Nkya: Serikali inashindwa kuwalipia Watoto Bima kwa Bilioni 35 ila Viti Maalum wanalipwa Bilioni 200

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202

View: https://www.youtube.com/watch?v=Cw8PMRtKD5A
WhatsApp Image 2024-03-08 at 17.45.15_3b6281d1.jpg

WhatsApp Image 2024-03-08 at 17.57.12_78ca7164.jpg

WhatsApp Image 2024-03-08 at 17.57.14_36ad40fc.jpg

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, leo Machi 8, 2024, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kinaadhimisha siku hiyo kwa kufanya mjadala unaohusu "Uongozi na maamuzi ni haki ya Wanawake tuwape fursa".

Mjadala huo unajadili masuala mbalimbali ambayo yanaongozwa na wawasilisha mada wabobezi kwenye mada husika, ikiwemo masuala ya uchaguzi, Wanawake katika Vyombo vya Habari.

FB_IMG_1709900696536.jpg

Sehemu ya wazungumzaji
Mwanaharakati wa Haki za Wanawake amabaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Gemma Akilimali: Akiwasilisha mada kwenye mjadala huo uliondaliwa na LHRC, amesema kuwa wanapendekeza Viti Maalumu vifutwe ili Wanawake kwa kuwa imefika wakati ambao Wanawake wanaweza kusimama wenyewe kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi.

Amesema Viti Maalumu vinaweza kuwadumaza Wanawake kimtazamo kama vinaendelea kuwepo, amesema vimekuwa vikitazamwa kwa mtazamo tofauti usio wa kiushindani.

Hata hivyo, ameshauri kwenye mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi kuzingatiwa kwa masuala ya kijinsia kama wadau mbalimbali ambavyo wamekuwa wakishauri, amesema mazingira rafiki ya kijinsia yatawavutia Wanawake wengi kushiriki kwenye michakato ya kisiasa.

Mkurugenzi TAMWA, Dr. Rose Reuben: Akichangia mjadala kuhusu Vyombo vya Habari katika kukuza jitihada za Wanawake, amesema Vyombo vya Habari ni nyenzo muhimu katika kuibua na kukuza juhudi za Wanawake kwa sababu ndivyo vimekuwa vikioneshe vitu mbalimbali ambavyo vimekuwa vikifanywa na Wanawake

Amesema Vyombo vya Habari vimekuwa vikiwapa nafasi Wanawake na kuwapa nafasi za kuonesha walichonacho pamoja na kuwajengea ujasiri.

Ameongeza vimekuwa na mchango wa kuhamasisha Wanawake katika uongozi na masuala ya kisiasa, ambapo ameendelea kusisitiza Wanawake kutumia vyema vyombo vya habari kuonesha uwezo wao wa kiongozi na kwenye masuala mengine.

WhatsApp Image 2024-03-08 at 17.57.15_1349189f.jpg

WhatsApp Image 2024-03-08 at 17.57.15_640e55a2.jpg


Wakili Fatma Karume: Sheria bado hazijaweka mfumo rafiki kwa Wanawake kuingia kwenye siasa
Wakili Fatma Karume: Akizungumzia masuala ya Kisheria yanayomgusa Mwanamke, amesema kuwa Sheria bado hazijaweka mfumo rafiki kwa Wanawake kuingia kwenye siasa.

Ameongeza kuwa licha ya Katiba kutambua ushiriki wa Wanawake katika nafasi mbalimbali za Kisiasa hususani Ubunge, lakini amesema bado hata Wanawake ambao wamekuwa wakichaguliwa kwenda kwenye nafasi za kimaamuzi hasa Bungeni bado hawajapigania ipasavyo mabadiliko ya kimfumo ambayo yanaweza kuchochea Wanawake wengi kuingia kwenye siasa.

Ameshauri kuwa zinapotungwa Sheria lazima ziwazingatie Wanawake. Lakini amesisitiza kuwa kama Wanawake wanahitaji fursa za kisiasa hawana budi kuwekeza jitihada kuzitafuta bila kungoja waletewe fursa hizo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Jukata, Dkt. Ananilea Nkya
NKYA: TUPIGANIE VITI MAALUM VIONDOKE, HAVIWASAIDII WANAWAKE
Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Dkt. Ananilea Nkya amesema utaratibu wa Viti Maalum katika medani ya Siasa umekuwa ukichangia uvunjifu wa #Katiba kutokana na kukoseka kwa hadhi sawa na Uwajibikaji.

Amesema hayo wakati akichangia mada katika maadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2024, yaliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Jijini Dar es Salaam, akidai fedha za kuwalipa Viti Maalum zingeweza kutumia kwa maendeleo ikiwemo kuboresha Huduma ya Afya.

Amesema “Viti hivyo vikiondolewa vyama vitawajibika kuwaandaa wagombea wote bila kujali ni Mwanamke au Mwanaume."
 
Back
Top Bottom