana na riba wanazo tozwa.
 
Mabank ya Tanzania hayana huruma na mteja hakuna kitu Cha Bure hata kimoja
Mmnlisha achana na kukopa bank nimejiunga zangu kwenye Saccos imara yenye mtaji wa 14Bl
Na enjoy tu life siwaz Kausha damu Wala nini
 
Inaitwaje hiyo saccos? niko nje ya nchi naweza kujiunga?
 
Kila wakiambiwa wanawaona waislam kua primitives huku wao wakijiona kua ni modern
Lakini hii mikopo ujue haina tofauti sana , ukifanya mikopo ya kawaida ya riba sema utawekewa riba ya 14% , uka chukua islamic loans watakupa nyingi zinakuwa cost mark up ambayo ni sawa tu na 14%, kwahiyo mkopo wa kawaida utaanza lipa principal na riba ambayo kama ulichuku 10M na inabidi ulipe 18M basi utalipa kidogo kidogo mapaka utafikia hicho kiasi ila ukija islamic wewe utaanza lipa 18M ikipungua.
 
Najua nao wanazunguka zunguka tu
Bank ni wizi uliohalalishwa ndio maana hawamkopeshi masikini
Wanamfuata mwenye nacho ndio wamkopeshe
 
Najua nao wanazunguka zunguka tu
Bank ni wizi uliohalalishwa ndio maana hawamkopeshi masikini
Wanamfuata mwenye nacho ndio wamkopeshe
Bank hukopesha pesa wanazoleta wateja kuweka akiba sasa wewe utakubaali kuambiwa akiba yako imepotea kwasababu alikopeshwa masikini asiyeweza kurejesha
 
Back
Top Bottom