Njeru Kasaka: Unafiki wa WanaCCM Unaua Taifa

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Mkongwe na mmoja ya watu muhimu katika ujio wa mahitaji ya siasa za kisasa Nchini Tanzania Mzee Njeru Kasaka leo katika gazeti la Raia Mwema tarehe 11 January 2012.Ametoa makala yenye ujumbe mzito sana kwa Wanacccm wenzie kubadilika na kuacha siasa za FITINA [angekuwepo Mwalimu angeita Mizengwe].Mzee huyu anasema CCM ikiyumba maana yake na Nchi inayumba,hivyo siasa za kinafiki ndani ya CCM zina zaa UNAFIKI wa kwa TAIFA zima.

Katika Makala hiyo nzito iliyoshiba Mzee huyo maalufu sana miaka ya nyuma enzi hizo ndani ya Bunge kama mmoja wa kundi la G55.Amesema dunia ubadilika kutokana dhamila ya binadamu ambayo upelekea Mwanadamu kuitaji mambo mapya yenye kumzunguka anasema dhamira ilimfanya Mandera kwa kuzipinga sheria za kibaguzi za africa kusini.Hivyo dhamira mpya miongoni mwetu ndio chahchu za maendeleo na ustaarabu wa jamii.Kugandamiza dhamira na chipukio ya mambo mpya na kugangania uzamani uzalisha unafiki.

Anaseme sasa kumzeuka suala jingine ndani ya CCM,suala hilo ni unafiki.anasema unafaki sio kitu kizuri kuna viongozi wameanza kuulea na kueendeleza.Kwa mfano wakati wa kula za maoni baadhi ya viongozi wao binafsi kwa makusudi wanahamua kumuhujumu mmoja wa wagombea na kumpa ushindi mwingine ambae hakustahiki kwa sababu wanazojua wenyewe.

Hayo uendele kwa kujenga miafaka dhidi ya mdhaulumiwa na mshindi kwa vigezo vya kujenga chama uku mioyoni mwao wanavinyongo tele, ingawa kwa kufanya hivyo uonyesha jamii kuwa wamekomaa kiasasa.Wengi waliofikaw na mambo haya uendeleea kunungunika pembeni.

anasema mifarakano inayoendelea kwa sasa ndani ya CCm ni ishara kuwa UNAFIKI umefika kikomo.kwani katika zama za sasa za utandawazi [Pata picha ya Jammi forum wazo binafsi sio la Mzee Njeru] na uhuru wa vyombo vya habari hakuna taasisi inaweza kudumu kwa kujikita kwenye UNAFIKI na UDANGANYIFU.

"Unaweza kuwadanganya watu waote kwa muda,lakini uwezi kuwadanganya watu wote muda wote"... anasema leo kuna kila dalilil ya CCM kufumbia macho maovu wanayotendewa baadhi ya wanachama wake na viongozi wake.Upendeleo na hujuma ni mambo yasiyofichika.Kiongozi akishabikia waliotoa rushwa walizidiana ni lughaya kuhalalisha rushwa katika chaguzi za chama

Viongzoi wakikumbwa na mmomonyoko wa maadili [RUSHWA,UFISADI NA UNAFIKI] Taifa linakumbwa na mkanganyiko na mustakabali wake haueleweki.Viongozi ndio muhimili wa mustakabali waTaifa hasa katika Nchi kama Tanzania.ansema tujifunze kutoka Somalia.Ansema Naigeria imetumbukia kwenye matatizo kwa viongozi kwa kutokuchua hatua mapema dhidi ya UFISADI,UKABILA,UDINI,RUSHWA na kutotenda haki kwa baadhi ya jamii na maeneo ya baadhi ya Nchi
 
Huyu nae kuna wakati alichanganyikiwa akakimbilia CUF kwa muda mfupi !!!!
 
napata wakati mgumu sana kuwaamini watu ambao wameyaona maovu mara baada aya wao kutoka madarakani.haya yote anayoyasema siyo mageni yalikuwepo hata siku zake yeye lakini alikaa kimya leo hii ameamka usingizini ghafla.
 
kikwete nae siku akitoka madarakani atakuja kuzungumza ukweli lkn leo hawezi sema matatizo yaliyopo kiuhalisia sababu yanamhusu, maana lowasa na sumaye eti wanaona matatizo na kuyaelezea pumbaff
 
Njelu kasaka yupo sahihi. Viongozi wa CCM ni wanafiki sana, na hii ni sumu kwa CCM kwani unafiki huu hudumu wakati wahusika wakiwa kwenye uongozi tu kwenye madaraka, ni kawaida yao kuja na msimamo tofauti kabisa. Sote tunafahamu jinsi gani viongozi wakuu katika CCM, jinsi gani walikuwa wapo tayari kuhamia Chadema ili mradi tu wapate uongozi/madaraka, lakini baada ya kupata madaraka hayo ndani ya CCM, wakisikia mtu yoyote ndani ya CCM ana msimamo wa aina hiyo, basi huyo ni adui wa kuogopa kama ukoma. CCM Oyeeeeeeee.
 
mwenzie philip marmo alipewa uwaziri kwa mda mrefu,yeye alipomwagwa ccm akaanza kuwaona wabaya
 
napata wakati mgumu sana kuwaamini watu ambao wameyaona maovu mara baada aya wao kutoka madarakani.haya yote anayoyasema siyo mageni yalikuwepo hata siku zake yeye lakini alikaa kimya leo hii ameamka usingizini ghafla.

Mkuu huyu mzee alikuwa kichwa sana japo kwa wakati ule alionekana mkolofi yeye na wenzie walianzisha kikundi kinaitwa G55 kilichokuwa kinataka kama sikosei Serikali Tatu yani Tanganyika,Zanzibar na Serikali ya Muungano,wakakumbana na Rungu la Mwalimu kwa kuzidiwa hoja japo walikuwa na wazo zuri sema walishindwa kulitete kwa hoja madhubuti hata walipobanwa na Mwalimu hoja yao ilishindwa kujisimamia yenyewe.Nampenda kwa kuwa yeye na wenzie japo walijitahidi kusimama na sio UNAFIKI wa kusimama na kusema NDIO wakati moyoni unasema HAPANA.
 
Mkuu huyu mzee alikuwa kichwa sana japo kwa wakati ule alionekana mkolofi yeye na wenzie walianzisha kikundi kinaitwa G8 kilichokuwa kinataka kama sikosei Serikali Tatu yani Tanganyika,Zanzibar na Serikali ya Muungano,wakakumbana na Rungu la Mwalimu kwa kuzidiwa hoja japo walikuwa na wazo zuri sema walishindwa kulitete kwa hoja madhubuti hata walipobanwa na Mwalimu hoja yao ilishindwa kujisimamia yenyewe.Nampenda kwa kuwa yeye na wenzie japo walijitahidi kusimama na sio UNAFIKI wa kusimama na kusema NDIO wakati moyoni unasema HAPANA.

Mkuu penye G8 rekebisha ni G55
 
Mkuu huyu mzee alikuwa kichwa sana japo kwa wakati ule alionekana mkolofi yeye na wenzie walianzisha kikundi kinaitwa G55 kilichokuwa kinataka kama sikosei Serikali Tatu yani Tanganyika,Zanzibar na Serikali ya Muungano,wakakumbana na Rungu la Mwalimu kwa kuzidiwa hoja japo walikuwa na wazo zuri sema walishindwa kulitete kwa hoja madhubuti hata walipobanwa na Mwalimu hoja yao ilishindwa kujisimamia yenyewe.Nampenda kwa kuwa yeye na wenzie japo walijitahidi kusimama na sio UNAFIKI wa kusimama na kusema NDIO wakati moyoni unasema HAPANA.

Hakuna mtu mnafiki na mpenda madaraka kama Kasaka. Kuwa katika kundi la G55 bado hakujanishwawishi kumkubali Kasaka. Anayoongea hadharani si anayotenda iwe kwa jamii ama kwa familia yake. Alikimbilia CUF baada ya CCM kumwengua ama kumyima nafasi ya kugombea ubunge, alipokosa ubunge huko CUF akarudi CCM, huo ni upuuzi na kukosa msimamo.
Aliniacha hoi wakati mdogo wake alivyofariki na kuacha mke na watoto wawili wadogo wenye umri wa miaka 17 na 14. Kasaka alichukua mali zote za marehemu mdogo wake ikiwa ni pamoja na nyumba mbili (moja Sinza na nyingine Kimara), Mashamba mawili moja Mbeya na lingine Morogoro huku akiwafukuza watoto wa marehemu na mjane kwamba wakapange nyumba.
Mahakama iliingilia kati baada ya mjane kutoa wosia na maandishi ya marehemu kuonesha kwamba mali zote ni mali ya watoto na mjane huyo, bado hili zee liling'ang'ania mali hizo mpaka wazee wa kimila na wakuu wa serikali walivyoingilia kati ndiyo lilipowarudishia wahusika mali hizo. Katika kipindi cha kesi hii familia ya marehemu ilipata shida sana tokana na tamaa za fisi za hili zee. Ni mtu mnafiki na mwenye tamaa sana.
 
Kasaka alihoji serikali ya Tanganyika imefia wapi....Yaliyo mkuta, hana hamu.
Binafsi nataka kujua nchi ya Tanganyika iko wapi, na ndio nchi iliyopata uhuru siku kama ya leo 1961.
Nchi yenye bendera hii imeishia wapi!
1200px-Flag_of_Tanganyika.svg.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom