Njia Tano (5) za Kutumia Kuwekeza Kwenye Ardhi/Nyumba Ukiwa na Mtaji Mdogo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Bahati ya kununua kiwanja/nyumba kwa bei nafuu sana imejengwa kwenye kanuni maalumu. Kwa kanuni hiyo ni lazima uweke juhudi kubwa. Juhudi kubwa ndiyo ndugu wa bahati ya kununua kiwanja au nyumba kwa bei nafuu.

Kumekuwa na ongezeko la thamani (bei) ya ardhi kila mwaka kutokana na kutokuwepo kwa uzalishaji wa ardhi katika nchi yoyote duniani. Ongezeko hili la bei limepelekea hofu kwa wawekezaji.

Pia, kuna majiji makubwa kama Dar Es Salaam ambayo soko la ardhi na majengo likikomaa miaka iliyopita ukilinganisha na mikoa mingine. Hivyo, bei za ardhi na majengo limekuwa juu kuliko uwezo wa wawekezaji kuanza kuwekeza kwenye majengo yanayolipa.

Changamoto hii inakuwa kubwa zaidi kwa wawekezaji wanaoanza kumiliki nyumba ya kwanza. Makosa unayoweza kufanya kwenye nyumba ya kwanza yanaweza kuwa kikwazo kikubwa cha mafanikio yako ya kifedha.

Hivyo makala hii ninaamini inaongezeka uelewa wa mafanikio ya kifedha kupitia umiliki wa kiwanja au nyumba kwa bei nafuu sana kwa kuzingatia bajeti yako.

Mwekezaji anafikiria endapo angenunua nyumba au kiwanja miaka 10 au 5 iliyopita angeweza kupata kwa bei nafuu sana. Mawazo yote hayo yatasaidia kitu kwa sababu bei ya viwanja haiwezi kushuka iendane na hali yako ya chini ya kifedha.

Tafadhali soma njia hizi za kukuwezesha kununua kiwanja au nyumba kwa bei nafuu sana.

Njia 5 Za Kuwekeza Kwenye Viwanja/Nyumba Kwa Mtaji Mdogo.

Moja.

Miliki Nyumba Kwa Kupangisha Na Kuishi Kwa Wakati Mmoja (House Hacking Strategy).

Mbinu ya kumiliki nyumba kwa ajili kuishi familia yako na kuipangisha kwa wakati mmoja ni mbinu ya gharama nafuu. Kwa mbinu hii utaweza kutumia kipato cha kodi na biashara/ajira yako kulingana na hali ya masoko ya mahali unapowekeza.

Ni kawaida kwa wawekezaji kumiliki nyumba ya kuishi tofauti na nyumba ya kupangisha. Kitendo hiki kinahitaji kiasi kikubwa cha mtaji fedha. Endapo una kiasi kidogo cha mtaji fedha, tafadhali jenga au nunua nyumba inayopangishika kwa faida.

Hivyo utatakiwa kufuata kanuni zote za ujenzi wa nyumba inayolipa wakati unajenga nyumba ya familia. Hii ni kwa sababu nyumba yako ya familia yako itakuwa inatumika pia kwa ajili ya upangishaji.

Kanuni ambazo zinaweza kukusaidia kumiliki kiwanja au nyumba zinazolipa sana ni kama ifuatavyo;-

✓ Kanuni ya 2%.

✓ Kanuni ya uwiano wa 100:10:3:1.

✓ Kanuni ya umbali wa kilomita 5:3:1.

✓ Kanuni ya ukarabati wa nyumba za kupangisha ya 4% ya jumla ya gharama za ukarabati na maboresho ya nyumba husika.

✓ Kanuni; nyumba inayopangishika kwa miezi 11 au zaidi kwa kila mwaka.

✓ Ni lazima uzingatie nguvu ya kiuchumi ya eneo husika, nguvu ya sera za serikali kuu na serikali za mtaa katika eneo husika, nguvu ya idadi ya watu na nguvu ya usanifu na mpangilio wa viwanja na majengo kwenye eneo husika. Vyote hivi vinatakiwa kuwa na matokeo chanya katika kipindi cha miaka 5 ijayo ya uwekezaji wako.

Mbili.

Kutumia Mbinu Ya Nyumba Za Kupangisha Itwaayo B-R-R-R-R.

Mbinu hii ni mbinu ya kuwekeza bila mkopo kwenye nyumba ya kwanza tu. Mbinu hii inafaa sana kwa ambao tayari wana fedha za kuwasaida wawekezaji ambao wana biashara iliyo rasmi na ajira za mikataba zaidi ya 5.

Pia, ni mbinu bora ya kumsaidia mwekezaji kutumia kiasi kidogo cha mtaji fedha kwa kuwekeza kwenye nyumba za kupangisha tu.

Tatu.

Wekeza Mkoa Mwingine.

Endapo mkoa wa Dar Es Salaam, Arusha, au Mwanza imekuwa kubwa kuliko uwezo wako wa kifedha hamia mkoa mwingine. Nenda kawekeze Dodoma, Singida, Morogoro au Kigoma na mikoa mingine.

Bei haziwezi kufanana kwenye mikoa tofauti na haiwezi kufanana kwa wilaya za kila mkoa utakaochagua. Una bahati kufahamu kanuni za uwekezaji kwenye ardhi na majengo kupitia makala zangu.

Kwa kutumia kanuni hizo hizo, utaweza kufanikiwa kwa kila mkoa utakaochagua kuanza kuwekeza kwa kutumia mtaji fedha ulionao. Wewe sio mti, fanya utafiti wa mkoa ambao ardhi na majengo huuzwa kwa bei nafuu.

Pia, kuna wilaya ambazo gharama za ujenzi huwa chini sana ukilinganisha na wilaya zingine kutokana na sababu kama vile;-

✓ Gharama ndogo za ufundi.

✓ Bei nafuu za mchanga, mawe, mbao, milango, na madirisha.

✓ Bei nafuu za uwekezaji wa umeme, maji na mifumo ya takataka.

✓ Uombaji wa vibali vya ujenzi.

Nne.

Wekeza kwenye aina tofauti ya majengo.

Katika kila wilaya au mkoa kuna aina fulani za majengo ambazo hulipa zaidi ukilinganisha na aina nyingine za majengo ya kupangisha. Mfano;-

✓ Majengo ya makazi ya vyumba chini ya 20 huingiza faida ndogo ukilinganisha na majengo ya biashara ya kupangisha katika jiji la Dar Es Salaam.

✓ Majengo ya kupangisha ya biashara (commercial real estate) huwa yanalipa zaidi kwa Jiji la Dar Es Salaam.

✓ Majengo ya makazi yameonyesha kuingiza faida kubwa kwa mkoa wa Dodoma kwa sababu matumizi mseto.

Hivyo kama ulipanga kumiliki nyumba za kupangisha za vyumba 5 vya kulala na umeona hailipi, wekeza kwenye nyumba za wageni. Kama nyumba za kulala wageni hazilipi, tafadhali hamishia jicho lako kwenye majengo ya familia ya kupangisha.

Endapo fremu za biashara ya hazilipi, hamishia jicho lako kwenye magodauni au stoo. Endapo magodauni/mabohari hayalipi, tafadhali hamishia jicho lako kwenye majengo ya hosteli za wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu.

Tano.

Tafuta Eneo Tofauti Na Mahali Ambapo Una Uzoefu.

Njia pekee ya kulifahamu soko mahalia la ardhi au nyumba unayotaka kuwekeza ni kutumia kanuni ya uwiano ya 150:30:3 kwa wawekezaji wapya wanaotaka kupima hali ya soko mahalia.

Tofauti na njia hii ni kujidanganya tu. Endapo imejihakikishia kuwa sehemu unapotaka kuwekeza hapalipi na ni gharama kuliko fedha ulinayo, hamishia majeshi yako mtaa, kata au wilaya nyingine. Kwa kufanya hivi utanufaika na mambo mawili;-

✓ Kukutana na soko mahalia ambalo linaendana na kiwango cha mtaji fedha ulionao.

✓ Kukutana na muuzaji wa kiwanja au nyumba mwenye hamasa kubwa.

Hizi ni njia ambazo unaweza kutumia ili kumiliki kiwanja au nyumba ya uwekezaji ambayo inaendana na mtaji fedha mdogo ulionao. Kwa makala zingine jiunge na huduma za kupokea makala zangu za uwekezaji kwenye ardhi na majengo kwa njia ya barua pepe (emails).

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.


Njoo uungane na FAMILIA YA TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa utapata taarifa na maarifa sahihi ya kujikwamua kwenye hali uliyonayo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom