Njia rahisi na salama ya kuondoa ufisadi mfumo

JUST

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
552
234
Habari mwana jf

hii mada ni mahususi kwa vijana wote wa kitanzania wenye uzalendo na nchi hii yenye neema kuliko nchi zote duniani.

Utangulizi:
Kwa siku za hivi karibuni tumekuwa tukisikia ama kuona watu wakipambana na kinachoitwa ufisadi ila katika mrengo kuibwa kwa fedha za umma. Mimi binafsi napinga pia ufisadi huu ila sisi vijana tumesahau ufisadi wa kimfumo unaompa fusra mtoto wa aliye nacho na kumnyima mtoto wa asiyenacho ambao kimsingi ni ufisadi unaoruhusu watu kuiba fedha kirahisi na bila ya kuchukuliwa hatua.

Kwa mfano kama baba ni mwenyekiti wa kijiji, shemeji wa baba ni msimamizi wa usalama wa kijiji, rafiki wa baba ni kaimu mwenyekiti alafu mtunza fedha ni rafiki wa mtoto wa baba, kwa hakika hakuna atakayesulubishwa kwa uwizi wa kosa la ubadhirifu wa fedha au mali za kijiji.


Namana ya kupambana na ufisadi mfumo:

Kama nilivyosema hapo awali ufisadi mfumo ndio chanzo cha ufisadi wowote ule. Mfumo wa kifisadi kwenye nchi ni kuwepo kwa njia za uendeshaji nchi ambao hauzingatii haki sawa kwa wote na taaluma katika shughuli za kila siku.

Swali la kujiuliza je tanzania ya leo kukitangazwa kazi ya mkurugenzi mfumo uliopo utaruhusu vigezo kutumika au utaruhuru uwezo wa familia utokayo? Jibu utakuwa nalo na kwa sasa lihifadhi moyoni mwako. Natumia mfumo wa kwenye ajira kwa sababu vijana wengi wanaomaliza eleimu ya chuo ndoto zao ni za kuajiriwa kwa sababu mfumo mwingine wa kifisadi wa elimu hauwapi fursa ya kujiajiri, ninapata mashaka kama vijana hawa watapata ajira kwa vigezo vya taaluma

katika hali hii ya kuwepo kwa mifumo mibovu ni rahisi kuiondoka kama vijana tutafanya yafuatayo:

1. Vijana wote tuachane na ushabiki wa kisiasa tusimame pamoja kama vijana na kudai vitu vitakavyosaidia vijana wote kwa ujumla.

2. Tuanze michakato ya kuchukua nafasi za juu za uongozi kama vijana kuanzai kwenye vyama vyetu tusikubali kuwapigia wazee kampeni watuongoze sababu vichwa vyao na akili zimepitwa na wakati na hawawezi kufikiria kwa kasi ya dunia ya sasa. Mbona nyerere alichukua nchi akiwa kijana, mbona gadafi ukiacha mapungufu yake amefanya makubwa akiwa kijana na wengine wengi.

3. Tuanzishe mijala ya kitaifa ya vijana kupitia makungamano warsha n.k. Najua zipo jitihada lakini sasa wigo wake uongezeke.

4. Vijana tuelewe kwamba chama ni njia ya kisiasa kuchukua uongozi na kamwe si njia ya kuleta maendeleo kwa vijana. Na pia kwa mfumo ulio safi kadi yako ya chama si kigezo cha kupata kazi au tenda na kama wako wanaofiki hivyo ndio maana ufisadi unaendelea sababu tuna viongozi waliotokana na chama na sio vigezo

maoni:

Vijana tuamke tusikubali kuwa makarai ya kubebea zege, wakati ni wetu tunao uwezo wa kuchukua nchi umri usiwe kigezo cha kutuondoa kwenye sehemu za maamuzi.

Nawakilisha.

4.
 
Nafikiri umesahau kwamba kwenye demokrasia ushindani wa kisiasa wa vyama vya siasa ni muhimu ila bila ya kuwepo vyama vya kijamii katika demokrasia hii ni tatizo lingine.

vijana wengi wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa na kufkiri siasa vya vyama vya siasa kupitia uchaguzi ndiyo njia pekee ya kimaendeleo na kusahau umuhimu na jukumu muhimu la vyama shirikishi vya kijamii katika kusimamia majukumu ya serikali katika ngazi zote na kuleta hoja katika vyama vya siasa zitazotumika kitaifa. Nguvu ya vijana ipelekwe katika kuanzisha na kujiunga na hizi pressure groups kwani uongozi siyo wa siasa za uchaguzi pekee.
Vijana wasikuli kuac
 
Nafikiri umesahau kwamba kwenye demokrasia ushindani wa kisiasa wa vyama vya siasa ni muhimu ila bila ya kuwepo vyama vya kijamii katika demokrasia hii ni tatizo lingine.

vijana wengi wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa na kufkiri siasa vya vyama vya siasa kupitia uchaguzi ndiyo njia pekee ya kimaendeleo na kusahau umuhimu na jukumu muhimu la vyama shirikishi vya kijamii katika kusimamia majukumu ya serikali katika ngazi zote na kuleta hoja katika vyama vya siasa zitazotumika kitaifa. Nguvu ya vijana ipelekwe katika kuanzisha na kujiunga na hizi pressure groups kwani uongozi siyo wa siasa za uchaguzi pekee.
Vijana wasikuli kuac

nakubaliana na wewe na hilo ni tatizo kwa vijana wa kitanzania si unaona hata uchangiaji wa hii mada umepoa ila ningeweka mada ya kisiasa uchangiaji ungekuwa mkubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom