Njia za uhakika za kufanya biashara mtandaoni ili kuongeza kipato

muvika online

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
375
283
Hivi sasa teknolojia imekua ndio kila kitu hakuna mahali unapitia pasipo kutumia teknolojia, hiyo inadhirisha kuwa uwezekano wa kufanya biashara mtandaoni ni mkubwa sana cha msingi ni kujua ni vitu gani vya kufanya ili kuweza kuongeza kipato chako.

Kwa kuanza basi ni vyema nikwambie kabisa kuwa kama unataka kufanya biashara hizi mtandaoni, kama zilivyo biashara nyingine zinaitajika uwe mvumilivu na uwe unapenda kitu unachofanya tena ni vyema kutokufikiria pesa kwanza fanya kwanza unachokifanya kisha pesa itakuja baadae, kwa njia hiyo utaweza kufanya kitu hicho kwa uhakikia na bila kusimama au kuacha.
  • Fungua Blog au Tovuti
Katika swala zima la kufungua blog au tovuti hapa ni mahali muhimu sana pakuzingatia kwani watu wengi huanzisha blog na baadae kuacha sababu tu mambo yamekua magumu au muda umekua mchache wakati mwingine unakuta mtu alifungua blog ya kitu asichokipenda au sababu aliona mtu mwingine alifungua blog ya aina flani na akafanikiwa.

Cha msingi hapa ni kutafuta kitu ambacho unakipenda kwa asilimia 100 na ukifanye bila kutegemea chochote kile kwani matokeo hua badae kabisa na inategemea na kitu unachokifanya na jinsi unavyo kifanya.
  • Fungua Youtube Channel
Youtube ni mtandao ambao kujiunga ni bure kabisa, lakini pia ni sehemu ya kutengenezea pesa kama utakua unafanya kitu chenye mvuto kwa jamii pamoja na watu unaotaka kuwagusa kutokana na aina ya channel ambayo umefikiria kutengeneza.

Kwa hapa Tanzania kifupi ni kwamba watumiaji wa mtandao huo hawako wengi sana hivyo ni vizuri kufanya kitu ambacho ni bora kwa watu na kitavutia jamii kwa asilimia 100, hii pia inategemea na aina ya kitu unachofanya pamoja na ubora wa kitu unachofanya kumbuka pesa huja baadae hivyo fanya hivi kwa subira.
  • Fanya Biashara ya Kutafuta Masoko (Online Marketing)
Kuna watu wengi sana wanafanya au wanafikiria kufanya matangazo kupitia Instagram, Facebook, Twitter, Google pamoja na Youtube watu hao wengi wao hawajui cha kufanya hivyo ukianzisha biashara ya mtandaoni ambayo itakuwa inahusika na kufanya matangazo kwenye sehemu hizo basi hakika utafanikiwa kwa namna moja ama nyingine.

Kufanya biashara hii unatakiwa kujitengenezea jina zuri pamoja na kuonyesha kwanini watu wakuchague wewe, hivyo ni vizuri kutumia muda wako kujijengea jina kwanza kabla ya kuanza kufanya biashara hii kwa hiyo pia biashara hii inaitaji subira.
  • Fanya Kazi ya Kutafutia Kampuni Wateja (Affiliate)
Affiliate ni njia inayofahamika sana ya kufanya biashara mtandaoni kuna kampuni nyingi mtandaoni ziko tayari kutoa asilimia flani kutokana na wewe kumleta mteja mmoja, kuna mpaka kampuni zingine zinatoa asilimia 40 ya kipato kinacho patikana kwa mteja ulio mleta. Kufanya biashara hii unaitajika kuwa mtaalamu kidogo wa masoko na uwe na mtandao mkubwa wa watu ambao utaweza kuwa shawishi kununua bidhaa hizo ili kusababisha wewe kupata kamisheni.
  • Tengeneza Akaunti za Mitandao ya Kijamii
Una njia imeingia sasa hasa kwenye mtandao wa Instagram njia ni yakutuma matangazo mbalimbali ya biashara kwenye akaunti mbalimbali, njia hii ni nzuri kama utakuwa umetengeneza akaunti ya kitu ambacho unakipenda na uhakikishe una weka makala mpya kila siku ili kuvutia follower wengi kwenye akaunti zako.

Hakikisha ununui follower kwa namna yoyote ile acha watu wakufuate wenyewe kwani akaunti nyingi zilizo nunua follower unakuta mtu ana post picha wana like watu 1000 wakati akaunti hiyo ina follower zaidi ya watu laki mbili, hapo unakuta hao 1000 ndio wenye kufuata page yako kutokana na kitu unachokifanya. Hivyo ni muhimu kufanya kitu unachokipenda na acha watu wakufollow wenyewe hapo utapata wateja wengi.
  • Nunua na Uza Vitu Mtandaoni (Buy and Sell)
Kuna mitandao mingi hivi sasa ya kukupa uwezo wa kuuza vitu, unaweza kununua kitu kipya kisha ukakiuza kwenye mtandao au kama una kompyuta, simu au kitu chochote ambacho unaona huna matumizi nacho unaweza ukaanza kwa kukiuza kisha ukanunua tena na kuuza kwa faida.

Njia hii ni njia rahisi na inahitaji kuwa makini pale unapo nunua usije kununua kitu kibovu kwani biashara yako ndio inayotegemea, kuwa mvumilivu na hakikisha unafanya kwa umakini na ustarabu mkubwa sana ili kuongeza wateja kwenye biashara yako, pia hakikisha utafuti faida kubwa kwani hiyo itawafanya watu kuona ni bora waende dukani kuliko kununua kitu hicho kwako.

Hizo ni baadhi ya njia ambazo ukweli zinaweza kukusaidia kupata kipato na ukifuata kwa umakini utafanikiwa kwa asilimia 100, ukweli ni kwamba ukifanya unachokipenda lazima pesa na mafanikio yatakuja kwani utakifanya kwa ustarabu na umakini wa hali ya juu kwa sababu unakipenda utaki kuona kitu hicho kipo ovyo. Hakikisha unafuata ndoto zako na anza kufanya sasa

========


Kuna uhaba wa ajira sana nchini jambo ambalolinapelekea vijana wengi kukosa ajira na mitaji japo wana elimu ambayo wanaweza kuitumia na wakatengeneza pesa zaidi hata kuliko ambayo wangelipwa.

Internet ni fursa nzuri sana ya kutengeneza pesa na wengine wajikita kote mfano bloging and youtube monetization kupitia adsense na wengine kama propellar ads.

Njia hizi siyo rahisi na siyo kila mmoja anaweza kufanikiwa maana pia na mimi nilijaribu nikaishia kuwa natumai nguvu nyingi naishia kupata ela ndogo kabisa na muda mwingine ninakosa kabisa.
Ila nikaja na njia zangu ambazo zimenilipa na kwa sasa niko comfortable nazo.

1. Freelancing
2. Dropshing
3. Affiliate Marketing

Freelancing
Kuna mitandao mingi ya freelancing ila Upwork.com, freelancer.com. na Fiverr kwangu ndiyo the best. Freelancer ni rahisi kujiunga haina limitations na ukishajiunga utaanza kubid kazi moja kwa moja. Inaweza kukuchukua hata bids 50 mpaka upate kazi ya kwanza. Ukipata kazi mtaelewana na mteja wako atatengeneza kitu kinaitwa milestone kwenye escrow account ya kile kiasi mlichokubariana, utafanya kazi akiridhika atairelease iingie kwenye akaunti yako ya freelancer then utaweza kukiwithdraw via aypal, skrill, bank wire na express (hii kwa tz haipo unless unatumia payoneer). Pia utakatwa 10% ya kiasi utakacholipwa.

Kuna mambo ya kufanya hivyo utatafuta ale unapohisi wewe una fit. Upwork, hii iko so professional, na kwasasa wamebadirisha kanuni zao na ni ngumu sana kusubmit profile ukakubariwa unless uwe umeitengeneza unique hawataki watu wenye vigezo sawa wacompete sana kwa kazi moja. Pia hawa kubid kazi inahitaji uwe na vitu vinaitwa connects ambazo unazinunua connects 10 ni $1.5 na kazi inaweza hitaji 1 to 10 connects kutegemea na ukubwa wa malipo. nao wanataka commission yoa ukishalipwa.

Fiverr unatengeneza profile na kitu kinaitwa jig then client akiwa interested atakufuata mwenyewe. Ukikomaa hasa ukajijua unafaa wapi zaidi utatengeneza pesa nzuri tu. Mfano mimi Freelacer natatengeneza si chini ya $800 kwa mwezi pia Upwork nako si chini ya $300. Lakini si kuanzia hapo nilianza natengeneza pesa ndogo kama lak tatu kwa mwezi kwa ujumla nikaenda napanda na kupata permanent clients. Freelancer nilishaacha kubid nina permanent clients muda wote.

Challenges
sometimes kwasababu nina permanent clients unakuta hawatengenezi milestone kitu ambacho muda mwingine uwa wananicheleweshea malipo hata baada ya kumaliza kazi lakini mara zote uwa wanalipa.

Challnege nyingine ni makato ya ktuoa ela maana paypal kwetu changamoto hivyo ninatumia payoneer au skrill lakini zaidi payoneer kwakuwa inawahi pokea pesa sometimes conversation rate kudraw kwa atm inakuwa chini sana.
Makosa wanayofanya freelancer wengi

watu wengi uwa wanahisi ni kazi rahisi kwamba eti mtu anaingia mtandao kama freelancer anakuta mtu eti anasema atype page ya pdf kwenye word alipwe 250$, jua hao matapeli wamejaa sana freelancer. kwa akili ya kawaida hakuna mtu atakulipa pesa ndefu hivyo kwa kuretype page na ukimchek aliyeweka tangazo hajaverify account, hajaverify payment method hana review wala nini.

Pia freelancing watu wanaichukulia labda ni sehemu ataenda apige ela nyingi faster, hapana hakuna free money una work for sometimes unalala hata saa tisa mfano mojawapo ya kazi ninazofanya ni kuwekea subtitles video za channels flan za mambo ya afya za daktari mmareknai za youtube ananitumia maneno mm nafanya kuya sync na video zake yaende sawa zinanifanya nalala late nights lakini uzuri analipa vizuri japo si sana lakini ela inaingia ukifanya video moja kila siku una hakika unalaza ela kadhaa.

Dropshipping
Hii naifanya Etsy. Hii ni soko zuri kwa wauzaji wa vitu vya asili kama nguo vitu vya ngozi na kadharika.
Affiliate markeeting

Hii ndipo nimeianza ambapo unaandika review za bidhaa kwa uhalisia wake yani unaandika ubra na ubaya wake pasipo kucopy amazon, mtu akisoma akavutiwa akaclick link akaenda amazon akanunua unakula commision.
karibu tujadiri
 
Shukrani mkuu, maelezo mazuri sana...tutafanyia kazi hayo.
 
Mkuu hii mambo ni poa sana but nimejaribu kote nachemka kupata kazi, I always do translations, kuna client mmoja alinicheki inbox na tukawa tunafanya kazi na ananilipa but through those network naona kwangu inakuwa changamoto,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii mambo ni poa sana but nimejaribu kote nachemka kupata kazi, I always do translations, kuna client mmoja alinicheki inbox na tukawa tunafanya kazi na ananilipa but through those network naona kwangu inakuwa changamoto,

Sent using Jamii Forums mobile app
changamoto kutoa pesa ua changamoto yako ni ipi
 
Kuuliza si ujinga wakuu naomba kujuzwa ukisha jiuinga na kuwa freelancer, nikazi za namna gani ambazo unakua unazifanya na hii inahusu watu wenye taaluma ipi au mtuyoyote anaweza ku participate. Natanguluza shukrani zangu za zati kwa atakae nisaidia kunielewesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuuliza si ujinga wakuu naomba kujuzwa ukisha jiuinga na kuwa freelancer, nikazi za namna gani ambazo unakua unazifanya na hii inahusu watu wenye taaluma ipi au mtuyoyote anaweza ku participate. Natanguluza shukrani zangu za zati kwa atakae nisaidia kunielewesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila aina ya kazi inayoweza kufanya remotely unayofikiria iko huko
 
Kuna uhaba wa ajira sana nchini jambo ambalolinapelekea vijana wengi kukosa ajira na mitaji japo wana elimu ambayo wanaweza kuitumia na wakatengeneza pesa zaidi hata kuliko ambayo wangelipwa.

............
....'Kuona wanawake mtoa adhabu ndiyo anaongeza kasi'... nikwambie mtoa mada kudhalilishwa falaghani hakubambi na ni rahisi kukanusha kwamba haujafanywa lolote, ila unapodhalilishwa mbele ya wanawake adhabu hupenya sawasawa hadi kwenye damu.

Ukisikia kazi ya jeshi, imejengwa na kanuni ya 3W's, yaani War,Women,Whysky.

Pombe sana, wanawake sana na vita basi.

Hauwezi kusajiliwa jeshini kama jongoo halipandi mtungi,maana yake wanawake hutumika kutoa kipimo cha ushindi(hapa maelezo ni mengi, ukitaka ntakupatia).
Hivyo usishangae sana kwa hilo, ni kawaida.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
....'Kuona wanawake mtoa adhabu ndiyo anaongeza kasi'... nikwambie mtoa mada kudhalilishwa falaghani hakubambi na ni rahisi kukanusha kwamba haujafanywa lolote, ila unapodhalilishwa mbele ya wanawake adhabu hupenya sawasawa hadi kwenye damu.

Ukisikia kazi ya jeshi, imejengwa na kanuni ya 3W's, yaani War,Women,Whysky.

Pombe sana, wanawake sana na vita basi.

Hauwezi kusajiliwa jeshini kama jongoo halipandi mtungi,maana yake wanawake hutumika kutoa kipimo cha ushindi(hapa maelezo ni mengi, ukitaka ntakupatia).
Hivyo usishangae sana kwa hilo, ni kawaida.


Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ina alcohol % ya ngapi mkuu?
 
Back
Top Bottom