WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Tanzania, nchi yangu niipendayo kwa moyo wangu wote. Ndio maana hadi leo pamoja na kutembelea nchi nyingi za wenzetu na kuona mengi ya kutamanisha, bado nimekomaa hapa hapa na sina mpango kuikimbia nchi yangu pamoja na matatizo yake yote. Nina imani bado kuwa iko siku itageuka na kuwa paradiso yenye kutamaniwa na walimwengu!
Tanzania, nchi yangu iliyonilea na kunipa tumani jema. Najisikia mnyonge sana pale ninapotazama utajiri wa mali na rasilimali tulizopewa na Mwenyezi Mungu, Jinsi mali hizi zilivyobakia kama maua mazuri yaliyochorwa daftarini tu Maua ambayo ni picha nzuri kutizamwa lakini haina maana kwa sababu ya kukosekana namna nzuri ya kumfanya kila mtu afaidike na utajiri huu.
Tanzania, nchi yangu ya ajabu na maajabu. Ninashindwa kuelewa tumemkosea nini Rabuka hadi tujikute katikati ya rindi la dhiki na umasikini ilhali Muumba katusheheni na utajiri wa almasi na lulu Tumekosea wapi hadi tusiione thamani ya neema inayotuzunguka? Najua na wewe wajua kuwa sote ni wana wa Tanzania. Najua nawe wajua kuwa Tanzania ni yetu wote. Nafahamu nawe wafahamu kwamba njaa haichagui wala haibagui.
Naamini ila sijui kama unaamini kwamba "uhai" wetu na vizazi vyetu tumekabidhi mikononi mwako ewe kiongozi uliyechaguliwa na wananchi. Uongozi ni dhamana na siyo ufahari. Uongozi ni dhamana inayotisha na siyo kulewesha. Uongozi ni mzigo na siyo lelemama. Iweje dhamana hii isikuogofye ewe kiongozi? Iweje isikunyime usingizi ewe mwakilishi wangu niliyekuchagua kwa kura yangu? Iweje ujisahau na usahau ahadi zako lukuki ulizomwaga siku unakampeni?
Ahadi ni deni na hivyo basi ujue unadaiwa! Dawa ya deni ni kulipaHakuna jinsi nyingine. Usipolipa wewe leo ujue kizazi chako kitadaiwa hata mbele ya Mungu! Ninaotea kwamba kiongozi wangu ajaye ameshajionea mengi kwa waliotangulia. Amesikia malalamiko na vilio vya wanyonge wa Tanzania.
Ninaamini kabisa kwamba anajua ufahamu wa watanzania ni mkubwa kuliko enzi zileeeeeeeeeeeeeeeeee Ninaamini kwamba watanzania nao "wamefundishika" vya kutosha mpaka hapa tulipofiikia. Natamani kiongozi ajaye awe mwenye uchungu na maskini wa Tanzania wasiokuwa na makazi ya staha...( nyumba bora), wanaoshindia mlo mmoja kwa siku, waliokosa tumaini la kuiona kesho.
Awe mwenye hofu ya Mungu Awe mwenye kupima ufanisi wa wale anaowateua kwa kipimo kinachoeleweka. Hili siyo shairi wala ngonjera bali ni mawazo yangu yanayonijia kila nikitafakari kuhusu nchi yangu Tanzania. Msinizodoea kwamba mbona hakuna vina na mazagazaga mengine.
Mwenye njozi zake naye amwage hapa ili baadae tuchanganye ................. wanaosikia wasikie. Kuna msururu wa wanaotaka urais 2015. Tunataka watusome wajue 2015 siyo lelemama. Hatutadanganyika kwa maneno yale yale ya enzi zileeeeeee, Tutajipanga sana na kuwabana.