Njia ya mbinguni

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Kuna muubiri mpya mjini kwetu alitaka mahitaji yake posta. Kwa jitihada zake za kutafuta Posta iliko akakwama hivyo hakuwa na jinsi zaidi ya kutafuta mwenyeji amuulize. Mazungumzo yakawa hivi:-
Muubiri: Habari zenu vijana
Vijana: Nzuri mzee, shikamoo
Muubiri: Marahaba, vijana mnaweza kunionyesha Posta iliko?
Vijana wakamwelekeza iliko posta.
Baada ya kumaliza shughuli zake akarudia njia ile ile na kuwakuta vijana wale wale. Akawashukuru na kuwaambia:-
Vijana asanteni kwa kunionyesha njia ya kwenda posta. Mimi ni muubiri na leo nitaubiri pale kwenye uwanja wa kuchezea mpira hivyo karibuni na nitawaonyesha njia ya kwenda MBINGUNI.
Vijana wakahamaki, du we mzee chizi nini, njia ya posta huijui utajuaje njia ya kwenda Mbinguni?
Wana JF je tumeonyeshana njia wiki hii?
Mbarikiwe sana na weekend njema.
 
This happened to Billy Graham in one of his evengelistic ministry in Europe. He personally shared this story to his friends!
 
Back
Top Bottom